Wednesday, 23 July 2014

M.A.T WAOMBA MASHIRIKA MBALIMBALI KUINGILIA KATI UTUPAJI WA MIILI NA MASALIA YA BANADAMU BILA UTARATIBU



Chama cha madaktari Tanzania M.A.T kimevitaka vyombo husika kama jeshi la polisi,wizara ya afya,baraza la madaktari Tanzania,tume ya usimamizi ya vyuo vikuuTCU,taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR, kuchukulia hatua stahiki kwa mtu au taasisi iliyotupa na kutekeleza mabaki ya viungo mbalimbali vya miili ya binadamu vinavyoaminika kuwaq vilikuwa katika mafunzo na utafiti

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini dare s saalam rais wa madaktari Tanzania dr Primus Saidia alisema kwamba kutokana na tasnia ya tiba  ni utaratibu unaokubalika duniani kote ikiwemo Tanzaniakutumia miili  na viungo asili vya binadamu katika  kufundisha na kufanyia utafiti

;miili na viungo hivi vinatumika kwa heshima  kubwa kama waalimu wa kwanza katika mafunzo ya utafitiza tiba ya mwanadamu  ambapo tafiti hizo ndio njia kuu katika kukuza ufahamu wa mwili wa binadamu na hivyo kuboresha utoaji wa huduma za afya;alisema dk Saidia

Halikadhalika alisema kitendo hicho kimekiuka kwa kiasi kikubwa  sheria,taratibu,na utu wa binadamu na maadili ya ufundishaji na taaluma ya udaktari kwa kitendo hicho cha kutupa cha kutupa miili hiyo

;watu na taasisi zilizohusika na kitendo hiki imepoteza sifa ya kufanya utafiti au kutoa mafunzo ya kidaktari kwa kutumia miili ya binadamu ,hii ina maana kuwa kama taasisi ya utafiti imepoteza sifa ya utafiti  na kama ni mafunzo imepoteza sifa ya kutoa mafunzo ya tiba,na kama ni hosptali imepoteza sifa ya kutoa tiba ka binadamu;alisema rais huyo

Halikadhalikaalibainisha taratibu za kuipata miili,kusafirisha ,kuhifadhi,kutumia na kustiri mabaki baada ya matumizi hufanyika kwa kufuata sheria ,maadili,afya ya jamii.utamaduni,miiko,na heshima kwa utu wa binadamu na jamii husika

;Kitendo kama hiki kwa nchi nyingine kinatosha kabisa kuifungia taasisi  kuendelea na mafunzo na tafiti au huduma za kibinadamu ;alisemadk saidia

Halikadhalika rais waserikali ya wanafunzi chuo cha muhimbili bwana Alex Elifuraha ameulalamikia uongozi wa wizara ya afya kwa kushindwa kuboresha na kufanyia marekebisho mashine ya kuchomea mabaki ya miili na viungo vya binadamu kwa kitaalam INCINIRATURE katika ospitali kuu ya muhimbil

TASO KUTOA ELIMU KWA WANALINDI KUHUSU UBORESHAJI WA KILIMO.




kajula
Iman Kajula Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo mchana kuhusu maonyesho ya NANE NANE yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mkoani Lindi, Kutoka kulia ni Mathew Gugae Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara EAG Group na katikati ni Engerbelt Moyo Mwenyekiti wa TASO.

  
Na Rose Masaka -MAELEZO

WANANCHI mkoani Lindi wanatarajiwa kuelimishwa njia bora na za kisasa za uvuvi, ufugaji na ukulima ili waweze kuboresha kipato chao na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima Tanzania(TASO) Engelbert Moyo wakati akiongea na waandishi wa habari.
Amesema kuwa wakati wa maonesho ya nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Lindi watajitahidi kuhakikisha wananchi wanajifunza teknolojia mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi ili waweze kuzalisha mazao yanayokidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

Moyo ameongeza kuwa watawaelimu wavuvi juu ya madhara ya uvuvi haramu na unavyohatarisha mazingira na viumbe wa majini.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa maonesho yatafunguliwa na Rais wa Serikali za Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Amesema kuwa Mawaziri mbalimbali watasaidia kutoa elimu kwa wakazi wa Mkoa huo kuhusu shughuli mbalimbali wanazozifanya katika kuwaletea maendeleo.

JK MGENI RASMI SIKU YA MASHUJAA

Picha na 1.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa zitakazofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Picha na 2
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar es salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema kuwa maadalizi ya sherehe hizo yamekamilika na kuongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu kihistoria yanalenga kuwaenzi wote waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa ardhi ya Tanzania, kuilinda na kudumisha amani na utulivu uliopo.

Amesema maadhimisho hayo yatapambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Gwaride la Kumbukumbu litakaloonyeshwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na uwekaji na silaha za asili, maua kwenye mnara wa kumbukumbu pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kutoa dua na sala kuliombea taifa.
Bw. Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika vi
wanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana, pia wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja huo. Aidha, katika hatua nyingine ameeleza kuwa wakati wa maadhimisho hayo barabara ya Lumumba, Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda kwa lengo la kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo

Sunday, 20 July 2014

CHADEMA:;'TUTARUDI KWA MARIDHIANO BUNGE MAALUM LA KATIBA NA USALAMA WA TAIFA NDIO UNATUMIKA KUBOMOA CHAMA CHETU''

kamati  kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema kilifanya mkutano ndani ya siku mbili kuanzia tarehe 18 julai hadi 20 julai ikijadili na kufanya maamuzi kuhusu masuala mbali mbali yanayoikabili nchi yetu na chama chao kwa ujumla

pamoja na hayo kamati kuu ilikuwa ikijadili ushiriki wa wajumbe wa CHADEMA kama sehemu ya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA katika bunge maalum na mustakabali wa mchakato wa katiba mpya

aidha  kamati kuu imepokea na kutafakari hali ya kisiasa ya nchi yetu kwa ujumla wake na hali ya kisiasa ndani ya chama chao ,uchaguzi unaoendelea katika ngazi mbali mbali  n ndani ya chama na masuala yote yanayohusu uchaguxi wa vijiji  na mitaa uliopangwa kufanyika  nchini baadae mwaka huu na kujadili taarifa ya fedha na mali za chama

MAAZIMIO JUU YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

CHADEMA kama sehemu ya UmojaWa Katiba Ya Wananchi UKAWA iendeleze mazungumzo na mheshimiwa Rais ambye ni msimamizi mkuu wa mchakato wa Katiba Mpya kwa upande serikali kuhusu namna ya kunasua mchakato huo ndani ya Bunge Maalum

Wajumbe wa Bunge Maalum wanaotokana na  CHADEMA kama sehemu ya UKAWA watarudi bengeni kwenye vikao vya bunge maalumendapo tu mamlaka ya benge hilo yatafafanuliwa kuwa ni ya kuboresha na sio kuibomoa au kuifuta misingi mikuu basic feature ya rasmu ya katiba mpya uiliyotokana na maoni ya ya wananchi na kuandaliwa na tume ya mabadilko ya katiba iliyoteuliwa na rais kwa ajili hiyo

wajumbe wa bunge maalum wanaotokana na CHADEMA kama sehemu ya UKAWA watarudu bungeni endapo tu na baada ya ufafanuzi uliotajwa katika aya ya 2 utahusisha marekebisho ya kifungu cha 25 cha sheria ya mabadiliko ya katiba, sura 83,inayohusu mamlaka ya bunge maalum,pamoja na kanuni husika za bunge maalum

wajumbe wote wa CHADEMA katika bunge maalum la katiba hawatashiriki katika kikao chochote cha bunge maalum au kamati zake hadi hapo ufafanuzi wa mamlaka ya bunge maalumuliotajwa katika aya za 2 au 3 utakapofanyika kwa mujibu wa maazimio ya kamati kuu

endapo bunge maalum litapitisha rasmu ya katiba mpya isiyotokana na maoni ya wananchini kama yalivyoakisiwa kwenye rasimu ya katiba mpya iliyoandaliwa na tume,CHADEMA kama sehemu ya UKAWA ,itafanya kampeni nchi nzima kuwashawishi wananchi kuikataa katiba hiyo katika kura ya maoni

kwa sababu yoyote ile,bunge maalum litavunjika kabila ya kupitisha Rasmu ya Katiba Mpya ,CHADEMA kama sehemu ya UKAWA itafanya mapambano ya kupata katiba mpya ya kidemokrasia kuwa sehemu kuu ya kampeni na operesheni zote za chama kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao na hata baada ya uchaguzi

