Katibu
wa CCM kata ya Ruaha Rashid Shungu ( wa pili kushoto ) na kada wa
Chadema aliyehamia CCM Ibrahim Mmasi pamoja na wanachama wengine wa
CCM wakiwa wameshika bendera ya CCM ambayo itapepea katika ofisi mpya
ya kata ya Ruaha ,ofisi ambayo awali ilikuwa ikimilikiwa na Chadema
kabla ya kufukuzwa kwa kushindwa kulipa deni la kodi kiasi cha Tsh
540,000 , kushoto fundi rangi akiendelea kupaka rangi ya CCM
Fundi akipaka rangi kuta za ofizi hiyo
CHAMA
cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kata ya Ruaha jimbo la Iringa
mjini kimepata pigo kubwa baada ya kufukuzwa katika nyumba
waliyopanga kama ofisi ya kata hiyo baada ya kushindwa kulipa deni
la pango kiasi cha Tsh 540,000 walizokuwa wakidaiwa na mwenye nyumba
deni ambalo limelipwa na Chama cha mapinduzi (CCM ) kata ya Ruahakabla ya kuichukua ofisi hiyo .
Mmiliki
wa nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Ngeleli Ipogolo Bi Neema Mwasika
alifikia hatua hiyo ya kuwataka kuondoka katika ofisi hiyo baada
ya jitihada za kudai deni lake kushindikana na hivyo kulazimika
kupangisha nyumba hiyo yenye chumba kimoja na sebure kwa mpangaji
mpya ambae ni CCM kata ya Ruaha.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo katibu wa CCM kata ya Ruaha Rashid
Shungu alisema kuwa awali CCM kilikuwa na ofisi yake eneo la Ruaha
jirani na mto hivyo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mwaka jana
zilipelekea ofisi hiyo kuharibiwa vibaya na hivyo kukosa kabisa
ofisi .
Alisema
kuwa kutokana na kutokuwa na ofisi cham a kilikuwa kikitumia nyumba
ya mtu binafsi kama ofisi pale ilipohitajika kukutana viongozi ama
wanachama .
Shungu
alisema kuwa jitihada za kutafuta nyumba ya kupanga ili kutumika
kama ofisi ya muda ya CCM kata hiyo ya Ruaha ziliendelea kufanyika
chini ya aliyekuwa kada wa Chadema kata hiyo kabla ya kujiunga na CCM
Bw Ibrahim Mmasi
Hata
hivyo alisema ofisi hiyo alisema kuwa baada ya kuona ofisi hiyo
imefungwa kwa muda na kuwasiliana na mwenye nyumba alikubali
kuwapangisha kwa makubaliano ya kulipa deni kwanza jambo ambalo
lilifanyika hivyo na kulipia kodi ya miaka miwili zaidi.
”
Tumeipata ofisi hii kihalali na sio hujuma kwani makubaliano kati
ya mmiliki wa nyumba na mpangaji yalifanyika na hivyo kwa kuwa hitaji
letu nyumba ya kupanga tuliona hiyo ina sifa ambayo tuliitaka
hivyo tunachofanya ni kufuta rangi na nembo za Chadema na kuweka
rangi ya CCM na nembo zetu …..na tutaizindua rasmi jumapili wiki hii”
Kwa
upande wake kada wa CCM aliyehama kutoka Chadema Bw Mmasi alisema
kuwa ofisi hiyo ilikuwa imezinduliwa na viongozi wa kitaifa kupitia
zoezi la oparesheni Sangara tarehe 19 mey 2011 chini ya naibu mkuu wa
Chadema enzi hizo Zitto Kabwe na mbunge wa jimbo la Iringa mjini
mchungaji Peter Msigwa na viongozi wengine .
No comments:
Post a Comment