Wednesday, 11 March 2015

MLINZI WA DK SILAA AELEZA UKWELI JUU YA SHTUMA ZAKE

Mlinzi huyo wakati akizungumza na wanahabari akionyesha majeraha aliyoyapata wakati wa kupokea kipigo hicho
Aliyekuwa mlinzi binafsi wa katibu mkuu wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA dk WILBROAD SLAA kwa jina la Khalid Kangezi leo ameibuka na kukanusha taarifa zilizotolea na chama chake kuwa alikuwa anakula njama za kumuua katibu mkuu huyo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma za wazi ndani ya  chama hicho.


Akizungumza kwa uchungu ndani ya ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam mbele ya wanahabari leo amesema kuwa kilichotokea hakijui ila anashangaa kuwa chama kimeamua kumtenda na kumpiga sana wakimtuhumu kutaka kumuua kiongozi huyo jambo ambalo amesema kuwa ni la kushangaza na halina ukweli wowote ule.
Amesema kutokuelewana kwake na katibu mkuu wa chama hicho kiulianza pale alipokuwa na kupishana kwa maneno kati yake na mke wa docta slaa ambapo docta alimuamuru aende kwa mke wake akamalize ugomvi wake na mke wake ndipo aendelee na kazi jambo ambalo amesema kuwa alishangaa kuwa kuwa hakuwa na ugomvi na mke wa docta slaa na hakuweza kufanya hivyo.

Amesema kuwa siku ya jumamosi aliitwa makao makuu ya chama kwa mualiko kuwa kuna kikao maalum na mwenyekiti wa chama hicho na alipofika aliingizwa chumbani ambapo aliwakuwa vijana watano wa chama hicho ambao amewataja kwa majina na bila kumjuza kitu chochote walianza kumpiga mateke,kumtesa,kumvua nguo,kumwagia maji huku wakimtuhumu kuwa amepewa sumu na viongozi wa chama cha ccm ili amuue katibu mkuu dk slaa.
Amesema kuwa baada ya kupokea kipigo kikali kwa zaidi ya masaa sita kutoka kwa vijana hao wa chadema wakimtaka kukiri kuwa anatumika na viongozi wa ccm na usalama wa taifa kukihujumu chama nayeye kukataa walianza kushauriana kuwa wamuue ili waondoe ushahidi wake na ndipo walipanga wampeleke mstuni kwenda kumuua.


Amesema kuwa baada ya kuona kuwa hali inaanza kuwa mbaya na wanaweza kuua kweli aliamua kudanganya ili kuokoa maisha yake kwa kukiri kuwa anatumika na chama cha mapinduzi na wakuu wa idara ya usalama wa taifa kutaka kumuua kiongozio wa chadema docta slaa na aliwaeleza hivyo ili wapunguze makali ya kumtesa ambapo amesema kuwa baada ya kusema hivyo viongozi hao walipunguza makali ya kumpiga na wakatoka nje kuanza kushauriana cha kumfanya,

Anaendelea kueleza kuwa wakati hayo yanafanyika makao makuu ya chama hicho katibu mkuu wa chama hicho dk slaa na viongozi wengine wa chama hicho walikuwa katika ofisi zao na walikuwa wanasikia kila kitu ambacho kinaendelea lakini hawakufanya jambo lolote zaidi ya kaucha aendelee kushushiwa kipigo kutoka kwa vijana hao.


Aidha baada ya muda kadhaa majira ya saa sita usiku vijana hao walimchuukua katika gari nyeusi hadi katika hoteli moja sinza na kumlaza hapo hadi asubuhi,ambapo ilipofika asubuhi vijana wale wakamtaka aandike barua ya kukiri kuwa amepewa sumu na viongiozi wa ccm ili amuue dk slaa lakini yeye alikataa na ndipo walipoleta vifaa ambavyo walikuwa wakivitumia  katika utesaji ili kuanza kumtesa upya na ndipo alipoaamua kuandika barua ya kukiri kuwa anatumika na viongozi wa ccm na usalama wa taifa kukihujumu chadema.


Barua hiyo ambayo ndiyo iliyotumiwa na kiongozi wa chadema MABERE MARANDO kuwaeleza wanahabari kuwa mlinzi huyo alikuwa na njama za kumuua dk slaa ilikuwa inakiri kuwa amekuwa akitumika na viongozi hao katika kukihujumu chama.


Mlinzi huyo ambaye alikuwa akizungumza huku akiwa na machungu amesema kuwa yeye alikuwa akijitolea kumlinda docta slaa bila hata malipo kwani alikuwa anafanya hivyo kwa imani kuwa anawasaidia watanzania .

No comments:

Post a Comment