MAAZIMIO KUHUSU HALI YA KISIASA NDANI YA CHAMA CHAO HAYA HAPA..................
Kamati kuu imekuwa ikipokea taarifa mbalimbali  za baadhi ya viongozi wa CHADEMA wa mikoa ya KIGOMA ,KATAVI,na TABORA hivyo kamati kuu ina taarifa za mipango ya ya viongozi wengi kuandaliwa kujiuzulu katika mikoa mingine kwa lengo la kutoa taswira potofu kwa umma kwa chama chao kinabomoka na kina migogoro mikubwa wa kiuongozi kufuatilia kufukuzwa kwa waliokuwa viongozi wa chama hicho na wajumbe wa kamati kuu ZITTO ZUBERI KABWE ,DkKITILLA MKUMBO,na SAMSON MWIGAMBA .Kamati kuu inafahamu kwamba mipango hiyo inaratibiwa na USALAMA WA TAIFA pamoja na CHAMA CHA MAPINDUZI CCM .

KUHUSU VIONGOZI WA MKOA WA KIGOMA WALIOJIUZULU Aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa mzee JAAFAR KASISIKO,mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi SHAABAN MAMBA,katibu wa mkoa MSAFIRI WAMALWA na katibu wa baraza la wanawake wa CHADEMA BAWACHA mkoa wa kigoma MALUNGA SIMBA wamekuwa kwenye uongozi wa chama katiks nafasi hizo kwa muda mrefu na katika kipindi hicho chote wameshindwa kukuza chama katika mkoa

Tangu mwaks 1993,chama kimekuwa na wabunge 1 tu wa kuchaguliwa kati ya wabunge tisa wa kuchaguliwa wa mkoa wa Kigoma.Kwa ulinganisho, chama cha NCCR-Mageuzi kimeongeza idadi ya wabunge wake wa kuchaguliwa kutoka sifuri mwaka 2005 hadi kufikia wanne mwaka 2019

Chama kimepunguza idadi ya madiwani wake katika Halmashauri ya wilaya ya Kigoma Vijijini kutoka madiwani watano mwaka 2005 hadi diwani mmoja mara baada ya uchaguzi mkuu 2010

Hii siyo mara ya kwanza kwa mkoa wa Kigoma kukabiliwa natatizo la vyama vya upinzani kusalitiwa na viongozi wao na kuchaguliwa kujiunga na CCM au kuwa mawakalawa chama hichoMifano ya nyuma ni pamoja na DK AMANI WALID KABOUROU aliyekuwa katibu mkuu na baadae kuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na mbunge wa jimbo la kigoma mjini KIFU GULLAMHUSSEIN KIFU na DANIELNSANZUGWANKO waliokuwa wabunge wa majimbo ya kasulu na kigoma kusini kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi.Wasaliti wote hao wa nyuma hawajawahi kuzima nguvu ya mageuzi katika mkoa wa kigoma na wasaliti wa sasa na wajao hawatazima nguvu hiyo


Kuhusu viongozi wa mkoa wa TABORA waliojuzulu katibu wa mkoa ATHMANI BALOZI mwenyekiti wa baraza la vijana wa CHADEMA BAVICHA wa mkoa HUSSEIN KUNDECHA na wengine katika uongozi wa wilaya kadhaa za mkoa huo hao pia wamekuwa katika uongozi wa chama kwa muda mrefu bila kuongeza tija yeyote kwa chama .Licha ya chama kutoa vifaa vya kazi kama vile magari kwa nkoa huo kwa muda mrefu


hata hivyo kamati kuu imewataka viongozi,wanachama ,wapenzi na mashabiki wa chama chao pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mapambano makali dhidi ya chama chao kamati kuu itachukua hatua zote stahiki kuhakikisha kwamba kama ambvyo wasaliti na makawala wa CCM WA MIAKA MINGI YA NYUMA HAWAKUATHIRI KUKUA NA KUJIIMARISHA KWA CHAMA CHAO,WASALITI NA MAWAKALA WA CCM wa sasa na wasaliti na mawakala watarajiwa hawataweza kuathiri kukua na kujiimarisha kwa chama hicho katika kipindi hiki ambacho chama kinajiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015

