x
|
Wateja
watano wa Vodacom Tanzania wamejishindia milioni 1 kila mmoja wao
katika droo ya tatu na ya nne ya promosheni ya Jaymillions iliyofanyika
mwishoni mwa wiki.
Washindi
hao ni Janeth Peter Nganyange,mjasiriamali na mkazi wa Njombe,Stanley
Bagashe mkazi wa Shinyanga na
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Ibizamanta,Evarista Minja mkazi
wa Mwanza na mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustine, Ramadhan Hamis Maulid mkazi wa Dodoma ambaye ni
mkulima na Walter Minja ambaye ni Dalali.
“Nimefurahi
sana kwa kushinda milioni 1 kupitia promosheni ya Jaymillions kwa kuwa
kwa kiasi kikubwa fedha hizi
zitanisaidia kupanua biashara yangu na kununulia watoto wangu mahitaji
mbalimbali”.Anasema Janeth Peter Nganyange (40) mkazi wa Njombe mmoja wa
washindi.
Nganyange
amesema ushindi huu umeleta faraja kubwa kwake na familia yake
ikizingatiwa kwamba miezi mitatu iliyopita
alifiwa na mme wake na kumuachia familia yenye watoto wawili ambao
anahangaika nao kuwalea. “Mungu ni mkubwa na ushindi huu umeleta faraja
kubwa kwangu na nashukuru Vodacom kwa kubadilisha maisha yangu kwa maana
kwa muda mrefu nilikuwa nahangaika kutafuta
mkopo wa kuendeleza biashara yangu bila mafanikio”,Anasema.
Mteja
mwingine aliyejishindia milioni ni Walter Minja,mkazi wa Mbezi beach
jijini Dar es Salaam ambaye ni mwajiriwa
ambaye pia amesema kuwa amefurahia kuibuka mshindi hasa katika kipindi
hiki cha mwezi wa kwanza ambao unakuwa ni mgumu kwa watu wengi.
“Nafurahi
kujishindia milioni moja ya Jaymillions na itanisaidia sana kuvuka
katika mwezi huu mgumu wa Januari
ambao unakuwa na mambo mengi.Nashukuru Vodacom kuandaa promosheni hii
na nawahimiza watanzania wenzangu kushiriki kwa kucheki namba zao za
simu kama zimeshinda “.Amesema Minja.
Stanley
Bagashe mkazi wa Shinyanga na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya
Ibizamanta amesema amefurahi kupata
ushindi na fedha hizo zitamsaidia kutimiza ndoto yake ya muda mrefu wa
kufungua duka la M-Pesa “Fedha hizi zimekuja wakati muafaka naamini
ndoto yangu ya kufungua duka la M-pesa imetimia”.Alisema.
Mshindi
mwingine Evarista Amedeus Minja mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria
katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Augustine amesema amefurahia kujishindia milioni 1/- za Promosheni ya
Jaymillions na zitamsaidia kukamilisha masomo yake. “Fedha hizi
zimepatikana katika wakati mwafaka na zitanisaidia kulipia gharama za
hosteli na kumalizia utafiti wangu kwa kuwa sipati
mkopo kutoka Bodi ya Mikopo”.Alisema kwa furaha.
Naye Ramadhan Maulid alisema amefurahia ushindi huu na fedha hizo zitamsaidia katika shughuli zake za kilimo
“Nashukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii na nawasihi watanzania wenzangu tuendelee kushiriki “.alisema.
Mbali na washindi hao wa fedha taslim wateja wengi wamejishindia muda wa maongezi.
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu
(kushoto) akiwasiliana na mmoja wa washindi wakati wa kuchezesha droo
ya nne ya Jaymillions ambapo Jumla ya wateja watano wamejishindi
shilingi Milioni moja kila mmoja.Ili mteja kujua kama ameshinda
anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.kushoto kwake ni msimamizi
wa bodi ya michezo ya kubahatisha Mrisho Millao. Ili mteja kujua kama
ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda
15544.
Kwa upande wake ,Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia amewapongeza washindi na kuwahimiza
wateja wote wa Vodacom kuangalia namba zao kila siku kama zimeshinda kwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno JAY kwenda namba
15544 ili wasipoteze nafasi zao za kushinda.
“Promosheni hii inayoendelea ya
Jaymillions itakayofanyika kwa siku 100 mfululizo
inawahusisha wateja wote wa Vodacom ,kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa
kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki. Mara tu ujumbe huu
unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha
kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na
kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/-
tu”.Alisema.
Vodacom
imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/-
na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia
washindi elfu
kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-
| ||||
Msimamizi
wa bodi ya michezo ya kubahatisha Mrisho Millao(kulia)akihakiki
namba ya mmoja ya washindi toka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto) wakati wa kuchezesha droo ya nne ya
Jaymillions ambapo Jumla ya wateja watano wamejishindi shilingi Milioni
moja kila mmoja.Ili mteja kujua kama ameshinda
anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
.Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Mrisho Millao
aliyesimama(kushoto) akionyeshwa namba ya mmoja wa washindi na
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina
Nkurlu(katikati)wakati wa kuchezesha droo ya nne ya promosheni ya
Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika mwishoni mwa
wiki,wengine
katika picha(kulia) ni mtaalamu wa mifumo ya kompyuta Michael
Kanakakis,waliokaa (kutoka kulia) ni Dimitrios Lintis na Zakaria
Kanyi.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda
No comments:
Post a Comment