Pichani ni kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga picha na maktaba
Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamanda Mohammed Mpinga
amesema katika mahojiano maalum kuwa madereva wameanza kuelewa kuwa
tabia ya
kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (SMS) wanapokuwa
wanaendesha vyombo vya moto ni uvunjaji wa sheria za barabarani.
Mafanikio hayo yamekuja baada ya kampeni endelevu ya usalama barabarani kufanyika mikoa mbalimbali Tanzania
Kampeni
hii ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria
za usalama barabarani ilizinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo
ya Ndani, Mheshimiwa Mathias Chikawe hivi karibuni na sasa imeanza
kuonyesha mafanikio.
“Tangu
kuanza kampeni hii ambayo tayari imefanyika katika mikoa mbalimbali
ujumbe umeanza kuwafikia madereva kwa kuwa wanapokuwa wanatumia simu na
kuwaona askari wa usalama barabarani wanashtuka na kuacha kuzitumia.
Hii inadhihihirisha kuwa wameanza kuelewa kuwa ni kosa kufanya hivyo na
tutazidi kuwapatia elimu na wanaovunja sheria kuchukuliwa hatua kwa
mujibu wa sheria,” alisema Mpinga.
Alisema
madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali
zinazoendelea kutokea kila siku zitapungua na aliipongeza kampuni ya
Mawasiliano
ya Vodacom Tanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika
kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu .
Kwa
upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia, alisema Vodacom itaendelea
kushirikiana
na serikali kuunga mkono jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii
kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi
maisha murua na marefu. “Tunatoa rai kwa madereva wote kuzingatia kauli
mbinu ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama barabarani mwaka
huu isemayo ‘Maamuzi yako barabarani ni hatma yetu - Fikiri kwanza’.”
Aliongeza
kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za
kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni
ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Alisema
kampeni hii itaendelea kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini ili
ujumbe uwafikie madereva wengi ambako hadi kufukia sasa imeshafanyika
katika
mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Pwani, Morogoro,
Dodoma,Singida na Shinyanga.
Katika
kampeni hizi wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa
usalama barabarani na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
wamekuwa
wakifanya uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu
wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za
kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa
wanaendesha vyombo vya moto pamoja na zoezi la kupima madereva kubaini
kama wanatumia vilevi linafanyika ambapo wadereva wanaokutwa
wanaendeshwa vyombo vya moto wanachukuliwa hatua kali za kisheria.
Baadhi
ya madereva na abiria ambao wameshuhudia kampeni hii ikifanyika
katika sehemu mbalimbali wamesema ni ya muhimu na itasaidia kupunguza
ajali
nchini. “Hivi sasa ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasababishwa
na uzembe wa madereva,kampeni hizi zikiendelea zitapunguza ajali kwa
kiasi kikubwa,” alisema Bi. Zainab Khalfan mkazi wa Singida.
Naye
James Mshiu mkazi wa Dar es Salaam alilipongeza Jeshi la Polisi na
wadau wa kampeni hii kuwa kwa kiasi kikubwa imepunguza matukio ya ajali
katika
msimu wa Krismas na mwaka mpya. “Katika miaka iliyopita kumekuwepo na
matukio mengi ya ajali katika msimu wa sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya
lakini mwaka huu uhamasishaji wa kuzingatia sheria za barabarani
uliofanyika katika kipindi hiki kwa kiasi kikubwa
umepunguza matukio ya ajali za barabarani,” alisema.
No comments:
Post a Comment