TAARIFA YA
KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA ILIYOKUTANA OKTOBA
11, 2014- DAR ES SALAAM
Kikao
cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) kimefanyika leo kujadili matukio ya hivi karibuni, hasa mwenendo wa wadau
wa Bodi ya Ligi. Shirikisho linatoa tamko kwa umma kama ifuatavyo:
1.
Kamati ya Utendaaji imesikitishwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni mpya
za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo inaomba radhi kwa wadau ambao wameguswa na
kusumbuliwa na matukio hayo.
2.Kufuatia
matukio hayo, Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, imefungua
mashtaka kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Damas Ndumbaro ambaye ni mjumbe
wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba. Pia wadau
wote waliohusika na upotoshaji huo wakiwemo wafanyakazi wa TFF na Bodi ya Ligi
watashughulikiwa kulingana na nafasi zao.
3.Kutokana
na madai ya klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu 2014/15, Kamati
ya Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu siku ya Jumamosi,
Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana kuhusu changamoto za
kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla.
4.Kamati
ya Utendaji itaendelea kuboresha Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi (Governing
Regulations) ili kuweka uwiano wa utendaji na kuepusha tofauti kati ya Bodi ya
Ligi, vilabu na TFF. Aidha Kamati ya Utendaji itafanya kila linalowezekana kuboresha
ligi kwa kuijengea uwezo Bodi ya Ligi kwa lengo la kuwa na ligi zinazoendeshwa
kisasa (Professional Leagues).
No comments:
Post a Comment