Friday, 18 July 2014

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA ANGELLAH KAIRUKI AKIFANYA MAJUMUISHO YA WIZARA YAKE ALIYOIFANYA WIKI HII

PIX 1 (1)Mkurugenzi mkuu wa kituo cha haki za binadamu  Hellen Kijo Bi. Simba(LHRC) (kulia) akimshukuru Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria baada ya kutembelea Taasisi zinazoshughulikia msaada wa kisheria jijini Dar es Salaam.
PIX5Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akiongea na wanahabari(hawapo pichani) kutoa maelezo ya majumisho ya ziara yake ya siku tano ya kuzitembelea Taasisi zinazotoa Huduma ya Msaada wa Kishria Mkoani Dar es Salaam.
Picha na Rose Masaka-MAELEZO.

MBOWE ;RAIS ACHANA NA ITIKADI ZA CHAMA CHAKO ILI TUPATE KATIBA MPYA KWA TAIFA

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE  AMETAKIWA KUACHANA NA ITIKADI ZA CHAMA CHAKE TAWALA CCM  KATIKA MCHAKATO HUU WA KATIBA ILI AWEZE KUINUSURU TAIFA  NA WANANCHI AMBAO HAWAPATI HAKI KATIKA KATIBA YA ZAMANI


MCHAKATO HUO AMBAO ULIINGIWA NA DOSRI WAKATI WA  MAJADILIANO YALIYOKUWA YANAFANYIKA NA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA BAADA YA KUTOKUELEWANA KATIKA RASIMU ILIYOKUWA MEZANI KWA MAJADILIANO NA KUUPELEKEA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI UKAWA KUAMUA KUTOKA NJE YA BUNGE HILO

RAI HIYO IMETOLEWA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA MH FREEMAN MBOWE WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KIKAO CHA NDANI CHA KAMATI KUU YA CHAMA HICHO KILICHOFANYIKA MBEZI GARDEN LEO HII

KIKAO HICHO KITAFANYIKA NDANI YA SIKU MBILI CHENYE AJENDA ZA MAJADILIANO YA TATHMINI YA MUENDELEZO HALI YA KISIASA HAPA NCHIN,JINSI YA KUUKOMBOA MCHAKATO WA KATIBA KWA SASA TAARIFA ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA NA BUNGE LABAJETI,MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA,UTENDAJI WA CHAMA NA TAARIFA MBALIMBALI  NA MAADHIMIO YAKE

HATA HIVYO ALIWEKA WAZI MSIMAMO WA UKAWA KUWA HAWATAKUWA TAYARI KURUDI KATIKA BUNGE LA KATIBA KWA KUSHINUIKIZWA NA WATU BINAFSI AU TAASISI  BINAFSI BALI WAKO TAYARI KURUDI KWA MARIDHIANO YA MAONGEZI NA MAKUBALIANO YA UFUATLIAJI WA AGENDA NA KANUNI ZA BUNGE MAALUMU LA KATIBA NA KUJADILI VILIVYOMO KATIKA RASIMU N ASIYO VINAVYOTOLEWA NA UONGOZI WA CCM

\RAIS WETU KASHINDWA KUINGILIA KATI TATIZO HILI LA BUBNGE MAALUM LA KATIBA NA AMEWAACHIWA WATU NA TAASISI BINAFSI KUTOA MATAMKO JUU YA BUNGE HILO SISI TUTARUDI KWA MAKUBALIANO NA MARIDHIANO YA UFUATILIAJI WA KANUNI ZA BUNGE HILO ALISEMA KIONGOZI HUYO

