Na Karoli
Vinsent
MWENYEKITI
wa Chama cha NCCR Mageuzi Jems Mbatia amesema chama chake,hakitamvumila mjumbe ambaye atausaliti Umoja wa Kutetea katiba ya
Wananchi UKAWA na kurejea kwenye Vikao vya Bunge Maalum la katiba,basi kama akitokea
chama hicho kitamchukulia hatua kali sana.
Kauli hiyo ya Jemsi Mbatia
ameitoa ,Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anaongea Wajumbe wa
Mkutano mkuu wa Chama cha NCCR mageuzi kuhusu mipango mbalimbali ya kukijenga
chama hicho,ambapo Mbatia alitumia nafasi hiyo kuwasihi wajumbe wanaotoka chama
chake kuachana kabisa na mipango ya kurejea kwenye Bunge hilo kwa madai
mchakato wa katiba umujumiwa na CCM.
Na endapo ikitokea mjumbe ambaye
atakwenda kinyume na kurejea kwenye Bunge Maalum La Katiba basi atakuwa
amejifukuzisha mwenyewe kwenye Chama hicho.
“Ngoja kabisa niseme endapo Mjumbe
yeyote anayetokana na Umoja huu wa Ukawa
anayetoka chama NCCR Mageuzi akirejea kwenye Bunge hilo basi ajue kabisa chama
hakitamvumilia na kitamchukulia hatua kali sana ya Kinidhamu ikiwezekana hata
kumfukuza kabisa,maana atakuwa amekwenda kinyume na mapendekezo ya Chama chetu”alisema
Mbatia
Kauli hiyo ambayo iliungwa na
Wajumbe wote wa Chama hico waliokuwepo Ukumbini hapo na kuitikia wote kwa sauti
moja kwamba mjumbe yeyote kutoka chama cha NCCR mageuzi basi ajue atakuwa
amejifukuzisha mwenyewe.
Mbatia ambaye naye ni Mjumbe wa
Bunge Maalum la katiba alisema Umoja huo wa ukawa hauwezi kukatishwa Tamaa na
wajumbe wachache walioasi na kurejea kwenye Bungeni,kwani yeye anajua tama ya
fedha ndiyo iliyowapeleka huko.
“Tumeona jinsi wajumbe wachache
wa Ukawa ambao wametusaliti na kurejea Bungeni juzi na wajumbe hao wametoka
kwenye chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na wamefanya hivyo hao wajumbe
ni tamaa za pesa ndizo zimawarudisha bungeni tu na wala hawakuwa teyali
kuwatetea wananchi na sisi hatuwezi kukatishwa na watu hao”alizidi kusema Mbatia
Vilevile Mbatia alitumia nafasi
hiyo kumshambaulia Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta,na kusema
ndiye mtu ambaye anafaa kulaumiwa kutokana na yeye kusimamia upotevu wa
Mabilioni ya Watanzania huku akijua Katiba haiwezi kupatika.
Mbatia ambaye vilevile ni Mbunge
wa kuteuliwa na Rais alizidi kusema Bunge hilo linafanya ufisadi wa kutisha
kwenye pesa za Watanzania.
“Jamani nchii hii ni masikini
leo ukipita mjini balabala ni mbovu,lakini Sitta anaendelea kusimamia Bunge la
katiba ambalo limejaa ufisadi wa kutisha,haiwezekani kabisa bunge hili la
katiba vipaza sauti tu kwa siku vinatumia milioni tisa,jamani Sitta haoni huu
wizi kweli?”
“Leo wajumbe walioko huku
bungeni wanatupigia simu na kusema mnakosa pesa ,eti wanasema hivyo kutokana na
wao wamefuta jumamosi na jumapili kwenye ratiba za bunge maalum,badala yake
wamejingezea siku sitini,yaani maana yake kila mbunge ataondoka kwa kwenye
vikao hivi zaidi ya milioni 27 huku wakijua katiba haitopatikana kutokana na
kutokuwa 2ya 3”alizidi kuhoji Mbatia
Katika hatua nyingine Chama
hicho kimezidi kumuomba Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge maalum la Katiba
kutokana na kukosa sifa ya kuendelea kwake badala yake wameomba katiba iliyopo
iendelee na kupisha uchaguzi mkuuu na katiba hiyo ya zamani ifanyiwe
marekebisho ikiwemo kuwepo na kipengere cha tume huru ya Uchaguzi,pamoja na
umri wa mgombea wa Urais upunguzwe,
Na uchaguzi mkuu ukikamilika basi mchakato wa
katiba mpya uendelee.Ukawa ni muunganiko wa vya Vikuu vya Upinzani ikiwemo CHADEMA,
CUF na NCCR-Mageuzi pamoja na Baadhi ya wajumbe 201 waliochaguliwa na Rais
Kikwete wamesusia vikao hivyo kwa madai mchakato huo umehujumiwa na CCM.
Click here to Reply or Forward
|
No comments:
Post a Comment