Gari lilipata ajali likiwa limevamia nyumba lakini halikuweza kuleta madhara yeyote kwenye nyumba hiyo.
Ajali ya kusikitisha imetokea maeneo ya Bunju B karibu na darajani leo majira ya saa 5 asubuhi, ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya Defender lenye namba T289 CJX ambalo lilikuwa linasafirisha mwili wa marehemu kutoka Dar kwenda Bagamoyo kwa ajili ya maziko.
Chanzo cha ajali hiyo imesadikika ni kwamba dereva wa gari ambalo lilikuwa limebeba maiti alikuwa anaovertake gari nyingine, ambapo ghafla alilikutana na lori , baada ya kuona hivyo dereva ilimbidi achepuke barabara kuu na kuingia kwenye korongo na kufanya gari hilo kupinduka mara tatu na kuvamia nyumba.
No comments:
Post a Comment