HALIKADHALIKA KIONGOZI HUYO ALIBAINISHA KUTOKUWA TAYARI KWA CHAMA CHAKE KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI MWAKA 2015 KWA KUTUMIA KATIBA ILE YA ZAMANI KWANI IMEKUWA NA MAKOSA MENGI SANA NA HAIWEZI KUTUMIKA KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO

;KWA KWELI KWA UPANDE WA CHAMA CHANGU SITAKUWA TAYARI KUONA MCHAKATO HUU WA KATIBA UNAPOTEZWA NA RAISI WETU NA KUSHINDWA KUPATIKANA KATIBA MPYA ITAKAYO TUMIKA KWA WANANCHI HATA HIVYO SITAIPA NAFASI CHAMA CHANGU KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI KWA KUTUMIA KATIBA YA ZAMANI\ALISEMA KIONGOZI HUYO

VIVYO HIYO AMEMTAKA RAIS WA AWAMU HII KUACHANA NA MAMBO YA KIUNAFIKI KWA KUWADANGANYA WANANCHI JUU UPATIKANAJI WA KATIBA KWA KUTUMIA CHAMA CHAKE HIVYO AITUMIE NAFASI HII KWA KUIMARISHA UPATIKANAJI HUO ILI AWEZE KUMALIZA UONGOZI WAKE KWA USALAMA ZAIDI


Thursday, 17 July 2014

JESHI LA POLISI KIKOSI CHA BARABARANI CHAPUNGUZA AJALI KWAASILIMIA KUBWANCHINI

TAKWIMU ZINAONYESHA KUWA JUHUDI ZA KIKOSI CHA POLISI BARABARANI KIMEENDELEA KUPUNGUZAAJALI NA MAJERUHI INGWA KUNA ANGEZEKO LA WATU WALIOFARIKI KATIKA AJALI JUNUARY HADI JUNE 2014

TAKWIMU  ZINAONYESHA KWAMBAIDADI YA AJALI  2013 JANUARY HADI JUNE NI 11,311 AMBAPO  JANUARY HADI JUNE 2014 NI 8405  NI SAWA NA  26% VIFO VILIVYOTOKEA JANUARY HADI JUNI 2013 NI 1739 NA JANUARY HADI JUNE 2014 NI 1743 SAWA NA 0.2%NA MAJERUHI KWA JANUARY HADI JUNE 2013 NI 9889 NA JANUARY HADI JUNE 2014 NI 7523 SAWA NA 24% HIVYO KUONEKANA KWA ASILIMIA KUBWA KUPUNGUA KWA AJALI HIZO

HALIKADHALIKA KAMANDAWA POLISI KIKOSI CHA BARABARANI MOHAMED MPINGA ALIZITAJA MIKOA INAYOONGOZA KWAAJALI ZA BARABARANI KWA MIEZI SITA HII NI PAMOJA NA KINONDONI 25.5% ILALA 18.6% TEMEKE 16.1% MOROGORO 6.1% NA KILIMANJARO 4% AMBAPO KWA DAR ES SAALAM PEKEE NI ASILIMIA 60.2 ZA AJALI ZILIZOTOKEA

KUTOKANA NA KUONGEZA KWA AJALI HIZO KUNA BAADJI YA MIKOA AJALI HIZO HUPUNGUATOKEA 2013 HADI 2014 NI KINONDONI 30% PWANI 59% ARUSHA 71% KILIMANJARO  52% NA MOROGORO  19% KWA MWAKA HUU

 VIVYO HIVYO TAKWIMU HIZO ZILIONESHAMAKUNDI YANALIYOATHIRIKA NA AJALI ZA BARABARA KWA MIEZI SITA NI 1.743 VIFO.MAJERUHI 7523 NA IDADI YA PIKIPIKI ZILIZOHUSIKA NI KWA ASILIMIA 15% PIKIPIKI ZA AJALI 20%PIKIPIKIZILIZOUA NI 7%NAPIKIPIKI ZILIZOJERUHI NI 22%

