001.MkurugenziMtendajiwa
Vodacom Tanzania, Rene Meza,
akiongeanawaandishiwahabariwakatiwauzinduzirasmiwakutumanakupokeapesanchini
Kenya kwanjiaya M-PESA. Uzinduzihuoulifanyikajijini Dar es Salaam.
.
MkurugenziwaMifumoyaMalipowaBenkiKuuya Tanzania, Bernard Dadi (katikati)
akifafanuajambokwaMkurugenziMtendajiwa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto)
baadayauzinduzirasmiwakutumanakupokeapesanchini Kenya kwanjiaya M-PESA
uliofanyikajijini Dar es Salaam. KulianiMenejawaMifumoyaMalipowaBenkiKuu
Tanzania, James Masoy.
Dar es Salaam, Tanzania,
Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hii,Mkurugenzi
Mtendaji
wa Vodacom Tanzania Rene Meza alisema kuwa takwimu zilizopo zinaonyesha
kuwa mwaka 2013 zaidi ya shilingi bilioni 200 zilitumwa kutoka
Tanzania
kwenda Kenya halikadhalika zaidi ya bilioni 1
zilitumwa kutoka Kenya kuja Tanzania.
“Kwa mujibu wa takwimu za Benki
ya Dunia zinaonyesha kuwa fedha karibu shilingi bilioni 200 zilizotumwa
nchi Kenya kutoka Tanzania zilitumwa
kwa njia rasmi za utumaji fedha na inakadiriwa kuwa kiasi cha fedha
hizo zaidi ya mara mbili zimetumwa kwa njia zisizo rasmi za utumaji
fedha ikiwemo kutumia madereva na makondakta wa mabasi au kutumia ndugu
na marafiki wanaosafiri”amesema Meza.
“Tumeona
ugumu wanaokabiliana nao wateja wetu kutuma fedha katika nchi jirani
ya Kenya na tumepata suluhisho kwa kuleta huduma hii ambayo ni ya haraka
na uhakika.Kuanzia leo hakuna sababu ya kutuma pesa kwa kumtumia
dereva au kondakta wa basi au kutozwa gharama kubwa kutoka taasisi za
kifedha unapolipa karo za watoto wanaosoma nchini humo,unaweza sasa
kufanya malipo na kulipa ankkra mbalimbali kutoka pochi
ya M-Pesa ukiwa umetulia nyumbani kwako,”amesema Meza.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Safaricom Bob Collymore alisema “Tunaamini
tumefungua ukurasa mpya wa kuendeleza huduma ya M-Pesa kwa kuwezesha
wateja
wa Kenya na Tanzania kutumia huduma hii katika kutumiana fedha na
kufanya malipo katika nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya”.Alisema
Alisema
katika awamu hii ya kwanza iliyozinduliwa leo inawawezesha wateja
kutuma pesa Kenya kama ambavyo wamekuwa wakituma hapa nchini, tofauti
itakuwa
wakati wa kutuma pesa kwenye simu kutakuwepo na kipengele
kinachoonyesha kuwa wanataka kutuma pesa kwa M-Pesa ya Kenya na kuandika
namba za mpokeaji kwa kutumia namba za Kenya yaani +254 na katika awamu
ya pili ya huduma hii wateja wa Safaricom ya Kenya wataweza
kutuma pesa kwa wateja wa Vodacom Tanzania kupitia huduma hii.”
Huduma
ya M-Pesa inatolewa na makampuni ya Vodacom Tanzania na Safaricom ya
Kenya yote yakiwa makampuni makubwa yanayotoa huduma ya mawasiliano
katika
ukanda huu wa Afrika Mashariki.Wakati Vodacom inatoa huduma za kutuma
na kupokea fedha kwa asilimia 65 nchini. “Ushirikiano huu wa mtandao
wetu wa M-Pesa wenye mawakala zaidi ya 75,000 nchini Tanzania
utawarahishia wateja wetu kupata huduma bora ikiwemo kufanya
mihamala yao ya fedha kwa urahisi na tumejipanga kutoa huduma bora kwa
wateja kwa muda wote wa masaa 24 kila siku.”Alisisitiza Meza.
“Kenya ni moja ya nchi inayofanya biashara kwa kiasi kikubwa na Tanzania ndio maana huduma hii imeanzia nchini humo na
kuzidi kuunganisha na kuimarisha ushirikiano wa nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Tunaamini kuwa mawasiliano hayana mipaka
kwa kuwa kwa kuwa huwaunganisha watu na jamii na jamii na kusaidia
kuharakisha maendeleo na ndio
maana Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika sekta
hii”.Alisisitiza Meza.
Kuna
zaidi ya Wakenya 300,000 wanaotuma fedha nchini kwao kwa kutumia njia
zisizo rasmi na salama kama vile kuwatumia makondakta na madereva wa
mabasi
vilevile kuna watanzania wengi wanasomesha watoto wao nchini Kenya
ambao nao wamekuwa wakipata shida kutuma fedha nchini humo.”Kwa kuanzia
leo huduma kwa wafanyabiashara kulipana zimerahisihwa ikiwemo kulipa
karo za shule na vyuo na mihamala mingine,Huduma
ya M-Pesa imerahisisha kila kitu na kuzidi kufungua milango ya
biashara na ushirikiano”Aliongeza kusema Meza.
Alimalizia
kusema kuwa huduma hii itafanya maisha ya watumiaji wake kuwa murua kwa
kuwa watatuma fedha zao na kuwa na uhakika wa kuwafikia walengwa moja
kwa moja na ni njia ya uhakika na yenye usalama inayowapunguza adhabu
kubeba kiasi kikubwa cha fedha mifukoni na kwenye mabegi pia walengwa
watapokea malipo kwa viwango vya ubadilishanaji sahihi visivyobadilika
kila siku
No comments:
Post a Comment