Thursday, 30 October 2014

Unaujua Ugonjwa wa Masundosundo Sehemu za Siri(Genital Warts) soma hapa

  NI vinyama laini vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya siri. Vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo [urethra], vulva, shingo ya kizazi [cervix], au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake.

Huu ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana [sexually transmitted infection(STI)].
Ugonjwa wa masundosundo husababishwa na jamii ya virusi wanaoitwa Human papilloma virus (HPV). Kuna zaidi ya aina 70 tofauti za virusi wa HPV ingawa si wote wanaosababisha masundosundo kwenye maeneo ya siri [genital warts]. Baadhi ya aina nyingine za HPV husababisha masundosundo kwenye ngozi inayozunguka sehemu nyngine za mwili kama vile kwenye mikono au miguu.

Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa baadhi ya aina za virusi wa HPV pia husababisha saratani ya shingo ya kizazi [carcinoma of the cervix] kwa wanawake au saratani ya njia ya haja kubwa [anal cancer] kwa jinsia zote mbili. Aina hii ya virusi hujulikana pia kama high-risk HPV.
 
Pamoja na kwamba ugonjwa wa masundosundo kwenye maeneo ya siri umejitokeza kwa kasi kubwa hasa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI, watu wengi waliopatwa na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile. Kwa mfano, kwa wanawake, virusi wa HPV wana uwezo wa kusambaa mpaka maeneo ya ndani kabisa ya kuta za uke au shingo ya kizazi [cervix] bila kuonekana wala kuhisiwa kwa urahisi. 
 
Kama tulivyotangulia kueleza hapo awali, maambukizi ya HPV husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni. Mara baada ya kuambukizwa, huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa masundosundo kuwa dhahiri, ingawa baadhi ya wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yeyote ile. Aidha imeonekana pia kuwa si kila mtu anayejamiina na aliye na maambukizi ya HPV au mwenye masundosundo anaweza naye kupata ugonjwa huu.
Vihatarishi  
Watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupatwa na masundosundo kwenye maeneo ya siri
•    Wenye wapenzi wengi
•    Kufanya ngono isiyo salama/ ngono zembe
•    Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo
•    Watumiaji wakubwa wa sigara pamoja na pombe
•    Kupatwa na maambukizi ya virusi wa herpes na wakati huo huo kuwa na msongo mkali wa mawazo
•    wajawazito
•    kuwa na upungufu katika mfumo wa kinga mwilini kwa sababu ya magonjwa mbalimbali au kwa sababu ya matumizi ya dawa fulani fulani kwa watoto wadogo, ukiona mtoto amepata masundosundo basi ni vema kufanya uchunguzi ikiwa amewahi kubakwa au kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Dalili za masundosundo [genital warts]
Masundosundo [genital warts] huonekana kama vioteo laini vinavyojitokeza juu ya ngozi ingawa wakati mwingine vinaweza kuwa vidogo mno kiasi cha kutoweza kuonekana vizuri kwa macho ya kawaida.
 
Kwa wanaume, vioteo hivi hutokea zaidi kwenye uume, ngozi ya pumbu, eneo la mitoki, mapajani pamoja na maeneo ya kuzunguka nje ya njia ya haja kubwa au ndani yake; wakati kwa wanawake hutokea ndani ya uke au njia ya haja kubwa, nje ya uke au ngozi ya nje kuzunguka njia ya haja kubwa, au ndani ya uke kuzunguka eneo la shingo ya kizazi.
 
Kwa wale wanaopenda kufanya ngono ya mdomoni [oral sex], wanaweza kupatwa na masundosundo/genital warts kwenye maeneo ya kuzunguka mdomo, lips, kwenye ulimi na hata kwenye utando unaozunguka koo.
 
Dalili nyingine ni kama vile mgonjwa kujihisi kukosekana kwa hisia [kufa ganzi] maeneo yaliyozungukwa na masundosundo, kwa wanawake kuongezeka kwa utoko/ uchafu sehemu za siri, kuwashwa sana maeneo ya siri na wakati mwingine kutokwa na damu ukeni mara baada ya tendo la ngono. Hata hivyo dalili hizi hutokea mara chache sana.
 
Wanawake wengi vijana wanaojihusisha na vitendo vya ngono [sexually active] huambukizwa sana ugonjwa huu lakini wengi wao hupona bila hata kuhitaji matibabu, wakati wanaume wanaoambukizwa, wengi wao huwa hawaoneshi dalili zozote za ugonjwa ingawa wanaweza kuwaambukiza wenzi wao bila ya wao kujua.
Uchunguzi na vipimo
Kwa wanawake, uchunguzi wa ugonjwa wa masundosundo/genital warts hujumuisha uchunguzi wa maeneo ya nyonga [pelvic examination] ambapo daktari huchunguza eneo hilo kwa kutumia vifaa maalum vinavyomuwezesha kuona uwepo wa masundosundo na wapi vilipo. Wakati fulani, kunyunyizia dawa yenye tindikali ya acetic acidhusaidia kufanya masundosundo kuonekana kwa urahisi zaidi. Wakati mwingine daktari anaweza pia kufanya kipimo cha pap smearkwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi [kwa vile kama tulivyoona hapo awali, zipo aina fulani fulani za HPV ambazo husababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake].
 
 Kwa wanaume, uchunguzi wa maeneo ya siri ni muhimu sana ili kufahamu kama kuna masundosundo au la.
Matibabu
Ni vema genital warts zitibiwe hospitali na daktari; haishauriwi kutumia dawa za kununua kujitibu mwenyewe kwa vile kuna uwezekano mkubwa wa kuchanganya aina ya dawa zinazotumika maalum kutibu aina nyingine za warts kwa ajili ya kujitibu genital warts.
 
Matibabu ya genital warts hufanyika hospitali kwa mganga kuondoa vioteo juu ya ngozi iliyoathirika au kwa kutumia dawa utakazoandikiwa na daktari na kuelekezwa namna ya kuzitumia mwenyewe nyumbani kwa siku kadhaa mpaka majuma kadhaa. Dawa zinazotumika ni pamoja na Podophyllin na podofilox, Trichloroacetic acid (TCA) au Imiquimod 
 
Ukiachilia mbali matumizi ya dawa, masundosundo yanaweza pia kutibiwa kwa njia ya upasuaji mdogo kama vile kwa kuvikata, au kuvimaliza kwa kutumia njia ya baridi/barafu [cryosurgeryLaser therapy].
 
Matibabu ya masundosundo, kama yalivyo matibabu ya magonjwa mengine yanayosambaa kwa njia ya ngono, ni lazima yahusishe pia tiba kwa mwenza wa mgonjwa. Wakati mwingine hata kama utajihisi huna dalili za waziwazi, ni vema kumuona daktari ili uchunguzwe na kutibiwa kuepusha kusambaza ugonjwa kwa watu wengine au kuachia ugonjwa mpaka ukakuletea madhara zaidi. Aidha matibabu yanaweza kuhitaji kurudiwa rudiwa mara kadhaa mpaka masundosundo yatakapokuwa yametoweka kabisa. 
 
Kwa wanawake ambao wametibiwa genital warts na kupona au wale ambao wamewahi kuwa na wenza waliowahi kuugua ugonjwa huu, wanashauriwa sana kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa shingo za kizazi [pap smear ni vema kufanya pap smearwalau kila baada ya miezi 3 mpaka 6 tangu kupata matibabu ya awali ya genital warts. Na kwa wale watakaonekana kuwa na dalili za awali za saratani ya shingo ya kizazi, hawana budi kufanyiwa uchunguzi na tiba zaidi li kuepusha uwezekano wa kupata saratani kamili ya shingo ya kizazi.
 
