Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kesho (Oktoba 29
mwaka huu) anafungua kozi ya ukufunzi wa waamuzi ya FUTURO III ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Hafla ya ufunguzi
wa kozi hiyo inayoshirikisha zaidi ya waamuzi 40 wakiwemo baadhi ya wale ambao
bado wanachezesha mpira wa miguu kutoka nchi mbalimbali za Afrika itafanyika
saa 4 asubuhi kwenye hoteli ya Holiday Inn, Dar es Salaam.
Kati ya hao,
washiriki wanane wa kozi hiyo inayoanza kesho hadi Novemba 3 mwaka huu chini ya
wakufunzi wa FIFA wakiongozwa na Carlos Henriques ni kutoka Tanzania.
Washiriki kutoka
Tanzania ni Emmanuel Chaula, Joan Minja, Josephat Bulali, Paschal Chiganga,
Ramadhan Ibada, Richard Kayenze, Samuel Mpenzu na Soud Abdi.
SALUM ABUBAKAR MCHEZAJI BORA OKTOBA
Kiungo wa timu
ya Azam, Salum Abubakar amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali
nchini.
Abubakar ambaye
pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) aliwashinda wachezaji
wengine 20, huku wanne kati ya hao wakichuana naye kwa karibu.
Wachezaji hao ni
Joseph Mahundi wa Coastal Union, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (Kagera
Sugar) na Najim Magulu wa JKT Ruvu Stars.
Kwa kuibuka
mchezaji bora, Abubakar atazawadiwa kikombe na fedha taslimu sh. milioni moja
kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo maalumu la
makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi
kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili
kumpata mshindi wa mwezi.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment