Kamanda wa polisi kanda maalum Suleiman Kova akimuonyesha polisi feki wa usalama barabarani [kushoto] aliyevaa sare za polisi barabarani [traffic]
Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es
Salaam linamshikilia na kumhoji mtu mmoja aitwaye ROBSON S/O SEIF MWAKYUSA
EMMANUEL, miaka 30, Mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za
kujifanya afisa wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani akiendelea na kazi za
ukaguzi wa makosa ya usalama barabarani
Mtuhumiwa huyu alikamatwa tarehe
02/08/2014 huko Kata ya Chamazi, Mbagala Majimatitu Mkoa wa Kipolisi Temeke akiwa
amevalia sare za Polisi na cheo cha Stesheni Sajenti.
Baada ya kukamatwa alikutwa
na gari namba T723 BAK T/Cresta rangi nyeupe analilotumia kuzunguka maeneo
mbalimbali ya jiji kutapeli watu akiwadanganya yeye ni askari polisi. Gari hilo
lilipopekuliwa lilikutwa na....................
·
Radio
Call 1yenye namba GP380 aina ya Motorola
·
Leseni
za udereva zipatazo 40 za watu mbalimbali
·
Stakabadhi
02 za Serikali zenye nambari A0531562 na A1672464
·
Police
Loss Report mbalimbali.
·
Nakala
03 za Notification zilizojazwa.
·
Kofia
moja ya (Uhuru Cape) ya Usalama barabarani,
·
Beji
01 yenye jina la E.R. MWAKYUSA ya kuweka kifuani.
·
Ratiba
ya mabasi yaendayo Mikoani ya SUMATRA
Pia mtuhumiwa
alipekuliwa nyumbani kwake alikutwa na vitu vifuatavyo:
·
Pea
04 za sare ya Polisi ya KAKI.
·
Pea
03 za sare ya Polisi ya Usalama Barabarani
·
Koti
01 ya mvua ya Usalama Barabarani
·
Reflector
08 za Usalama Barabarani
·
Kofia
01 (Uhuru Cape) ya Usalama Barabarani
·
Kofia
02 (Barret) nyeusi za Polisi
·
Mikanda
02 ya Bendera mali ya Jeshi la Polisi
·
Mikanda
02 ya Polisi (Tunic Cross Belt) mweusi.
·
Mikanda
02 ya Filimbi.
·
Cheo
01 cha Sajenti
·
Vyeo
03 vya Stesheni Sajenti.
·
Vifungi
08 vya chuma mali ya Jeshi la Polisi.
·
Cheo
01 cha Stesheni Sajenti cha JWTZ
·
Notification
Form zilizojazwa zipatazo 62.
·
PF3
Forms zipatazo 04
·
Notification
Forms ambazo hazijajazwa zipatazo 08
Mtuhumiwa huyu
aliwahi kuwa askari polisi aliyejiunga na Jeshi hilo Mwaka 2000 akiwa mwenye
namba F2460 lakini alifukuzwa kazi kwa fedheha mnamo tarehe 21/03/2014 huko
Kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha Stesheni Sajenti.
Uchunguzi wa awali
unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akijitambulisha kuwa ni askari hivyo
kufanikiwa kuwatapeli wananchi mbalimbali na kujipatia kiasi kikubwa fedha kwa
njia za udanganyifu. Wananchi waliotapeliwa wanatakiwa kuja kutambua leseni zao
ili sheria iweze kuchukua mkondo wake
Katika hatua
nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia majambazi
wawili kwa kutuhuma za kujihusisha na unyang’anyi wa kutumia silaha katika
maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
Watuhumiwa hao
walikamatwa tarehe 30/07/2014 huko Makumbusho Kijitonyama, kufuatia msako
makali unaoendelea wa kuwasaka kisha kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi wa
kutumia silaha na makosa mengine.
Walipopekuliwa
nyumbani kwao walikamatwa na Bastola mbili moja ni GROCK17 yenye namba B019259
iliyotengenezwa nchi ya Jamhuri ya CZECH ikiwa na risasi 13 ndani ya magazine.
Nyingine ni Bastola aina ya CHINESE iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi moja
ndani ya magazine.
Watuhumiwa
waliokamatwa ni hawa wafuato:
·
FREDY
S/O STEVEN, Miaka 25, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kiwalani.
·
IRENE
D/O NYANGE, Miaka 36, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kijitonyama, uchunguzi unakamilishwa
na watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa
Jeshi hilo la Polisi
Kanda Maalum DSM linamshikilia mlamavu aitwaye SAID S/O TINDWA, MIAKA 36, MKAZI
WA VIJIBWENI Wilaya ya Temeke kwa kosa la kufanya biashara ya dawa za
kulevya, taarifa za kiintelijensia zilizopatikana kupitia kwa raia wema
ziliwafikia makachero wa Polisi kuwa mlemavu huyo ambaye mguu wake wa kulia ni
wa bandia amekuwa akiutumia vibaya mguu huo kwa kuficha dawa za kulevya ambazo
aliwauzia watumiaji. Aidha kila kete alikuwa akiuza kwa shilingi Tsh.1000.
Ilikuwa mnamo
tarehe 01/08/2014 katika mtego maalumu uliowekwa na askari wa upelelezi ndipo
mlemavu huyo alikamatwa akiuza dawa hizo kwa wateja wake baada ya kuzitoa
alikozificha ambapo ni ndani ya mguu huo wa bandia.
Uchunguzi wa awali
unaonyesha kwamba mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia mbinu hiyo kwa muda mrefu
kabla ya kukamatwa. Aina ya dawa alizokuwa akiuza ni zile za viwandani kama
vile Cocein , Heroin na wakati mwingine bhangi. Uchunguzi wa shauri hili bado
unaendelea na jalada la kesi yake litapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili
sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aidha natoa onyo
kwa watu wenye ulemavu kwamba wasitumie kigezo cha ulemavu kufanya uhalifu kwa
makusudi kwani wanawaharibia walemavu wengine ambao ni raia wema na ambao mara
nyingi huonewa huruma na kutotiliwa mashaka.
Halikadhalika Jeshi hilo linawashikilia wanawake watatu kwa kosa la kujihusisha na
mtandao haramu wa nyara za Serikali. Mnamo tarehe 23/07/2014 huko eneo la
Mbagala Mission Polisi walipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa eneo hilo lina
watu wanajihusisha na biashara ya nyara za serikali.
Polisi walifika eneo la
tukio na kufanikiwa kumkamata WEMAEL D/O MSHANA na alipopekuliwa nyumbani kwake
alikutwa na vipande sita vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola za Kimarekani
30,000 (Dolla elfu thelathini) sawa na
shilingi za kitanzania 49,750,000/= (milioni arobaini na tisa mia saba hamsini
elfu) ambao ni sawa na tembo wawili waliouawa.
Taarifa za awali
zinaonyesha kuwa mtuhumiwa anashirikiana na watuhumiwa wengine ambao ni UPENDO
D/O MSHANA, Miaka 33, na STELLA D/O DANIEL, Miaka 17, Mwanafunzi wa Chua cha
Genessis cha Mtoni kwa Azizi Ali.
Uchunguzi zaidi
unafanyika kwa kushirikiana na Idara ya wanyama pori ili kuhakikisha sheria
inachukua mkondo wake.
S. H.
KOVA
KAMISHNA
WA POLISI KANDA MAALUM
DAR
ES SALAAM
No comments:
Post a Comment