Naibu katibu mkuu wa CUF bi MAGDALENA SAKAYA akizungumza na wanahabari mapema leo makao makuu ya chama hicho juu ya uapishwaji wa viongozi wa serikali za mitaa unaoendelea nchini |
Chama cha wananchi CUF kimetangaza kulaani vikali zile wanazoziita vurugu na hujuma wanazodai zinafanywa na chama cha mapinduzi CCM katika zoezi la uapishwaji wa viongozi wa serikali za mitaa linaloendelea nchi nzima.
Akizugumza
na wanahabari Naibu katibu mkuu wa chama hicho bi MAGDALENA
SAKAYA amesema kuwa mkakati wa CCM ulianza katika zoezi la uchaguzi huo
katika kubatilisha matokeo ambayo chama cha CUF kilishinda na sasa CCM
imeamua kutumia mbinu chafu ya kutaka kuwaapisha viongozi wao ambao
hawakushinda katika matokeo ya uchaguzi huo.
Akitaja
maeneo kadhaa ambayo wagombea wa CUF walishinda lakini wasimamizi wa
uchaguzi wakashindwa kuwatangaza na badala yake kuwapeleka viongozi wa
CCM kwenda kuapa kuwa ni mtaa wa mwinyimkuu kata ya mzimuni kinondoni
ambapo mgombea wa cuf HASSAN ABUBAKARY alishinda katika uchaguzi huo
lakini msimamizi wa uchaguzi huo aliitisha uchaguzi mwingine uchaguzi
ambao uligomewa na wanachi na badala yake akatangazwa mgombea wa CCM,
FUNUA ALLY kuwa ndiye mshindi.
Mtaa
mwingine ni mtaa wa ukwamani kata ya kawe ambapo mgombea wa cuf
alishinda lakini fomu za ushindi hazikusainiwa hadi leo na badala yake
mgombea wa ccm ndiye ametangazwa mshindi. Aidha maeneo mengine ambayo
amesema yamefanyika mchezo huo ni mtaa wa msisiri kata ya
mwananyamala,mtaa wa kiwalani kata ya migombani,mtaa wa kigogo
fresh,pamoja na mtaa wa malapa,kinyerezi,migombani, bunda mara,pamoja na maeneo mengine ambayo wanachi wanazidi kurepoti tukio hilo.
Aidha
bi SAKAYA amesema kuwa kutokana na uchakachuaji huo mkubwa ni wazi kuwa
lazima viongozi waliohusika ikiwa ni pamoja na mkurugenzi wa uchaguzi
wa kinondoni na waziri husika wawajibike kwa kuachia nafasi zao mara
moja kwani ni aibu kwa taifa kuwaibia wanachi kwa kiasi hicho.
Aidha
amekionya chama cha mapinduzi kwa kile alichosema hii ni mipango yao ya
kuiviuruga Amani ya Tanzania kuwa nguvu ya umma waliyokutana nayo
uchaguzi huu itakuwa ni Zaidi katika uchaguzi ujao hivyo mbinu chafu
hazitavumilika hata mara moja.
Kumeshughudiawa
vihoja katika zoezi la kuapishwa viongozi wa serikali zaa mitaa jijini
Dar es salaam ambapo katika ukumbi wa landmari pamoja na kule ilala
juzi kulizuka fujo kubwa baada ya kugundulika kuwa kuna viongozi ambao
hawakushinda ila walipewa barua za kwenda kuapishwa jambo ambalo wanachi
hawakuliafiki na kusababisha fujo kubwa
No comments:
Post a Comment