Friday, 23 January 2015

MAMA MKULIMA ASHINDA MIL. 10/- ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM

 


Mkazi wa kijiji cha Inyonga Mkoani Rukwa Hyness Petro Kanumba (20) leo ameibuka mshindi wa kwanza wa Milioni 10 katika droo ya nane ya promosheni ya Jaymilions inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Hyness ambaye ni mama mwenye mtoto mmoja pia mkulima amesema kuwa amepokea taarifa hizo kwa furaha akiwa shambani katika kazi zake za kilimo, kwa kuwa anaamini Mungu amemuona na kwa ushindi huu utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

“Kwa muda mrefu nimekuwa nikihangaika na kazi za kilimo na kukumbana na changamoto nyingi kama vile  ukosefu wa masoko ya mazao ,pembajeo za kisasa .Kwa ushindi huu naamini nitaboresha shughuli zangu za kilimo ikiwemo kuanzisha biashara ndogo na kuboresha makazi yetu,nashukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii”.Alisema Hynes kwa furaha.

Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi,Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote wa Vodacom kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda.

Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja watano wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja  na  maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya nane hivyo bado kuna mamilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha  kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544. 

 Promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions  inawahusisha wateja wote wa Vodacom,kiasi kikubwa cha fedha kitaendelea kutolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu”.Alisema.

Vodacom  imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-

No comments:

Post a Comment