Wednesday, 23 July 2014

TASO KUTOA ELIMU KWA WANALINDI KUHUSU UBORESHAJI WA KILIMO.




kajula
Iman Kajula Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo mchana kuhusu maonyesho ya NANE NANE yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mkoani Lindi, Kutoka kulia ni Mathew Gugae Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara EAG Group na katikati ni Engerbelt Moyo Mwenyekiti wa TASO.

  
Na Rose Masaka -MAELEZO

WANANCHI mkoani Lindi wanatarajiwa kuelimishwa njia bora na za kisasa za uvuvi, ufugaji na ukulima ili waweze kuboresha kipato chao na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima Tanzania(TASO) Engelbert Moyo wakati akiongea na waandishi wa habari.
Amesema kuwa wakati wa maonesho ya nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Lindi watajitahidi kuhakikisha wananchi wanajifunza teknolojia mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi ili waweze kuzalisha mazao yanayokidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

Moyo ameongeza kuwa watawaelimu wavuvi juu ya madhara ya uvuvi haramu na unavyohatarisha mazingira na viumbe wa majini.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa maonesho yatafunguliwa na Rais wa Serikali za Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Amesema kuwa Mawaziri mbalimbali watasaidia kutoa elimu kwa wakazi wa Mkoa huo kuhusu shughuli mbalimbali wanazozifanya katika kuwaletea maendeleo.

No comments:

Post a Comment