Wednesday, 11 February 2015

MKUYA KUWATETEA WANAOMILKI MABILIONI USWISI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akitafakari jambo

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, amesema siyo haramu kwa Watanzania kuweka fedha nje hivyo, Watanzania 99 waliotajwa kuwa na akaunti Uswisi haimaanishi wote wametorosha fedha.
        
         Hata hivyo, amsema serikali inaangalia ripoti ya Swiss Leaks ili kuona uhalali wa akaunti hizo za siri.  
         “Sisi hatujaona kama ni kosa kwa Watanzania kuwekeza fedha zao kwenye mabenki ya nje na wala isionekane kama ni jambo haramu kabisa. 
        Kama serikali tungetamani wawekeze kwenye benki nchini ili kukuza sekta ya fedha lakini pia hatuwafungi kutowekeza nje,” alisema.
         “Tunachofanya ni kuiangalia hiyo ripoti ili kujua ukweli wa taarifa hizo, lakini taarifa hiyo haimaanishi kwamba ni kosa kubwa kisheria kwa Mtanzania kuweka fedha nje,” alisema.
        Mkuya alisisitiza kuwa hakuna shida yoyote kwa Watanzania kuweka fedha kwenye akaunti nje ya nchi.
         Waziri Mkuya ameyasema hayo siku moja tu baada ya vyombo vya habari nchini kuripoti taarifa ya kuwapo vigogo 99 wa Tanzania kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi kutokana na ripoti ya mtandao wa Swiss Leaks chini ya Waandishi wa Habari za Uchunguzi wa Kimataifa (ICIJ).
        Taarifa ya Swiss Leaks iliyotolewa juzi Jumapili, inaonyesha kuwa vigogo hao wa Tanzania wana akaunti za siri zenye Dola za Marekani milioni 114 ambazo ni sawa na Sh. bilioni 199.6.
          Msingi wa ripoti hiyo umetokana na aliyekuwa mfanyakazi wa benki ya kimataifa HSBC, HervĂ© Falciani, kuvujisha siri za akaunti za wateja baada ya kuacha kazi; na mwaka 2008, alivujisha siri za akaunti za siri za baadhi ya watumishi wa umma na wanasiasa kwa Serikali ya Ufaransa ambayo mamlaka za kodi nchini humo ilifanya uchunguzi na kuthibitisha.
Ripoti hiyo ya Swiss Leaks, inaeleza kuwa taarifa za kiuchunguzi kutoka benki ya  HSBC nchini Uswisi zinaonyesha kuwa akaunti hizo zinahusishwa na baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara wakubwa na watumishi wa umma ambao wamejipatia utajiri wa siri unaotokana na kampuni hewa (offshore companies)

No comments:

Post a Comment