Na Karoli
Vinsent
SABABU za
Mtangazaji Maarufu wa Kipindi cha Michezo na Burudani Maulidi Kitenge kuipiga Chini Redio one na Kuamia Redio mpya E.fm 93.7 ya hapa Dar Es
Salaam, sasa sababu zaanza
kufichuka,Mtandao huu Umedokezwa Sababu hiyo
Maulidi
Kitenge ambaye ametanga rasmi mwanzoni mwa wiki hii kupitia mtandao wake wakijamii wa facebook kwamba Miaka 14 aliyokaa
redio na Kituo cha Tv cha Itv inatosha yeye kukaa mjengoni hapo na tena yeye
kushindwa kuweka wazi sababu ya kuondoka hapo na kuondokea kwenye kituo kipya
cha Redio cha E.fm 93.7 Dar Es Salaam,
Taarifa za kuaminika Ambazo Mtandao huu
umedokezwa kutoka kwenye Vyanzo mbalimbali vilivyopo hapo E.FM Redio pamoja
na Radio one zinasema sababu iliyomfanya
aondoke hapo ndio sababu ambayo inahisiwa ndio itakayowafanya Watangazaji wengi waondoke
Redio one.
Akielezea
Sababu hiyo,Mfanyakazi wa kituo redio cha Efm, alichohaamia Kitenge ambaye
hakutaka Jina lake litajwe Mtandaoni alisema mtangazaji huyo amekosa uhuru ndio ikapelekea
kutoelewana na mabosi zake.
“Da ni kweli Kitenge sahivi ni
mfanyakazi Mwenzetu na teyali kasaini Mkataba,ila sababu iliyomfanya aondoke
pale Redio one,inatoka na y eye kuhusika katika kutengeneza Tangazo linalohusu Ujio wa Timu ya Wazee wa
Realmadrid ambao watakuja Tanzania wiki ijayo,sasa baada ya kutengeneza Tangazo
lile Viongozi Radio one wakakasilika kwa yeye kutengeneza Tangazo linalohusu
redio nyingine tena kwenye Studio tofauti na hapo”alisema mpashaji huyo
Chanzo hicho kilizidi kusema
mara baada ya kitenge kutengeneza Tangazo hilo aliitwa kujitetea na Mabosi wa Redio one,lakini yeye alionekana kama
anakosa Uhuru kutokana na kuingiliwa hata sehemu zengine ambazo hazihususiani
na kazi yake kutokana na kufanya kazi pale inapohitajika,ndipo akachukua
maamuzi ya kuachana Redio hiyo.
Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta
Mkurugenzi wa Redio One Deogratus Rweyunga na kutaka kujua ukweli wa taarifa
hizi,ambapo Rweyunga alimtaka Mwandishi wa Mtandao huu amtafute Kitenge
mwenyewe na kuzidi kusema yeye hana ugomvi na kitenge.
“Hebu sikiliza Mtafute Kitenge
mwenyewe,maana yeye kwenda kwenye Redio hiyo ni changamoto zengine na
tunamtakia maisha mema na sisi hatuna ugomvi na kitenge kaamua kuacha kazi hapa
ni sawa yeye ameona ni sahihi,na harafu unaposema Tangazo hilo alilotengeneza ndio
imetufanya tukasilike na tumfukuze kazi sio kweli kwani mbona yeye katengeneza
matangazo mengi ikiwemoa Tamasha la matumaini atujakasilika na limepigwa Redio
nyingi sana na hatujamfukuza iweje leo ”alisema Rweyunga
Mwandishi wa Mtandao huu alipomtafuta kitenge
kujua ukweli wa Taarifa hizo hakuweza kupatikana mara moja kutokana na
kutopatikana kwenye simu,
Sababu hiyo ya kitenge Kuondoa Redio
one iliwai kutolewa mara kwa mara kwa
Watangazi waliohama hapo wakisema wanakosa
Uhuru wanapokuwa kwenye Redio hiyo.
No comments:
Post a Comment