Baadhi ya nchi zilizoendelea zina utaratibu wa kuwapatia chanjo ya kuwakinga wanawake vijana au wasichana wadogo wenye umri kati ya miaka 10 mpaka 25 dhidi ya maambukizi ya HPV. Chanjo hii hutolewa hata kwa wale ambao wamewahi kuugua genital warts ingawa imeonekana kuwa ufanisi wa chanjo ya HPV dhidi ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kwa wale waliowahi kupatwa na genital wartszilivyosababishwa na high risk HPV huwa ni mdogo ukilinganisha na wale ambao hawajawahi kuugua lakini wapo katika hatari ya kupatwa na ugonjwa huo.
 
Hata hivyo, pamoja na kuwa umetibiwa, bado unaweza kuwaambukiza wengine virusi hawa wa HPV hivyo ni muhimu kuchukua hatua za kujikinga wakati wa kujamiiana.
Madhara ya masundosundo
Kama tulivyoeleza hapo awali, baadhi ya aina fulani za HPV wameonekana kusababisha saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya vulva. Kiujumla, HPV ndiyo kisababishi kikuu cha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wengi. Tofauti na wanawake, ifahamike pia kuwa aina za HPV zinazoweza kusababisha genital warts kwa wanaume ni tofauti kabisa na zile zinazoweza kusababisha saratani ya uume [cancer of the penis] au saratani ya njia ya haja kubwa [anal cancer].
 
Kwa baadhi ya wagonjwa, masundosundo yanaweza kuwa mengi na makubwa sana kiasi cha kuhitaji matibabu ya muda mrefu na ghali zaidi pamoja na ufuatiliaji wa kina.
Kinga dhidi ya genital warts
Njia mojawapo ya uhakika kabisa ya kujiepusha na ugonjwa wa genital wartspamoja na magonjwa mengine ya ngono/zinaa ni kujiepusha na matendo ya ngono na zinaa kabisa. 
 
Lakini kwa wale ambao ni ngumu kufanya hivyo, wanaweza kupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa huu kwa kujihusisha kingono na mwenza mmoja tu ambaye una uhakika kuwa hajaambukizwa wala hayupo katika hatari ya kuambukizwa magonjwa haya.
 
Tofauti na magonjwa mengine ya zinaa, matumizi ya condom hayana uhakika wa asilimia mia moja katika kukukinga dhidi ya HPV kwa sababu virusi wa HPV au hata masundosundo yanaweza kuwa nje nje kwenye ngozi ambayo uwezekano wa kugusana ni mkubwa. Pamoja na hayo, bado condom inaweza sana kupunguza hatari ya kuambukizwa masundosundo ikiwa tu itatumika vema na inashauriwa kuitumia mara zote unapokutana kingono na mwenza usiye na uhakika naye. 
 
Tukumbuke kila wakati kuwa HPV inaweza bado kuambukizwa kwa mtu hata kama mwenza hana masundosundo yanavyoonekana au hana dalili zozote zile. 
Ikiwa kuna uwezekano, ni vema kwa wanawake wote wenye umri wa miaka kati ya 9 mpaka 26 kupata chanjo dhidi ya virusi wa HPV ili kuzuia uwezekano wa kuambukizwa virusi hao ambao hatimaye husababishasaratani ya shingo ya kizazi.

Muigizaji Mzee Manento amefariki dunia.

MSIBA : Muigizaji Mzee Manento amefariki dunia.
Habari zilizotufukia hivi punde zinasema kuwa muigizaji Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Bado tunafuatilia kwa karibu habari hizi nz chanzo ch kifo cha mzee wetu huyu.

Mzee Mnento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakin na marehemu Kanumba. Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k pumzika kwa Amani

Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina.

RAIS MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA SATA, MEYIWA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (SAFA) kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na kipa wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.

Ametuma salamu hizo kwa Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya na Rais wa SAFA, Danny Jordan na kuongeza kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya ghafla vya Rais Sata na kipa huyo wa Bafana Bafana vilivyotokea wiki hii.

Rais Malinzi amesema kuwa misiba hiyo si pigo kwa Zambia na Afrika Kusini pekee bali Afrika kwa ujumla kwa vile walikuwa na mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa mpira wa miguu.

Amewaomba Rais Jordan na Rais Bwalya kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sata, na familia ya Meyiwa, na kuzitaka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito kwao.

