Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Shinyanga, Tabora na Simiyulengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco)
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya
watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na
Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na
Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini
inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na
Taneesco.
Meneja
wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo
mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na
wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani)
Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka kampuni ya
Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika kijiji
cha Nyamikoma kilichopo wilayani Busega Bw. Steve Thomson (kushoto)
No comments:
Post a Comment