VILEVILE KAMANDA HUYOAMEWATAKA WANANCHI NA WADAU KWA UJUMLA KUTOA USHIRIKIANO KWA KUFUTA SHERIA KANUNI NA MAELEKEZO KWAAJILI YA USALAMA WAO WATUMIAPO BARABARA


Tuesday, 15 July 2014

TAZAMA PICHA ZA TUKIO LA UBUNGO

 HUYU NI MMOJAWAPO WA KADA ALIYESHIKA BANGO KATIKA MKUTANO HUO JINA LAKE HALIKUWEZA KUPATIKANA
NA DIWAMI WA KATA MAVURUZA BWANA PASCAL MACHONA AKITULIZWA NA MBUNGE WA KINONDONI IDD AZADI  BAADA YA KUTOKEA FUJAO KWA KAULI ALIYOITOA NAIBU WAZIRI KWA WAFUASI WA CHADEMA KUKAMATWE NA POLISI WAKATI WAKIIMBA UWANJANI HAPO.
JOHN MNYIKA AKIWA AMEBEBWA NA WAFUASI WA CHAMA NA WANANCHI WA JIMBO LAKE

WAAMUZK WA MECHI YA SERENGETI BOYS WAFIKA

serengeti boys 
Waamuzi wa mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Afrika Kusini (Amajimbos) wanawasili leo (Julai 15 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

 Mechi hiyo itafanyika Ijumaa (Julai 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam na itachezeshwa na waamuzi hao kutoka Shelisheli. Kiingilio cha mechi hiyo ni sh. 2,000 tu.

 Waamuzi hao ambao wanawasili saa 2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ni Allister Barra, Gerard Pool, Jean Joseph Felix Ernest na Nelson Emile Fred.
 Kamishna wa mechi hiyo Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar pia anawasili leo saa 2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
 BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

SOMA HAPA .........................HALI HALISI LA JIMBO LA UBUNGO HII HAPA KWA SIKU YA LEO

NI WAKATI WA ZIARA YA UKAGUZI WA MAJI NA MIRADI ENDELEVU YA MAJI KATIKA JIMBO LA UBUNGO LIMEZUA HALI YA TAFRANI KWA MBUNGE WA JIMBO HILO MHESHIMIWA JOHN MNYIKA NA MGENI RASMI MHESHIMIWA AMOSI MAKALLA AMBAYE NI NAIBU WAZIRI WA MAJI BAADA YA WANANCHI AMBAO NI MAKADA WA VYAMA VIWILI CHA CCM NA CHADEMA KUTOKUWA NA UELEWA WA ZIARA HIYO NA KUIFANYA KUWA YA KISIASA

TAFRANI HIYO IMETOKEA WAKATI MBUNGE WAO MNYIKA KUNYANYUKA NA KUANZA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KATIKA KIWANJA CHA SHULE YA MSINGI MIZURUZA ILIYOKO KIMARA JUU YA UFUATILIAJI WA MIRADI YA MAJI KATIKA JIMBO HILO

MAKADA HAO WALIONEKANA KUWA NA MABANGO YENYE KAULI TOFAUTI TOFAUTI ZA MAJUNGU KUTOKA PANDE ZOTE MBILI ZA VYAMA HIVYO NA PANDE HIZO KUFANYA UPINZANI KWA VIONGOZI PINZANI NA TAWALA KUTOTAMKA CHOCHOTE  ZAIDI YA KUTOA SULUHU YA TATIZO HILO KATIKA JIMBO HILO

AKIZUNGUMZA NA WANANCHI HAO MNYIKA WAKATI HALI YA KUTOKUELEWANA KWA PANDE MBILI ZIKIENDELEA ALIOWATAKA WANANCHI KUTOKUANGALIA ITIKADI ZA VYAMA VYAO KWANI ZIARA HIYO HAIKUHUSU SIASA BALI MAENDELEO YA KIJAMII

'TUMEKUJA KWA AJILI YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAJI KATIKA JIMBO HILI NA SIYO SHUGHULI ZA KISIASA HIVYO BASI MNATAKIWA KULITAMBUA KUWA TATIZO LA MAJI HALI ANGALI UCHAMA WALA CHEO ULICHONACHO "

JIMBO HILO AMBALO  NI MIONGONI YA MAJIMBO YANAYOKABILIWA NA MATATIZO YA MAJI KWA MUDA MREFU KWA SASA AMBAPO LINATUMAINI BAADA YA MUDA MFUPI LIATAWEZA KUPATA MAJI NA KUWA MAMA WA MAJI BAADA YA MIRADI ENDELEVU YA MAJI YA RUVU JUU NA RUVU CHINI  KUJENGWA KATIKAJIMBO HILO NA UJENZI WA TENKI LA MAJI AMALO LINABEBA TAKRIBANI YA LITA MILIONI KUMI NA KUUHIFADHI DAADA YA KUTOKEA RUVU AMBAPO MPAKA SASA TSHILINGI BILIONI 97 ZIMEKWISHA KUFIKISHWA NA SERIKALI KATIKA MRADI HUO

Wednesday, 9 July 2014

SOMALIA: AL SHABAAB WAVAMIA IKULU

Wanajeshi wa kundi la Al shabaab.
Wanajeshi wa kundi la Al shabaab.

Shambulio katika mji wa Mogadishu.
Shambulio katika mji wa Mogadishu.

Vikosi vya serikali Somalia vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji mkuu Mogadishu baada ya hapo awali wapiganaji wa kiislamu kuishambulia.

Maafisa wanasema washambuliaji wapatao watano kutoka kundi la al-Shabab – waliuawa walipoingia katika eneo la ikulu hiyo.

Washambuliaji hao wanadaiwa kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu la Ikulu hiyo.

Waziri wa habari na mawasiliano wa Somalia Mustaf Dhuhulow amesema kuwa tayari mmoja wa washambuliaji hao amekamatwa na anahojiwa na polisi.


Waziri Mustaf amesema, ” Walishambulia ikulu ya rais saa za jioni. Alikuwa watu washambuliaji watatu pamoja na dereva wao. 

Washambuliaji hao waliuawa lakini dereva wao alipata majeraha madogo na anazuiliwa na polisi na kuhojiwa. Walijaribu kuvamia Villa Somalia lakini wakakomeshwa. Tutawapa maelezo zaidi baadaye. Na tutaweza kutoa maelezo zaidi kwa raia wa Somalia na dunia nzima.”

Hii ni mara ya pili kwa Al Shabaab kuvamia ikulu ya rais mjini Mogadishu mwaka huu japo mara ya kwanza walifanikiwa kuingia ndani. Rais Hassan Sheikh Mohamoud hakuwepo wakati wa shambulio hilo.


NI KERO JIJINI DAR ES SAAALAM

Baadhi ya Wananchi wakitembea kwa miguu kufuatia foleni kubwa siku ya leo.
Baadhi ya Wananchi wakitembea kwa miguu kufuatia foleni kubwa 
Msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Foleni katika jiji la Dares salaam.
Foleni katika jiji la Dares salaam.
 Ni kila Siku kuanzia asubuhi hadi jioni mji wa Dares salaam umekumbwa na foleni kubwa kitu kinasababisha wananchi kushindwa kufanikisha shughuli zao kwa muda muafaka.
Barabara mbalimbali za jiji la Dares salaam muda mwingi  hazipitiki. Kwa wale wanaokwenda katikati ya mji katika maeneo kama Posta nako foleni ni kubwa sana. Chanzo cha foleni ni kufungwa barabara ya Moroko. Baadhi ya wananchi hulazimika kushuka kwenye dala dala na kuamua kutembea kwa miguu.

BAADA YA KUFUNGWA 7-1 NA UJERUMANI UNAJUA ALICHOKISEMA?SAMO HAPA..................................


Luiz-Felipe-ScolariWWW.YALIYOMO YAMO BLOGSPOT 

Luiz Felipe Scolari, kocha wa Brazil
Nani anawajibika kwa matokeo haya? Ni mimi, ni mimi. Lawama za matokeo haya mabaya zinaweza kutuhusisha wote, lakini mtu aliyeamua timu ya kucheza na mbinu nilikuwa mimi.“Ni wakati mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kazi yangu ya ukocha na siku mbaya zaidi katika maisha yangu ya soka. Lakini maisha yanaendelea. Nani anawajibika kwa matokeo haya? Ni mimi, ni mimi. Lawama za matokeo haya mabaya zinaweza kutuhusisha wote, lakini mtu aliyeamua timu ya kucheza na mbinu nilikuwa mimi.

