Na Karoli Vinsent
SIRI ya kusalitiwa kwa Wajumbe wanaunda Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA yafichuka mtandao umegundua,Siri hiyo inakuja siku moja kupita baada ya Baadhi ya Wajumbe wakiwemo , John Shibuda mbunge wa (Maswa Magharibi), Said Arfi mbunge wa (Mpanda Mjini) na Leticia Nyerere mbunge wa (Viti Maalum) kuridhia kushiriki vikao vya Bunge Maalum.
Wajumbe hao wote wanatoka kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, ambao wamekwenda kinyume umoja huo wa UKAWA,ambao ni muunganiko wa vyama Vikuu vya upinzani nchini ambavyo ni Chadema,NCCR,CUF,ND
Pamoja na Baadhi ya wajumbe 201 waliochaguliwa na Rais Kikwete,ambao wote kwa pamoja walifikia maadhimio ya kutorejea kwenye Bunge hilo kwa kile wanachokisema mchakato huo umetekwa na Chama cha Mapinduzi CCM.
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata zinasema Ulafi,Tamaa ya Madaraka pamoja na kutokomaa kisiasa ni miongoni mwa sababu iliowafanya wajumbe hao kuwasaliti wenzao ambao wenye Malengo ya kuwatetea wananchi wa Tanzania.
Taarifa hiyo inasema kwa upande wa Mjumbe Leticia Nyerere ni Tamaa ya madaraka imemfanya awapige chini na kupuuza uongozi wa chama chake cha Chadema na kurejea kwenye bunge hilo.
Akithibitisha hayo Rafiki wa Karibu wa mwanamama huyo Leticia nyerere,ambaye aliomba mtandao huu usilitaje Jina lake, alisema mama huyo amepewa ahadi nyingi sana na Chama cha Mapinduzi CCM,ikiwemo ukuu wa Mkoa.
“Mimi mwenyewe nilijua tu lazima Rafiki yangu atarejea kwenye Bunge hilo,maana anataka sana uongozi huyo,nasikia amehaidiwa vitu vingi sana ikiwemo hata Ukuu wa Mkoa na CCM wewe unafikiri mchezo nakwambia huyo lazima afanye hivyo”
“Anajua Chadema lazima wamfukuze tu,kutokana na ugeugeu aliokuwa nao,na yeye anakwenda zake CCM,anafikiri atapewa utawala huo”kilisema chanzo hicho ambacho ni karibu sana na Leticia Nyerere.
Kwa upande Mjumbe mwengine ambaye ameusaliti umoja huo, John Shibuda ni Mbunge wa Maswa Magharibi CHADEMA,naye alionekana wiki hii kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma na kusaini sehemu ya maudhurio na tayari kulipwa na posho.
“Shibuda alikuja ofisini kwangu huku mguu wake ukionekana kuwa umevimba hivyo akaomba ruhusa kwenda kupatiwa matibabu, lakini hao wengine wamejiandikisha tu na kuondoka hata hivyo hawajaonekana tena,”alisema.
Duru za Kisiasa zinasema John Shibuda alitabiliwa tu kati ya watu wangewasaliti Ukawa shibuda ni mtu wa kwanza kutokana na kutokomaa kisiasa.
Shibuda ,ambaye aliwahi kutajwa kipindi cha nyuma na Makada wa chadema waliofunguliwa Kesi ya Ugaidi na Serikali,kwamba ni miongoni mwa watu waliokuwa wanafanikisha kesi hiyo ya kubambikiziwa ya Ugaidi kwa makada hao,ambapo Shibuda alitajwa kushirikiana na Meya wa Ilemela, Henry Matata kutengeneza Hujuma hiyo.
Lakini shibuda alibuka na kukanusha kwamba taarifa hizo na kusema sio za kweli,lakini licha ya kukanusha taarifa hizo Mwanasiasa huyo anehamahama vyama kila kukicha alionekana mara kwa mra kwenye majukwaa ya chama cha Mapinduzi CCM,akisema vibaya chama chake cha Chadema,na kupelekea kufukuzwa kwenye vikao vya ndani vya chama hicho kutokana na usaliti wake,
Duru hizo ziliziidi kusema kwa siasa za ovyo alizokuwanazo John Shibuda ni Ishara tosha kwamba Tanzania ina wakati mgumu sana kujijenga Upinzani,na kitendo alichokionyesha wiki hii ni wakati chama Chake kichukue maamuzi magumu ikiwemo kumfukuza hata uanachama.
Mwandishi wa Mtandao huu,alimpotafuta katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa kuhusu ugeugeu huu unaofanywa na wajumbe wanaotoka chama hicho kuwasaliti na kurejea kwenye Bunge hilo ambapo alisema kuhusu Said Arfi (Mpanda Mjini) huyo awezi kumzungumzia na kumtaka mwandishi wa Mtandao huu kuwasiliana na Uongozi wa Chadema Mpanda atapata Taarifa kamali.
Na,alipoulizwa kuhusu mjumbe mwingine John Shibuda,Katibu huyo alizidi kusema Shibuda anajulikana kwa tabia yake ya usaliti na chama hicho kinapanga kumchukulia hatua kali ikithibitika kwamba amefanya usaliti huo.
“Kuhusu Leticia Nyerere siwezi kulizungumzia mwandishi, na bado hatujathibitisha na tumesoma kwenye magazeti inasemekana amesaini tu,na tulivyomtafuta kwenye simu sisi kama chadema akasema hayupo Dodoma ila amesaini kwahiyo siwezi kulisema hilo,kuhusu Shibuda huyo anajulikana kwa siasa zake za ovyo tu na chama akiwezi kumvumilia mtu kama huyo na tutamchukulia hatua kali sahivi”alisema Slaa
No comments:
Post a Comment