Friday, 20 March 2015

KOVA AWARUDIA CHADEMA JUU YA MPANGO WA KUMUUA DK SILAA

Kamishna wa Kanda Maalum ya Polis Mkoa wa Dar es Salaa
Suleiman Kova\
Akizungumza na Waandishi wa Habari
mda huu jijini Dar 
JESHI la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha kuhusika kwa Idara  Usalama wa Taifa katika mipango ambayo inaidaiwa ya kutaka kumuua Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa.
 
      Kauli ya jeshi la polisi kanda hiyo ni kama inakuwa inamjibu Mjumbe wa kamati kuu ya chadema CC,Mabere Marandu ambaye katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari alimtuhumu Naibu mkuu wa idara ya Usalama mkoa wa Kinondoni Elisifa Ngowi kuandaa mipango miovu kwa dokta Slaa akishirikiana na Mlinzi wa Katibu huyo-
 
     Bwana Khalid Kagenzi pamoja na Makumu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara,Philip Mangula.
 
       Akikanusha taarifa hizo leo Jijini Dar es Salaam,Kamishna wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova wakati na mkutano na vyombo vya Habari amesema Jeshi hilo limefanya uchunguzi wakina ikiwemo kuchukua taarifa upande wa chama cha Chadema na Mlinzi wa Dokta Slaa na kubaini hakuna ukweli idara ya Usalama wa Taifa kuhusika.
 
   “Kiukweli bado tunaendela na uchunguzi ikiwemo kuwahoji watu wote wanaotuhumiwa tumebaini kwa dhati kabisa hakuna mtu yeyote wa usalama wa Taifa kuhusika katika mipango ya kumdhulu Dokta Slaa na tena nomba iwe hivyo”Amesema Kamishna Kova.
 
    Kamishna Kova,ameongeza kuwa kwa sasa bado wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo na uchunguzi ukikamilika watafawakisha watu mahakamani bila hata kumwogopa mtu yeyote.
 
   “Mbona nyie waandishi wa habari mnaangali upande wa usalama mbona amtuhoji kama tumemuhoji nani upande wa Chadema lakini ukweli ni kwamba tunaendelea na uchanguzi ikiwemo mahojiano ya kina kati ya watuhumiwa wote wale wanao tuhumiwa na chadema pamoja na Mlinzi wa Dokta Slaa bwana Kagenzi”
 
       “Nawahakikishia uchanguzi ukikamilika lazima wafikishwe mahakamani na sisi hatutanii”Ameongeza Kamishna Kova.
 
     Katika hatua nyingine Jeshi hilo kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikiria watu wawili waojiita ni viongozi wa watu waliopata mafunzo ya mgambo kwa kosa la kuratibu na kuongoza vikao vya uchochezi vya mgambo dhidi ya serikali.
 
     Kwa,mujibu wa Kamishna Koma amewataja watuhumiwa kwa majina ni  Mathias lubega miaka 43,mkazi wa bunju ambaye amekamatwa maeneo ya Mission pup huko mbagala mkoa wa polisi Temeke.
 
      Wa pili ni Mohamed  Ally miaka 38 naye pia ni mkazi wa Mbagala .
 
    Mbali na kuwakamata watuhumiwa hao kamishna Kova alithibitisha kuwa jeshi hilo katika msako wake mkali limefanikiwa kukamatwa kwa noti bandia za dolla za kimarekani azipatazo 426 ambazo ni noti 36 ni za dolla 100 na noti 390 za dolla 50.
 
        Kamishna kova pia aliwataja kwa majina watuhumiwa ambao pesa hizo zilikutwa kwao ni Ramadhani Mhambo miaka 34,mkazi wa Mwanayamala jijini hapa,Eliazr Jackob Nkurarumi na Juma Mohamed mrundi miaka 25 ambaye ni mlinzi  wa Colombia Hoteli.

    Mbali na watuhumiwa hao Kamishna Kova aliwataja watuhumiwa wengine ni Rajabu Nassor vmiaka 30 ambaye ni fundi simu,Mkazi wa mwananyamala kwa sindano ambapo wote walipkuwa kwenye makazi yao walikutwa na fedha hizo bandia.

BEACH SOCCER YAWASILI SALAMA MISRI


Timu ya Taifa ya soka la Ufukweni (Beach Soccer) imewasili salama jijini Cairo nchini Misri tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli.

Msafara wa timu ya soka la Ufukweni ulipokelewa na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania waliopo nchini Misri,  pamoja na viongozi wa chama cha soka nchini Misri (EFA).

Leo jioni kikosi kinatarajia kufanya mazoezi mepesi, kabla ya kesho kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja utakaofanyika mchezo siku ya jumapili.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF linaitakia kila la kheri timu ya soka la ufukweni katika mchezo wake wa marudiano siku ya jumapili dhidi ya Misri.


Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kufanyika siku ya jumapili katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam siku ya jumatatu Machi 23 mwaka huu kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mchezo huo wa fainali utazikutanisha timu za Mbao FC ya Mwanza dhidi ya Kiluvya United FC ya Pwani, ambapo mshindi wa mchezo ndio atakua Bingwa mpya wa Ligi Daraja la Pili.

Jumla ya timu nne tayari zimeshapanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutoka Ligi Daraja la Pili (SDL) ambazo ni Kiluvya United ya Pwani, Mji Njombe ya Njombe, Mbao ya Mwanza na Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma.

Wednesday, 11 March 2015

MLINZI WA DK SILAA AELEZA UKWELI JUU YA SHTUMA ZAKE

Mlinzi huyo wakati akizungumza na wanahabari akionyesha majeraha aliyoyapata wakati wa kupokea kipigo hicho
Aliyekuwa mlinzi binafsi wa katibu mkuu wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA dk WILBROAD SLAA kwa jina la Khalid Kangezi leo ameibuka na kukanusha taarifa zilizotolea na chama chake kuwa alikuwa anakula njama za kumuua katibu mkuu huyo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma za wazi ndani ya  chama hicho.


Akizungumza kwa uchungu ndani ya ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam mbele ya wanahabari leo amesema kuwa kilichotokea hakijui ila anashangaa kuwa chama kimeamua kumtenda na kumpiga sana wakimtuhumu kutaka kumuua kiongozi huyo jambo ambalo amesema kuwa ni la kushangaza na halina ukweli wowote ule.
Amesema kutokuelewana kwake na katibu mkuu wa chama hicho kiulianza pale alipokuwa na kupishana kwa maneno kati yake na mke wa docta slaa ambapo docta alimuamuru aende kwa mke wake akamalize ugomvi wake na mke wake ndipo aendelee na kazi jambo ambalo amesema kuwa alishangaa kuwa kuwa hakuwa na ugomvi na mke wa docta slaa na hakuweza kufanya hivyo.

Amesema kuwa siku ya jumamosi aliitwa makao makuu ya chama kwa mualiko kuwa kuna kikao maalum na mwenyekiti wa chama hicho na alipofika aliingizwa chumbani ambapo aliwakuwa vijana watano wa chama hicho ambao amewataja kwa majina na bila kumjuza kitu chochote walianza kumpiga mateke,kumtesa,kumvua nguo,kumwagia maji huku wakimtuhumu kuwa amepewa sumu na viongozi wa chama cha ccm ili amuue katibu mkuu dk slaa.
Amesema kuwa baada ya kupokea kipigo kikali kwa zaidi ya masaa sita kutoka kwa vijana hao wa chadema wakimtaka kukiri kuwa anatumika na viongozi wa ccm na usalama wa taifa kukihujumu chama nayeye kukataa walianza kushauriana kuwa wamuue ili waondoe ushahidi wake na ndipo walipanga wampeleke mstuni kwenda kumuua.


Amesema kuwa baada ya kuona kuwa hali inaanza kuwa mbaya na wanaweza kuua kweli aliamua kudanganya ili kuokoa maisha yake kwa kukiri kuwa anatumika na chama cha mapinduzi na wakuu wa idara ya usalama wa taifa kutaka kumuua kiongozio wa chadema docta slaa na aliwaeleza hivyo ili wapunguze makali ya kumtesa ambapo amesema kuwa baada ya kusema hivyo viongozi hao walipunguza makali ya kumpiga na wakatoka nje kuanza kushauriana cha kumfanya,

Anaendelea kueleza kuwa wakati hayo yanafanyika makao makuu ya chama hicho katibu mkuu wa chama hicho dk slaa na viongozi wengine wa chama hicho walikuwa katika ofisi zao na walikuwa wanasikia kila kitu ambacho kinaendelea lakini hawakufanya jambo lolote zaidi ya kaucha aendelee kushushiwa kipigo kutoka kwa vijana hao.


Aidha baada ya muda kadhaa majira ya saa sita usiku vijana hao walimchuukua katika gari nyeusi hadi katika hoteli moja sinza na kumlaza hapo hadi asubuhi,ambapo ilipofika asubuhi vijana wale wakamtaka aandike barua ya kukiri kuwa amepewa sumu na viongiozi wa ccm ili amuue dk slaa lakini yeye alikataa na ndipo walipoleta vifaa ambavyo walikuwa wakivitumia  katika utesaji ili kuanza kumtesa upya na ndipo alipoaamua kuandika barua ya kukiri kuwa anatumika na viongozi wa ccm na usalama wa taifa kukihujumu chadema.


Barua hiyo ambayo ndiyo iliyotumiwa na kiongozi wa chadema MABERE MARANDO kuwaeleza wanahabari kuwa mlinzi huyo alikuwa na njama za kumuua dk slaa ilikuwa inakiri kuwa amekuwa akitumika na viongozi hao katika kukihujumu chama.


Mlinzi huyo ambaye alikuwa akizungumza huku akiwa na machungu amesema kuwa yeye alikuwa akijitolea kumlinda docta slaa bila hata malipo kwani alikuwa anafanya hivyo kwa imani kuwa anawasaidia watanzania .

TANZANIA KUIVAA MISRI IJUMAA BEACH SOCCER


Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kucheza na timu ya Taifa ya Misri siku ya ijumaa majira ya saa 10 kamili jioni, mchezo utakofanyika katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini Dar es salaam.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo, ambapo kwa takribani wiki mbili kipo kambini Bamba Beach wakijifua kwa mchezo huo.

Tanzania ilifuzu hatua ya pili baada ya kuiondoa timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12 -9, na endapo itafanikiwa kuwaota Misri, itafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za soka la Ufukweni zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli mwezi April  mwaka huu.

Waamuzi wa mchezo huo ni Eid Haitham Eid Hassan (Sudan), mwamuzi msaidzi wa kwanza  Abaker Mohamed Bilal (Sudan), mwamuzi msaidizi wa pili Abdalla Hassain Hassaballa, mtunza muda (time-keeper) Boubaker Bessem (Tunisia) wakati kamisaa wa mchezo huo ni Khiba Herbert Mohoanyane kutoka Lesotho.

Nayo timu ya Taifa ya Misri inatarajiwa kuwasili Dar es salaam kesho (jumatano) mchana, ambapo itafikia katika hoteli ya Double Tree by Hilton iliyopo Masaki, huku waamuzi wa mchezo huo wakitarajiwa pia kuwasili kesho na kufikia katika hotel ya Protea Oysterbay.

Aidha siku ya alhamis makocha wa timu zote wataongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume kuanzia majira ya saa 5 kamili asubuhi.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika wiki ijayo nchini Misri kati ya Machi 20,21 na 22 mwaka huu.

Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), inaitakia kila la kheri na ushindi timu ya Taifa ya soka la ufukweni (Beach Soccer) katika huo dhidi ya Misri.
Wakati huo huo michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyokuwa iichezwe kesho (jumatano)  kati ya JKT Ruvu dhidi ya Young Africans katika uwanja wa Taifa, na Mgambo Shooting dhidi ya Azam FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga imeahirishwa  na sasa mechi hizo zitapangiwa tarehe nyingine.

 MKUTANO MKUU WA TFF
Maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka wa TFF utakaofanyika mjini Morogoro kati ya Machi 14,15 mwaka huu katika Ukumbi wa Morogoro Hotel yanaendelea vizuri.
 Agenda za mkutano mkuu ni:
1.Kufungua Mkutano
2. Uhakiki wa Wajumbe
3. Kuthibitisha Ajenda.
4. Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita.
5. Yatokanayo na Mkutano uliopita.
6. Hotuba ya Rais.
7. Ripoti kutoka kwa Wanachama
8. Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
9. Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013.
10. Kuthibitisha ripoti ya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu.
11. Kupitisha bajeti ya 2015
12. Marekebisho ya Katiba
13. Mengineyo
14. Kufunga Mkutano.