Rais Sata (77) alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya King Edward VII nchini Uingereza alipkuwa kwenye matibabu, wakati kipa Meyiwa aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili mjini Vosloorus.

TFF YATANGAZA 100000 KWA MBUNIFU WA JEZI YA TAIFA STARS


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.
*       
Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).

Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.

SDL KUANZA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 22
Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 zitakazocheza katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyoketi jijini Dar es Salaam jana (Oktoba 29 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange ilipitia maandalizi maandalizi ya ligi hiyo ikiwemo mwongozo wake (roadmap).

Kwa mujibu wa mwongozo huo, usajili wa wachezaji utamalizika Oktoba 31 mwaka huu. Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Novemba 1 hadi 7 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajia kukutana Novemba 11 mwaka huu kwa ajili ya kupitisha usajili.

Pia Kamati ya Mashindano imepitisha viwanja vya timu zote, isipokuwa uwanja wa timu ya Mpanda United ya Katavi na ule wa Town Small Boys ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Uwanja wa Town Small Boys haukupitishwa kwa vile hauna uzio wa kudumu ( wa chuma) wa kutenganisha wachezaji na washabiki, na pia ufikaji wa timu Tunduru ni mgumu kutokana na ubovu wa barabara ikizingatiwa kuwa ligi hiyo itachezwa hadi kipindi cha Masika.

Kwa upande wa uwanja wa Mpanda United, umekataliwa kwa vile hauna vigezo vya msingi vinavyotakiwa ikiwemo vyumba vya kubadilishia nguo, kutokuwa na nyasi na uzio wa kudumu kutenganisha wachezaji na washabiki.

Kutokana na uamuzi huo, Mpanda United sasa itatumia Uwanja wa Mandela uliopo Sumbawanga wakati Town Small Boys itachezea mechi zake kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
 
29 WAITWA KIKOSI CHA MABORESHO TAIFA STARS
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya pili ya maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars) inayojumuisha vijana wenye umri chini ya miaka miaka 23.
 
Katika awamu hii, Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ameteua majina ya wachezaji 29 ambao watakuwa wakiingia kambini mara moja kwa mwezi siku ya Jumapili baada ya kuwakilisha timu zao kwenye mechi za ligi.
 
Kikosi hicho cha maboresho kitakuwa kikifanya programu maalumu za mazoezi mpaka siku ya Jumatano na kucheza mechi za kirafiki na timu za ndani au nje ya nchi.
 
Lengo hasa la programu hiyo ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji ambao walipatikana katika awamu ya kwanza ya mpango wa maboresho mwanzoni mwa mwaka huu Tukuyu mkoani Mbeya, lakini wamekuwa hawatumiki. Pia kuwandaa vijana ili kujenga timu ya ushindani na imara ya Taifa ya muda mrefu.
 
TFF ina imani kubwa kuwa programu hii itakuwa na manufaa kwa soka ya Tanzania. Timu hiyo itaingia kambini kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka huu katika hoteli itakayotangazwa baadaye.
 
Wachezaji walioteuliwa ni Aishi manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Aboubakar Ally (Coastal Union), Miraji Adam (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) na Joram Mgeveke (Simba).
 
Edward Charles (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kassim Simbaulanga (African Lyon), Pato Ngonyani (Yanga), Adam Salamba (Kahama), Hassan Banda (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hashim Magoma (Stand United), Makarani Ally (Mtibwa Sugar), Said Juma (Yanga) na Said Hamis (Simba).
 
Aboubakary Ally Mohamed (Zanzibar), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Malombe (Geita Gold), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda SC), Kelvin Friday (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Alfred Masumbakenda (Kahama) na Simon Msuva (Yanga).
 
