Waamuzi
wa mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Afrika
Kusini (Amajimbos) wanawasili leo (Julai 15 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
Mechi hiyo itafanyika Ijumaa
(Julai 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini
Dar es Salaam na itachezeshwa na waamuzi hao kutoka Shelisheli.
Kiingilio cha mechi hiyo ni sh. 2,000 tu.
Waamuzi hao ambao wanawasili saa
2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ni Allister Barra, Gerard Pool,
Jean Joseph Felix Ernest na Nelson Emile Fred.
Kamishna wa mechi hiyo
Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar pia anawasili leo
saa 2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment