Na Karoli
Vinsent
SIKU moja
kupita baada ya Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kusema haina Mamlaka ya kulivunja
Bunge Maalum la Katiba kwa madai kwamba Hakuna kipengere cha Sheria kinachotoa
mwanya kwa Rais kulivunja Bunge hilo.
Pia Ikulu ikasema Bunge hilo
litaendelea na hata kama Wajumbe wanaounda Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi
UKAWA,kutokuwepo kwani umoja huo ni idadi ndogo sana ya wajumbe .
Nao Umoja wa Kutetea Katiba ya
Wananchi UKAWA,umeibuka na kusema Ikulu hiyo inashindwa kudagavua sheria vizuri
Kauli hiyo imetolewa leo na
Mwanasheria wa Umoja wa kutetea katiba ya Wananchi UKAWA Tundu Lissu wakati
alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu juu ya taarifa hiyo ya Ikulu.ambapo
Lissu alisema ni kweli Rais Kikwete hana mamlaka ya kulivunja bunge hilo.
Bali Rais amefanya mambo mengi
kwenye mchakato huu wa katiba na hakuna kipengele chochote cha sheria
kinachompa mamlaka ya kufanya mambo hayo.
“Ni kweli mwandishi hakuna
kipengele chochote cha sheria kinachompa mamlaka Rais kulivunja bunge hilo,ila
nashangaa sana ikulu inaangalia sheria kwa juu juu tu,hivi mbona Rais amefanya
mambo kwenye mchakato huu wa katiba pasipokupewa idhini ya sheria,”
”kwa mfano niambie ni wapi kuna
kipengele cha sheria kinachompa mamlaka Rais kufungua Bunge Maalum la Katiba
lakini mbona Rais alikwenda kulifungua bunge la katiba? Na ni sheria gani
inayompa mamlaka Rais kuongeza mda vikao vya bunge la katiba mbona kaongeza mda
sheria hizi zinatoka wapi”alihoji Lissu.
Tundu Lissu ambaye pia ni Mjumbe wa
Bunge Maalum la Katiba alizidi kusema kwamba kwenye sura za Katiba za nchi
zinampa Mamlaka Rais kuteua na kufukuza mtumishi yeyote inakuwaje leo ikulu ije
na kauli yenye ukakasi kama hiyo.
Kuhusu kufunguliwa mirango wazi kwa
Wajumbe wa UKAWA kwenda ikulu kuonana na Rais.
Tundu Lissu alisema amezipata
taarifa hizo ila kwa sasa anawasiliana na Wenzake ili kujua wanachukuliaje
maamuzi hayo.
Kuhusu utata
unaoibuka sasa kuhusu 2 ya 3 wajumbe kutoka Zanzibar.
Tundu Lissu,ambaye pia ni Mbunge wa
Singida mashariki CHADEMA alisema anashangaa jinsi ikulu inavyodanganya
watanzania kwani ukweli huko pale pale hakuna uwezekano wa kupatikana 2 ya 3 ya
wajumbe kutoka Zanzibar.
“Ukisoma waraka wa chama cha
Mapinduzi CCM,uliotolewa baada ya kumalizika kwa vikao vya kwanza vya Bunge
maalum la Katiba wanasema wazi kwamba 2 ya 3 ya wajumbe wa Bunge maalum la
katiba kutoka Zanzibar haipo sasa hao ikulu wanasemaje idadi hiyo ipo , mimi
nawashangaa sana”alisema Lissu
No comments:
Post a Comment