Na Karoli
Vinsent
BAADA ya
kuzoa wanachama wengi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Chama
kipya cha Siasa nchini cha Alliance for change and Transparency ACT,sasa
kimezidi kuzoa wanachama wengine ikiwemo viongozi kutoka vyama vingine vya
upinzani .
Hayo yamejidhililisha wiki hii Jijini Dar es Salaam wakati walipokuwa wakitambulishwa
wanachama wapya waliohamia chama cha ACT-Tanzania Mbele ya Waandishi wa
habari,Ambapo Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT-Tanzania Masega Muhamedi Masega
alithibitisha kupokea wanachama wapya watatu ambao walikuwa viongozi waandamizi
kutoka Chama cha Upinzani cha Sauti ya Umma SAU,
Viongozi hao Waandamizi ni Fred
Kisena,ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Mahusiano ya Jamii na sera Taifa ya chama
cha SAU ,Majinus Mwembe Mkurugenzi Mkuu
wa Fedha pamoja na Zabroni Shilumbi ambaye alikuwa Naibu katibu mkuu wa Sera wa
chama hicho.
Wakizungumza wote kwa pamoja viongozi
hao wa chama cha SAU ,waliohamia chama cha ACT-Tanzania walisema wameamia kwenye chama hicho baada ya
kupendezewa sera ya chama hicho na kusema kwa sasa wanaimani chama cha
ACT-Tanzania ndio mkombozi Watanzania kutoka kwenye hali ngumu ya Maisha
inayowakabili.
Naye Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT-Tanzania Masega Muhamedi Masega
aliwashukuru sana viongozi hao wa chama cha SAU kwa kuungana nao katika kutetea
Watanzania na kusema chama hicho kitahakikisha kinashirikiana na wanachama hao kuhakikisha
wanamkomboa mtanzania wa leo na kuwataka watanzania kujiunga na chama hicho
kwani ndio kimbilio lao,
Katika Hatua nyingine Chama hicho
kipya cha Siasa cha ACT-Tanzania,kwaanzia kesho kitaanza Ziara kwenye mikoa 15
kwa lengo ya kueneza na kukijenga chama hicho hadi ngazi za chini.
Akizungumzia Ziara hiyo Katibu
Msaidizi wa Chama hicho Leopald Luca Mohona alisema wameandaa makundi matatu
yatakayogawanywa mikoa 15 ambapo kundi la kwanza litaongozwa na Mwenyekiti wa
Mda chama hicho Lukas Kadawa Limbu akisaidiwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya
Athumani Balozi.
Ambapo ziara
hiyo itatumia siku 17 kufikia majimbo 22 kwenye mikoa mitano.
Vilevile Kundi Jingine litaongozwa na
Makamu mwenyekiti akisaidiwa na Naibu katibu mkuu Taifa pamoja na kundi jingine
pia litakalo ongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Samsoni Mwigamba
atakayeambatana na Katibu Uenezi wa chama hicho kwenye mikoa mengine,
No comments:
Post a Comment