Pichani niKatibu Mkuu wa Baraza la Mitiani nchini NECTA Dkt Charles E Msonde Akizungumza leo na Waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam |
BARAZA la
Mitihani nchini NECTA limetangaza matokea ya kidato cha pili yaliyofanyika
mwaka jana 2014 huku idadi kubwa ya wanafunzi wakiwa wamefaulu na kujiunga kidato cha
tatu, ikiongeza kwa asilimia 92.66 ikilinganisha na mwaka 2013 ambapo idadi ya
wanafunzi waliofaulu ilikuwa asilimia 89.34.
Matokeo hayo yametangazwa leo Jijini Dar
es Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitiani nchini NECTA Dkt Charles E Msonde
wakati wa mkutano na waandishi wa Habari ambapo alisema watahiniwa waliofanya mtiani huo uliofanyika mwezi
Novemba mwaka jana ilikuwa 405,204 sawa na asilimia 89.40 Kati ya hao wasichana
walikuwa 233,834 sawa na asilimia 51.60 na wavulana walikuwa 219,357 sawa na aslimia 48.40.
Dkt Msonde alisema kati ya watahiniwa hao
waliofaulu na kupata alama na kuweza kuendelea na kidato cha tatu walikuwa
375,434 Sawa na asilimia 92.6 ya watahiwa wote waliofanya mtihani huo ambapo wasichana
walikuwa 195,328 sawa na asilimia 92.8 na wavulana 180106 sawa na aslimia
92.69.
Aidha,Dokt Msonde aliwataja watahiniwa
ambao wamepata alama ambazo hawawezi kuendelea na kidato cha Tatu na itawanalazimu kurudia kidato cha pili
walikuwa 29770 kati ya asilimia 7.34.
Vilevile ,Dokta Msonde alitaja masomo yaliyofanya vizuri ikiwa i pamoja na historia geography kiswahili na english
Wana habari wakiwa katika mkutano
Pia Masomo waliofanya vibaya watahiniwa hao ni
ya Hesabu,Kemia,kilimo,Somo la Biashara
pamoja na Biolojia.
Alibanisha
kuwa sababu iliofanya idadi ya wanafunzi mwaka huu kuwa mazuri imetokana na mipango mizuri ya serikali huku
ikizingatia sasa kuwepo na mfumo mpya wa matokea mkubwa sasa na akawata walimu
na wazazi waendele kutoa mshikamano kwa walimu.
Matokeo yote
ya Kidato cha pili yatakuwepo kwenye Mtandao wa baraza la Mitiani nchini,tovuti
ya Wizara ya Elimu na Ofisi ya Wzari Mkuu Tamisemi, pamoja na Kwenye shule
husika ya Mwanafunzi anayesoma.
No comments:
Post a Comment