Mechi ya
kiporo katika michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam kati ya klabu za Panama
FC dhidi ya Boom FC, itapigwa kesho kwenye uwanja wa Airwing,ukiwa ni mchezo
ambao utatoa fursa kwa DRFA kutangaza timu 18 zilizofanikiwa kutinga katika
hatua ya 18 bora ya michuano hiyo.
Michuano
hiyo ya ligi mkoa wa Dar es salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36,inaingia
katika hatua ya mwisho katika hatua ya mwisho ambayo itatoa wawakilishi wa mkoa
Dar es salaam katika ligi ya mabingwa wa mikoa ya TFF.
Kivumbi cha
hatua ya 18 bora,kitaanza kutimka tarehe 4 /02/2015.
LIGI YA WANAWAKE YA MKOA WA DAR ES
SALAAM.
Ligi ya soka
la wanawake kwa mkoa wa Dar es salaam inataraji kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao
kwa kushirikisha jumla ya timu 12,zitakazoumana kuwania ubingwa huo.
Itakumbukwa kwamba
DRFA iliamua kusogeza mbele mashindano hayo ambayo yalikuwa yaanze januari
16/2015,kutokana na upungufu wa wachezaji kwa timu husika ambao wengi wao wanashiriki mashindano ya
kuwania kombe la Taifa Wanawake,ambayo sasa imeingia katika hatua ya robo
fainali.
Timu zote 12
zitakazoshiriki ligi hiyo ya mkoa wa Dar es salaam,zitawekwa hadharani hapo
baadaye.
No comments:
Post a Comment