Na karoli
Vinsent
KWA muda
miezi mitatu sasa Mtandao huu umefanya utafiti katika sekta ya Habari hususani
magazeti na kutaka kujua ni Waandishi gani wa Habari kwenye magazeti ambao makala zao zinapendwa sana.
Mtandao huu katika utafiti wake
uliangazia magazeti zaidi ya 20 ambayo yamesajiliwa na msajili wa magazet
nchini,utafiti huo ulijikita zaidi katika kuangalia hamasa za watanzania katika
kutaka kuzisoma habari za waandishi hao.
Katika utafiti huo walishirikishwa hadi
wauza magazeti pamoja na wasomaji wa magazeti.
Wafuatao ni ndio Waandishi watano
Bora ambao Makala zao zinasomwa sana nchini Tanzania.
1..Jenerali Ulimwengu
Huyu ndio
miongoni mwa Waandishi wa Makala bora kabisa nchini Tanzania,ambaye anaandika
makala ambapo wananchi hawataki hata wiki ipite bila kusoma makala zake.
Ulimwengu ambaye anaandikia
makala zake kwenye Gazeti la Raia mwema na Raia Tanzania,katika magazeti hayo
amekuwa akiandika makala mbalimbali ikiwemo za Kisiasa pamoja na kijamii,na
kufanya Gazeti la Raia Mwema kuwa ni miongoni mwa gazeti linalopendwa zaidi,
Gazeti la Raia Mwema ni Gazeti
linalotoka maramoja kwa Wiki limekuwa likipendwa sana kutokana na mchango
anaoufanya mwandishi huyo.
Ulimwengu makala zilizompa heshima
kubwa sana ni –Acha kelele toa hoja,pamoja Hapa kwetu tunakimbilia wapi ,na
makala nyingine.
2..Saed Kubenea
Huyu naye
ameshika nafasi ya pili ya Waandishi bora wa Makala nchini Tanzania,Kubenea
jina lake sio geni sana kwenye masikio ya watanzania kutokana na kazi kubwa
anayofanya hapa nchini kwenye sekta ya Habari.
Kubenea anasifika kutokana na
Ujasili aliokuwa nao,mwandishi huyo makala zake nyingi anaandikia kwenye gazeti
La Mawio.
Kabla ya kuandikia Mawio kubenea
pia alikuwepo kwenye Gazeti la lilofungiwa kwa muda usiojulikana la Mwanahalisi.
Katika gazeti la Mwanahalisi
kubenea alikuwa ni mkurugenzi wa gazeti hilo,baada ya kufungiwa gazeti
hilo,kubenea hakutaka kipaji chake kupotea cha kuhabalisha watanzania ndipo
akajiunga kwenye Gazeti la Mawio.
Uwepo wake kwenye Gazeti hilo
la Mawio ndipo amelifanya limekuwa gazeti linalopendwa zaidi sana nchini Tanzania,gazeti
la Mawio linatoka kila alhamisi.
Kwa Mujibu ya wauza magazeti wanasema
katika magazeti yanayofanya Vizuri gazeti la Mawio lipo.
3---Edo Kumwembe.
Huyo naye ameshika nafasi ya
Tatu kati ya Waandishi wa Habari ambao wanaandika makala zinazopendwa zaidi.
Kumwembe,ambaye ni tofauti na
Ulimwengu,kubenea kwani Kumwembe yeye anaandika makala za habari za Michezo
kwenye gazeti la Mwanaspoti.
Kabla ya kuandika mwanaspoti
Kumwembe alikuwa anaandika makala kwenye Gazeti la michezo Dimba,ambapo
alipokuwa huko kumwembe alisifika sana kwa kuandika makala nzuri zenye
kuwafanya wasomaji wasikubali hata wiki kupita bila kusoma makala zake na hata
alivyoamia Mwanaspoti huko ndipo alipozidi kupata umaharafu sana kwa makala
zake zenye ubora.
Kitu kinanchomtofautisha kumwembe
na waandishi wengine wa makala za michezo kumwembe amekuwa mtu anayefanya
utafiti kabla ya kuandika makala zake ikiwemo hata kwenda hata nchi za nje.
4—Edson Kamukara
Huyu naye ameshika nafasi ya Nne kati ya
Waandishi wa Habari wanaoandika makala zinazowafanya wasomaji wazipende zaidi.
Edsoni Kamukara ambaye anatoka
kwenye Gazeti la kila siku la Tanzania Daima naye anasifika sana kwa kuandika
makala zenye kupendwa zaidi amekuwa akiandika makala bila ya uoga wowote.
Kamukara ambaye pia ni Mhariri
wa Gazeti hilo ,amekuwa akiandika makala zenye kutoa elimu pamoja na kuwakosoa
vongozi walioko Makadarani ambao
wanakwenda kinyume.
Umakini wa Kamukara umelifanya Gazeti
la Tanzania Daima kuwa ni miongoni mwa magazeti linalopendwa zaidi.
5---Jabir Idrissa
Huyo naye ameshika nafasi ya
Tano kati ya Waandishi wanaongoza kwa undikaji wa Makala zinazowafanya wasomaji
walipende Gazeti kulisoma kila siku.
Jabir ambaye anatoka kwenye gazeti
la Mawio naye amekuwa ni miongoni mwa Waandishi wanaongoza kwa uandishi makini
wa Habari pamoja na Makala zenye kuifanya Jamii ilipende kusoma gazeti hilo.
No comments:
Post a Comment