Saturday, 5 July 2014

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA CHAENDELEA KUKUA MKOANI MOROGORO




NI VIONGOZI WA KIJIJI CHA MWAYA WAKISIKILIZA KWA MAKINI KATIKA MKUTAANO HUO



MWENYEKITI TAWI LA MWAYA AKISOMA RISALA MBELE YA MGENI RASMI BWANA ALPHONCE MAWAZO




MGENI RASMI AKIKATA KAMBA KUASHIRIA UZINDUZI WA TAWI LA MWAYA



MWENYEKITI WA MKOA WA GEITA KAMANDA MAWAZO ALIPHONCE AKIPANDISHA PENDERA YA CHAMA BAADA YA UZINDUZI WA TAWI LA MWAYA WILAYA YA KILOMBERO








ALPHONCE AKIMSHKA MKONO MZEE ALIYEJITOLEA NYUMBA YAKE KUWA OFISI ZA  TAWI LA MWAYA





Wednesday, 2 July 2014

MWAKYEMBE AFUKUZA 11 UWANJA WA NDEGE LEO

Waziri wa uchukizi tanzania HARSON MWAKYEMBE akizungumza na wanahabari leo ofisin kwake jijini Dar es salaam
           Waziri wa uchukuzi nchini Tanzania mh  HARSON  MWAKYEMBE amewafuza kazi katika uwanja wa ndege muda huu watumishi takribani 11 kutoka katika wizara za kilimo,afya,pamoja na wizara ya mifugo na uvuvi,kwa kushindwa kufwata taratibu za kazi katika uwanja wa ndege wa JK NYERERE jijini Dar es salaam.
      
            Akizungumza na Wanahabari muda huu ofisini kwake waziri MWAKYEMBE Amesema kuwa watumishi  wamekiuka sheria za kazi kutokana na kuendekeza vitendo kama vya rushwa,ubaguzi uwanjani hapo jambo ambalo Amesema kuwa hawezi kufumbia macho vitendo kama hivyo viendelee katika uwanja huo
         
        “Tunahangaika sana kupambana na madawa ya kulevya katika uwanja wetu wa jk nyerere,sasa wanajitokeza watu ambao sio waaminifu wanatuharibia sifa ya uwanja wetu kwa sababu zao,kiukweli hatuwezi kuvumilia tabia hizo na kuanzia sasa saa sita mchana sitaki kuwaona pale na nimeagiza waondolewe na polisi warudishwe maofisini kwao”alisema MWAKYEMBE.
        
         Hatua hiyo imekuja baada ya kuwasilishwa kwa malalamiko kutoka nchi za uarabuni,india na china kufanyiwa upekuzi tofauti na wengine na kuchukuliwa vyakula vyao na bidhaa mbalimbali kinyume na sheria ambapo bidhaa hizo zimekuwa hazirudishwi kwa wenyewe.
Waziri MWAKYEMBE amewataja wahusika hao kuwa ni -
                                           
                                   Wizara ya kilimo
1-TEDDY MWASENGE
2-ESTER KILONZO
3-REHEMA MRUTU
4-MARY KADOKAYOSI
5-KISAMO SAMJI
6-ANNETH KILIANGA
                               
                                   Wizara ya afya
1-AGNESS SHIRIMA
2-HAMIS BORA
3-VALERI CHUWA
4-ELINGERA MGHASE
5-REMEDIUS KAKULU
                              
                          Wizara ya mifugo na uvuvi
1-ESHI SAMSON NDOSI
2-ANNE SETEBE

             Aidha waziri MWAKYEMBE ametoa onyo kali sana kwa wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa JK NYERERE watakaoingia kwa sasa kutojihusisha na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria ikiwemo rushwa kwani wizara yake haitawavumilia hata kidogo