Thursday, 14 August 2014

SERIKALI YAJIPANGA KUKABILIANA NA EBOLA TANZANIA

Na Karoli Vinsent

SERIKALI imesema hakuna mtanzania yeyote aliyegundulika kuwepo na Ugonjwa wa Ebola ,bali serikali imejipanga kuhakikisha hakuna Mtu atakayeupata Ugonjwa  huo.
        Kauli hiyo ya Serikali inakuja Siku moja kupita Baada ya Gazeti la Sani,toreo la Jana Jumatano   tarehe 13 hadi  18 mwezi huu,kuripoti taarifa  juu ya kuingia Ugonjwa wa Ebola nchini.
             Akinusha Taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo Assah Mwambene,amesema taarifa  hiyo haina ukweli , kwani hakuna Mtanzania yeyote aliyegundulika kuwa na ugonjwa huo.
              “Gazeti hilo limeandika taarifa ambayo sio za kweli kwani hakuna mtanzania ambaye amegundulika kuwapo na ugonjwa wa Ebola na serikali kwasasa imejipanga kuhakikisha hakuna mtanzania ambaye ataupata ugonjwa huo kwa sasa”alisema Mwambene.
                Mwambene ambaye pia ni Msemaji wa Serikali alizidi kusema kwa sasa amemwandikia Barua Mhariri wa Gazeti la Sani na kumtaka ndani ya siku 18 awe amekanusha Taarifa hiyo,ambayo imewachanganya wananchi na kuwapa hofu kubwa.
                    Vilevile Mwambene alitumia nafasi hiyo kuwasihi Wahariri na Waandishi wa Habari nchini kufanya kazi kwa ukweli na wazi.
“Natumia nafasi hii,kuwaomba waandishi wa Habari nchini pamoja na Wahariri kufanya kazi kwa weredi mkubwa tukumbuke Habari za Ugonjwa wa Ebola ni habari za kuwa makini sana ,hizi sio Habari kama za UKAWA,hizi ni Habari zinazohusu maisha ya watu moja kwa moja kwahiyo tuwe makini sana”alisema Mwambene.
              Taarifa hiyo ya Mwambene inakuja siku moja kupia baada ya Gazeti hilo pendwa toreo No.1148 la kuanzia Jumatano 13 hadi 18 mwezi lilobeba kichwa cha Habari Ebola Yatua nchini,huku likitoa picha ya Mgonjwa ambaye ameupata ugonjwa huo,taarifa hiyo ambayo ilizidisha hofu kubwa kwa Watanzania.
               Ugonjwa huo wa Ebola ambao mpaka sasa umeua watu zaidi ya elfu kumi huko Afrika ya Magharibi na kujeruhi mamia ya watu,huku mpaka sasa hakuna dawa ya Ugonjwa huo .    

No comments:

Post a Comment