Monday, 9 March 2015

Wateja wa Vodacom M-PESA sasa kutuma pesa nchini Kenya

Kampuni kubwa za mawasiliano Afrika mashariki Vodacom Tanzania na Safaricom ya Kenya leo zimezindua huduma mpya ambapo kuanzia sasa zaidi ya wateja Milioni 7 wa M-Pesa waVodacom Tanzania wanaweza kutuma  na kupokea pesa  kwa watumiaji zaidi ya milioni 18 wa Safaricom M-Pesa ya Kenya. Huduma hii mpya ambayo imebuniwa na makampuni haya yanayoongoza kutoka huduma za mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki itawawezesha wateja  wake kutuma pesa kwa kutozwa viwango  sawa na vinavyotumika katika nchi husika.




001.MkurugenziMtendajiwa Vodacom Tanzania, Rene Meza, akiongeanawaandishiwahabariwakatiwauzinduzirasmiwakutumanakupokeapesanchini Kenya kwanjiaya M-PESA. Uzinduzihuoulifanyikajijini Dar es Salaam.




. MkurugenziwaMifumoyaMalipowaBenkiKuuya Tanzania, Bernard Dadi (katikati) akifafanuajambokwaMkurugenziMtendajiwa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto) baadayauzinduzirasmiwakutumanakupokeapesanchini Kenya kwanjiaya M-PESA uliofanyikajijini Dar es Salaam. KulianiMenejawaMifumoyaMalipowaBenkiKuu Tanzania, James Masoy.
 Dar es Salaam, Tanzania, 


Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hii,Mkurugenzi
 Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza alisema kuwa takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa mwaka 2013  zaidi ya shilingi bilioni 200  zilitumwa kutoka Tanzania kwenda Kenya halikadhalika zaidi ya bilioni 1 zilitumwa kutoka Kenya kuja Tanzania. 

“Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa fedha karibu shilingi bilioni 200 zilizotumwa nchi Kenya kutoka Tanzania zilitumwa kwa njia rasmi za utumaji fedha na inakadiriwa kuwa kiasi cha fedha hizo zaidi ya mara mbili zimetumwa kwa njia zisizo rasmi za utumaji fedha ikiwemo kutumia madereva na makondakta wa  mabasi au kutumia ndugu na marafiki wanaosafiri”amesema Meza.


“Tumeona ugumu wanaokabiliana nao wateja wetu kutuma fedha katika nchi jirani  ya Kenya na tumepata suluhisho kwa kuleta huduma hii ambayo ni ya haraka na uhakika.Kuanzia leo hakuna sababu ya kutuma pesa  kwa kumtumia dereva au kondakta wa basi au kutozwa gharama kubwa kutoka taasisi za kifedha unapolipa karo za watoto wanaosoma nchini humo,unaweza sasa kufanya  malipo na kulipa ankkra mbalimbali kutoka pochi ya M-Pesa ukiwa umetulia nyumbani kwako,”amesema Meza.


Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Safaricom Bob Collymore alisema “Tunaamini tumefungua ukurasa mpya wa kuendeleza huduma ya M-Pesa kwa kuwezesha wateja wa Kenya na Tanzania kutumia huduma hii katika kutumiana fedha na kufanya malipo  katika nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya”.Alisema

Alisema katika awamu hii ya kwanza iliyozinduliwa leo inawawezesha wateja kutuma pesa Kenya kama ambavyo wamekuwa wakituma hapa nchini, tofauti itakuwa wakati wa kutuma pesa kwenye simu kutakuwepo na kipengele kinachoonyesha kuwa wanataka kutuma pesa kwa M-Pesa ya Kenya na kuandika namba za mpokeaji kwa kutumia namba za Kenya yaani +254 na katika awamu ya pili ya huduma hii wateja wa Safaricom ya Kenya wataweza kutuma pesa kwa wateja wa Vodacom Tanzania kupitia huduma hii.”

Huduma ya M-Pesa inatolewa na makampuni ya Vodacom Tanzania na Safaricom ya Kenya yote yakiwa makampuni  makubwa yanayotoa huduma ya mawasiliano katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.Wakati Vodacom inatoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwa asilimia 65 nchini. “Ushirikiano huu wa mtandao wetu wa M-Pesa wenye mawakala zaidi ya 75,000 nchini Tanzania utawarahishia  wateja wetu kupata huduma bora ikiwemo kufanya mihamala yao ya fedha kwa urahisi na  tumejipanga kutoa huduma bora kwa wateja kwa muda wote wa masaa 24 kila siku.”Alisisitiza Meza.

