Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeeleza kuguswa na tukio la mvua
kubwa iliyonyesha wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambayo imesababisha
vifo vya watu 42 na wengine mamia kujeruhiwa na kuacha familia nyingi
zikiwa hazina makazi na kuanzia leo imeanza kampeni ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tukio hilo.
Akiongea
na waandishi wa habari Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano
wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema anawaomba watanzania
wote wanaotaka kuchangia wahanga hao kutuma fedha zao kwenye namba
maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya
155990.
“Tukiwa
kama kampuni ya mawasiliano tumeguswa na tukio hili na tunawapa pole
waathirika wote na tunaungana na wakazi wa kahama kwa janga
hili tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kupitia kitengo chetu cha
kusaidia jamii cha Vodacom Foundation na tunawaomba watanzania wote
wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao na tutahakikisha
tunaifikisha sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu
ambao wako katika mazingira magumu na wanahitaji msaada wa haraka”.
Alisema kupitia njia hii ya namba maalumu ya”Red Alert” 155990 ya
kuchangisha fedha imewahi kurahishisha uchangishaji wa fedha kwa
waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na kuathiri wananchi
moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto
jijini Dar es Salaam na aliwahimiza wananchi kuitumia
kama njia rahisi ya uchangiaji.
Hata hivyo unaweza kuchangia kwa kuponyeza *150*00# alafu unachagua
namba 4 yaani Lipa kwa M PESA baada ya hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba
155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.
No comments:
Post a Comment