Saa chache baada ya radio ya Clouds fm kutangaza rasm
kutokutangaza habari yoyote inayohusioana na
wajumbe wanaounda kundi la umoja wa katiba ya wananchi ukawa kwa kile
kinachodaiwa umoja huo hauna jipya zaidi ya kujitafutia umaarufu tu
Kauli hiyo ambayo imekwenda kinyume na maadili ya uandishi
wa habari na utangazaji imetolewa na mtangazaji wa kipindi cha
power breakfast Babla Hassan wakati wa uchambuzi wa magazeti ya siku ambapo
amesema kwa sasa hawatazisoma habari zozote zinazohusu umoja huo wa UKAWA kwa
madai umoja huo ni wa binafsi na hawana jipya bali wanataka umaarufu tu
Naye mwanasheria mkuu wa
umoja huo wa UKAWA TUNDU LISSUamesema kwamba radio hiyo inajimaliza na
ndio inajionesha wazi inabagua upande mmoja wa kisiasa
Kauli hiyo yaTUNDU LISSU ameitoa muda huo wakati alipokuwa
akizungumza na mwandishi wa mtandao huu kuhusu waoUKAWA wanaipokeaje hiyo
kauli ya kutosomwa kwa taarifa zozote zinazohusu kundi hilo alisema ni kweli
hizo taarifa amezisikia na kama kweli wamejimaliza
’’kwanza nimezisikia hizo taarifa na kama kweli aliyose huyo
mtangazaji ndio msimamo wa radio nzima basi watakuwa watu wa ajabu sana maana
leo nchi nzima habari ya mjini ni UKAWA leo utasema UKAWA ni wabnasi wakati
wasomi na watu wengine wanaungana na sisi leo inakuwaje radio hiyo iseme hivyo
kama wako upande mmoja wa kisiasa waseme alisema LISSU
Tundu lissu ambaye ni mjumbe wa bunge maalum la katiba
alizidi kusema yeye sio mwaNAHABARI BALI anachokijua huo utakuwa msimamo wa
radio nzimana wao ukawa hawataogopa na kuacha kutetea wananchi kwani wako kwa
ajili ya kuwakomboa wananchi na hawawezi kukatishwa na tama na watu wachache
wenye maslahi ya upande mmoja
Halafu inashangaza sana leo nchi nzima inazungumza ukawa
halafu yeye aseme leo ukawa hautotangaza habari zao kwa misingi ipi? Alihoji TUNDU
‘mimi naona kusoma story
zinazohusu ukawa tunawapa kiki tu
wao si wamekuwa kutupotezea kutorejea bungeni I whon doing vile vikao
vinawanufaisha watanza wote wao ni wabnafsi tu the best I can do tunawapotezea
habari zao na ukiona habari inahusu ukawa tu usisome hapa kwenye radio na wakae
huko nje atuwataki ukawa bunbgeni alisema BABLA
Kauli hiyo iliyoungwa mkono n a watangazaji wengine wa
kipindi hichoPAUL JEMS anayejulikana kwa jina maarufu PJ alisema tangi sasa
hatasoma story yoyote inayohusu ukawa kwani wamelisusia bunge na wanatumia
fedha za wananchi tu
Msimamo huo wa watangazaji hao unakwenda kinyume na mmiliki
wa radio hiyo ya clouds fm joseph kusaga alipokuwa ana hojiwa na kpindi kimoja
cha runinga kutoka nchini uingereza kinachojulikana The Sporah Show ambapo
katika kipindi hiko alisema radio yake haina upande wowote wa kisiasa na
kuongeza ni radio huru inayofanya kazi bila kushabiki upande wowote
Lakini kwa sasa kauli ya mmiliki huyo imeenda tofauti na
ilivyo na kama radio ikifanya kama inavyofanya hivyo kwa sasa basi radio hiyo
itapelekea mchafuko makubwa kama yaliyowahi kutokea nchini Rwanda na kuuwa
maelfu ya watu na sababu kubwa ni radio za nchini humu zilikuwa na m,isimamo
kama waliyonayo clouds
Umoja huo wanaupinga wa ukawa unaundwa na muunganiko wa
vyama vikuu vya upinzani ikiwemo CHADEMA,CUF,NCCR Mageuzi.ND pamoja na baadhi ya
wajumbe 201 walioteuliwa na rais
Umoja huo umegoma kurudi kwenye vikao vya bunge la katiba
kwa madai rasmi inayotokana na maoni ya wananchi kuchakachuliwa na kitendo
hicho cha ukawa kimeungwa mkono na wananchi mbalimbali wakiwemo viongozi wa
dini pamoja na wajumbe wa iliyokuwa tume ya jaji WARIIBA
No comments:
Post a Comment