Wednesday, 23 July 2014

M.A.T WAOMBA MASHIRIKA MBALIMBALI KUINGILIA KATI UTUPAJI WA MIILI NA MASALIA YA BANADAMU BILA UTARATIBU



Chama cha madaktari Tanzania M.A.T kimevitaka vyombo husika kama jeshi la polisi,wizara ya afya,baraza la madaktari Tanzania,tume ya usimamizi ya vyuo vikuuTCU,taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR, kuchukulia hatua stahiki kwa mtu au taasisi iliyotupa na kutekeleza mabaki ya viungo mbalimbali vya miili ya binadamu vinavyoaminika kuwaq vilikuwa katika mafunzo na utafiti

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini dare s saalam rais wa madaktari Tanzania dr Primus Saidia alisema kwamba kutokana na tasnia ya tiba  ni utaratibu unaokubalika duniani kote ikiwemo Tanzaniakutumia miili  na viungo asili vya binadamu katika  kufundisha na kufanyia utafiti

;miili na viungo hivi vinatumika kwa heshima  kubwa kama waalimu wa kwanza katika mafunzo ya utafitiza tiba ya mwanadamu  ambapo tafiti hizo ndio njia kuu katika kukuza ufahamu wa mwili wa binadamu na hivyo kuboresha utoaji wa huduma za afya;alisema dk Saidia

Halikadhalika alisema kitendo hicho kimekiuka kwa kiasi kikubwa  sheria,taratibu,na utu wa binadamu na maadili ya ufundishaji na taaluma ya udaktari kwa kitendo hicho cha kutupa cha kutupa miili hiyo

;watu na taasisi zilizohusika na kitendo hiki imepoteza sifa ya kufanya utafiti au kutoa mafunzo ya kidaktari kwa kutumia miili ya binadamu ,hii ina maana kuwa kama taasisi ya utafiti imepoteza sifa ya utafiti  na kama ni mafunzo imepoteza sifa ya kutoa mafunzo ya tiba,na kama ni hosptali imepoteza sifa ya kutoa tiba ka binadamu;alisema rais huyo

Halikadhalikaalibainisha taratibu za kuipata miili,kusafirisha ,kuhifadhi,kutumia na kustiri mabaki baada ya matumizi hufanyika kwa kufuata sheria ,maadili,afya ya jamii.utamaduni,miiko,na heshima kwa utu wa binadamu na jamii husika

;Kitendo kama hiki kwa nchi nyingine kinatosha kabisa kuifungia taasisi  kuendelea na mafunzo na tafiti au huduma za kibinadamu ;alisemadk saidia

Halikadhalika rais waserikali ya wanafunzi chuo cha muhimbili bwana Alex Elifuraha ameulalamikia uongozi wa wizara ya afya kwa kushindwa kuboresha na kufanyia marekebisho mashine ya kuchomea mabaki ya miili na viungo vya binadamu kwa kitaalam INCINIRATURE katika ospitali kuu ya muhimbil

No comments:

Post a Comment