Tuesday, 20 January 2015

Aunty Achukizwa na Uamuzi wa King Majuto!


Aunty Achukizwa na Uamuzi wa King Majuto!
Wakati mwigizaji mkongwe wa filamu za vichekesho, King Majuto akidai kutoshiriki kazi na msanii yeyote kutokana na kuibiwa, msanii mwenzake, Aunty Ezekiel amechukizwa na uamuzi huo.


Akizungumza na GPL, Aunty alisema kuwa haamini kama wezi wa kazi zake ndiyo chanzo cha Majuto kuachana na filamu za kushirikishwa bali inawezekana kuna tatizo lake lingine
“Suala la wezi lipo miaka mingi na kama mkongwe na mpenda maendeleo alitakiwa kusimama maana kila mmoja akisema achukue uamuzi kama huo ni wazi kwamba kutakuwa hakuna msanii tena Tanzania,” alisema.

No comments:

Post a Comment