“Kenya ni moja ya nchi inayofanya biashara  kwa kiasi kikubwa na Tanzania ndio maana huduma hii imeanzia nchini humo na kuzidi kuunganisha  na kuimarisha ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Tunaamini kuwa mawasiliano hayana mipaka kwa kuwa kwa kuwa huwaunganisha watu na jamii na jamii na kusaidia kuharakisha maendeleo na ndio maana Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika sekta hii”.Alisisitiza Meza.


Kuna zaidi ya Wakenya 300,000 wanaotuma fedha nchini kwao kwa kutumia njia zisizo  rasmi na salama kama vile kuwatumia makondakta na madereva wa mabasi vilevile kuna watanzania wengi wanasomesha watoto wao nchini Kenya ambao nao wamekuwa wakipata shida kutuma fedha nchini humo.”Kwa kuanzia leo huduma kwa wafanyabiashara kulipana zimerahisihwa ikiwemo kulipa karo za shule na vyuo na mihamala mingine,Huduma ya M-Pesa imerahisisha kila kitu na kuzidi kufungua milango ya  biashara na ushirikiano”Aliongeza kusema Meza.


Alimalizia kusema kuwa huduma hii itafanya maisha ya watumiaji wake kuwa murua kwa kuwa watatuma fedha zao  na kuwa na uhakika wa kuwafikia walengwa moja kwa moja na  ni njia ya uhakika na yenye usalama inayowapunguza adhabu kubeba  kiasi kikubwa cha fedha mifukoni na kwenye mabegi pia walengwa watapokea malipo kwa viwango vya ubadilishanaji sahihi visivyobadilika kila siku

SIMBA, YANGA ZAINGIZA MIL 436


Mechi no.117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa jana, imeingiza jumla ya sh. milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C, Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani waliingia watazamaji 36,693.

Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600.

Mgao wa Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh. 11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata sh.81,727.83.

Wakati huo huo Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho siku ya jumanne katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.

Siku ya jumatano JKT Ruvu watawakaribisha Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Azam FC.

Aidha mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) barani Afrika kati ya Young Africans dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbabwe, itafanyika siku ya jumapili Machi 15, 2015 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Sunday, 8 March 2015

Vodacom watoa wito kuchangisha fedha kwa wahanga wa mafuriko

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeeleza kuguswa na tukio la mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambayo imesababisha vifo vya watu 42 na wengine mamia kujeruhiwa na kuacha familia nyingi zikiwa hazina makazi na kuanzia leo imeanza kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tukio hilo.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema anawaomba watanzania wote wanaotaka kuchangia wahanga hao kutuma fedha zao kwenye namba  maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya 155990.


“Tukiwa kama kampuni ya mawasiliano tumeguswa na tukio hili na tunawapa pole waathirika wote na tunaungana na wakazi wa kahama kwa janga hili tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kupitia kitengo chetu cha kusaidia jamii cha Vodacom Foundation na tunawaomba watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao na tutahakikisha tunaifikisha sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu ambao wako katika mazingira magumu na wanahitaji msaada wa haraka”.


Alisema kupitia njia hii ya namba maalumu ya”Red Alert” 155990 ya kuchangisha fedha imewahi kurahishisha uchangishaji wa fedha kwa waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na kuathiri wananchi moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto jijini Dar es Salaam na aliwahimiza wananchi kuitumia kama njia rahisi ya uchangiaji.


Hata hivyo unaweza kuchangia  kwa kuponyeza  *150*00# alafu unachagua namba 4 yaani Lipa kwa M PESA baada ya hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba 155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.

Wednesday, 4 March 2015

WADAIWA SUGU BILI WASABABISHA WANANCHI KUKOSA MAJI KATIKA MJI WA MPWAPWA, WAMO NMB


  • 18 

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa huku akiwa ameshikilia nyaraka za wadaiwa sugu wa bili za maji katika mji wa Mpwapwa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji katika mji huo Bw. Shadrack Mtemba. 



Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba amesema mradi huo ni mkubwa na unatosheleza mahitaji ya maji kwa  wananchi wa mji wa Mpwapwa. tatizo ni kwamba Taasisi na makampuni mengi hayalipi bili zao kwa wakati jambo ambalo linafanya uendeshaji kuwa mgumu huku akikabidhi nyaraka za wadaiwa hao mbele ya Kinana



 19 

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji katika mji wa Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa mara baada ya kukabidhi orodha hiyo ya wadaiwa sugu wa bili za maji kwa Mkuu wa mkoa wa Galawa ambaye anaonekana akiipitia orodha hiyo.

1 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye mfereji wakati alipokuwa akivuka mfereji huo akielekea akishiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa katika kijiji cha Berege Mpwapwa huku akiwa ameongozana na Bi Anna Mlewa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma ,  3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa wa pili kutoka kushoto na, wengine anayefuata ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Chiku Galawa (kulia) ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka mara baada ya kushiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa katika kijiji cha Berege kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa. 5 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga mfereji wa maji katika shamba la kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga kijiji cha Msagali. 6 

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Mazae kata ya Kisokwe kushiriki ujenzi wa zahanati. 7

Monday, 2 March 2015

TFF YATUMA SALAM ZA PONGEZI FMF


Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Boubacar Diara wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Mali (FMF) kwa kutwaa Ubingwa wa Afrika kwa vijana U17.
Katika salam zake mh. Malinzi amesema mafanikio mazuri waliyoyapata  FMF yametokana na uongozi bora, kamati ya utendaji na mipango thabiti waliyoiweka katika soka la Vijana.
Kwa kutwaa Ubingwa wa vijana Afrika U17, Mali wamepata nafasi ya kuliwakilisha Bara la Afrika kwenye fainali za U17 za Dunia nchini Chile pamoja na nchi za Afrika Kusini,Guinea na Nigeria.
Mali wametwaa Ubingwa wa vijana Afrika U17 baada ya kuifunga timu ya taifa ya vijana ya Afrika Kusini (Amajimbo's) kwa mabao 2-0.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania wanawapa pongezi  Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Mali (FMF) wa kutwaa Ubingwa huo.
Aidha Rais Malizi pia ametuma salam za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Afrika Kusini (SAFA) Bw. Dany Jordaan kwa timu ya Amajimbo's kushika nafasi ya pili.
Amajimbo's ndio timu pekee kusini mwa Bara la Afrika watakaowaklisha kwenye fainali za U17 za Dunia nchini Chile.
  
BEACH SOCCER YAENDELEA KUJIFUA BAMBA BEACH
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Sola la Ufukweni (Beach Soccer) iliyoingia kambini mwishoni mwa wiki Bamba Beach Kigamboni, inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Taifa Soka la Ufukweni ya Misri mwishoni wiki ijayo.
Maandalizi ya mchezo dhidi ya timu ya Misri yanaendelea vizuri Bamba Beach Kigamboni chini ya kocha mkuu John Mwansasu ambaye aliingia kambini mwishoni mwa wiki na wachezaji 14.
Mchezo wa kwanza unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya Machi 13 katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini  Dar es salaam na marudio yake kufanyika baada ya wiki moja nchini Misri.
Tanzania ilifanikiwa kufuzu hatu ya pili baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12- 9, mchezo wa awali Mombasa Tanzania ilishinda kwa mabao 5-3, na mchezo wa marudiano uliofanyika klabu ya Escape 1 kuibuka na ushindi wa mabao 7-6.
Fainali za Mataifa Afrika kwa Sola la Ufukweni (Beach Soccer) zinatarajiwa kufanyika mwezi April 2015 katika Visiwa vya Shelisheli.

VPL KUENDELEA JUMATANO
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi katika viwanja vitatu tofauti siku ya jumatano, Mkoani Morogoro katika uwanja wa Manungu-Turiani timu ya Mtibwa Sugar watawaribisha majirani zao timu ya Polisi Morogoro.
Katika uwanja wa Azam Complex - Chamazi maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha maafande wenzao timu ya Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya, huku timu ya Ruvu Shooting wakiwa katika Uwanja wa nyumbani Mabatini - Mlandizi kuwakaribisha timu ya Ndanda FC.