Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, SHEKH RAJAB KATIMBA akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam. |
JUMUIYA
na Taasisi za Kiislam Nchini imesema itawahamasishwa Waumini wa dini zote
popote walipo nchini kuipigia kura ya Hapana katiba iliyopendekezwa na
Bunge maalum la Katiba, pamoja na kuukataa Mswaada wa Marekebisho ya
sheria mbalimbali wa namba 2 wa mwaka 2014 unaotarajiwa kuwasilishwa
kwenye Bunge lijalo kutokana na Serikali kuwadanganya waislam nchini.
Kutokana na kitendo chake Serikali kupuuza matakwa yao wanaodai
uwepo wa Mahakama ya Kadhi ambao wanasema ilikuwepo kwenye makubaliano
kati ya Serikali na Waislam nchini juu ya uwepo wa Mahakama hiyo.
Hayo
yamesemwa Leo Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislam nchini, Rajabu Katimba wakati wa Mkutano na Waandishi
wa Habari ambapo alisema waislam wamechoka na ubabaishaji unaofanywa
na serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kulitekeleza Azimio la
uundwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini.
“Kwani
hata mswaada wa marekebisho ya kisheria mbalimbali unaowasilishwa na
serikali hautakuwa na tija kwa waislam nchini na umekuwa na propaganda
nyingi za unzishwaji wa mahakama ya kadhi lakini hauna utekerezaji na
ndio sababu tunasema hakuna nia ya dhati kati ya serikali ya CCM na
Waislam”
“Nchini
kwani wametudanganya kwenye Ilani yao ya Mwaka 2005 ilituhaidi
kuanzisha mahakama ya kadhi lakini kwa ghazba nyingi CCM haikutekeleza
ahadi hiyo baada ya kuingia madarakani kwa hoja kuwa hili ni Jambo la
Kikatiba”alisema katimba
SHEKHE Katimba alizidi kusema kwa Uchungu kwamba
“hata
wakati wa Bunge la katiba lilokuwa limeundwa na wajumbe wengi wa CCM
hawakuona umuhimu wa kutimzi ahadi yao ya kuweka Mahakama ya Kadhi
katika katiba pendekezwa na kwani wajumbe wengi wa CCM walishangilia
Jambo hili ili hali wanajua Dhahiri kuwa Waislamu hawakufurahishwa na
uamuzi wao na pia walikiuka ilani yao na ahadi kwa Waislam”
Aidha,Shekhe
Katimba alisema hata mswaada ambao wanaukataa wa merekebisho ya Sheria
wa namba 2 wa mwaka 2014 unakasoro nyingi ambazo wanasema hauna tija kwa
waislam katika kipengere cha Mahakama ya Kadhi-
Ikiwemo Mswaada umempa mamlaka “MUFTI”kuteua makadhi na kuengeneza
kanuzi za Uendeshaji wa mahakama ya Kadhi ili hali sio chombo cha
Sheria,na pia Mswaada huo umempa Mufti-
Mamlaka
ya kutenganisha kanuni za uendeshaji wa mahakama za kadhi ambalo
wanasema ni jambo la ajabu kwani ofisi ambayo haiundwi na sheria na
mamlaka ya kuengeneza kanuni za chombo.
Shekhe
Katimba alisema hata Mswaada wa kuikataa ,mahakama ya kadhi ijiendeshe
yenyewe badala ya kuendeshwa na Serikali ni Jambo ambalo haijawahi
kutokea Sehemu yeyote duniani Chombo, kama mahakama kujiendesha yenyewe.
Hata
Hivyo Shekhe Katimba aliwataka waislam kwa Ujumla kutoipigia kura ya
Ndio wakati wa kupigia kura katiba iliyopendekwa na Bunge mwezi March
mwaka huu kwakuwa katiba hiyo haina nia nzuri kwa Waislam nchiniwanahabari wakimsikiliza sheikh katimba kwa umakini
hayupo pichani
hayupo pichani
No comments:
Post a Comment