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


MBEYA CITY KUINGIA MKATABA WA KIBIASHARA NA TPB LEO

Mbeya City leo imeingia mkataba na benki tanzania posta bank kwa mkataba wa kibiashara

Akitoa taarifa hizi katika mtandao huu afisa habari na mawasiliano bwana dismas ten alisema mkataba huo ni wa kibiashara na siyo wadhamini

Mkataba huu ni wa kibiashara siyo udhamini kwa maana kwa kupitia ATM card watakazopewa washabiki wa mbeya city wataweza kuchangia timu yao kwa matumizi yao ya kibenki alisema bwana Dismas Ten

Halikadhalika mkataba huo utausaidia timu kuwajua washabiki na idadi ya washabiki nchi nzima kwa urahisi

Wednesday, 29 October 2014

CCM, YAPATA HATI CHAFU KUTOKA KWA CAG

1
   SIKU chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kukiri kupokea hati ya mashaka kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kumtaka aweke hadharani hesabu za vyama vingine, hatimaye imebainika kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nacho kimepata hati kama hiyo.
Hatua hiyo ilibainika jana wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo kwa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyokutana na Msajili wa Vyama vya Siasa na CAG.
Msaidizi wa ofisi ya CAG, Benja Majura alivitaja vyama vilivyopata hati zenye mashaka baada ya hesabu zake kuwa na mapungufu ya kiuhasibu kuwa ni CCM, CHADEMA, CUF, TLP na NCCR-Mageuzi.
Ukaguzi huo ulifanyika kwa mujibu wa sheria namba 5 ya mwaka 1992 ya vyama vya siasa, iliyofanyiwa marekebisho na sheria namba 7 ya mwaka 2009, unampa CAG mamlaka ya kukagua hesabu za vyama vya siasa.
Katika mwaka wa fedha 2012/13 Msajili wa Vyama vya siasa alitoa ruzuku ya sh.16.8 bilioni kwa vyama nane vya siasa ambavyo ni CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi, UDP, TLP, APPT-Maendeleo na DP.
Vyama hivyo ni kati ya 12 vilivyowasilisha hesabu zake kwa CAG, ambapo vipo pia ambavyo vimepata hati mbaya na chafu.
Majura alivitaja vyama vilivyopata hati chafu kwa kuwa hesabu zake hazikueleweka kuwa ni NRA, UMD, APPT-Maendeleo, NLD, ADC, SAU na Chaumma.
Alivitaja vyama ambavyo havijawasilisha hesabu zake na kufanyiwa ukaguzi kuwa ni pamoja na Tadea, UPDP, UDP, Demokrasia Makini, Chausta, DP, Jahazi Asilia, AFP na CCK.
Alisema kuwa ukaguzi huo umekumbana na changamato mbalimbali ikiwemo kukosa muongozo wa muundo wa kuandaa taarifa za kifedha kwa vyama hivyo, kutoa karatasi moja ya mahesabu, vyama kutokuwa na ofisi, ukosefu wa vitendea kazi.
Naye Jaji Francis Mutungi, alisema kuwa kati ya vyama hivyo vilivyokaguliwa UMD, NLD, APPT-Maendeleo, ADC, CCM na CUF vimewasilisha ukaguzi huo katika ofisi yake.
Alisema kuwa vyama vya NCCR-Mageuzi, CHADEMA na TLP havijawasilisha ukaguzi huo katika ofisi yake licha ya kukaguliwa.


Jaji Mutungi alivitaka vyama ambavyo havijawasilisha taarifa hizo katika ofisi yake kuhakikisha wanawasilisha taarifa hiyo kabla ya Oktoba 31 mwaka huu.

UFISADI WA KUTISHA BIMA YA AFYA-WAZIRI WA JK AHONGWA GARI KIFISADI ,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI


pichani ni Waziri wa Afya Dokta Seif Rashid
MFUKO wa Bima ya Afya (NHIF), umekumbwa na kashfa ya ufisadi ya kutumia zaidi ya sh. milioni 200 kununua gari jipya ambalo wamemkabidhi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
Pia Bodi ya mfuko huo ambayo hupata fedha kutokana na michango ya wanachama wake, imetumia zaidi ya sh. bilioni mbili katika kipindi kisichozidi miezi sita badala ya mwaka mzima kama ilivyotengewa kwenye bajeti ya mfuko huo kwa mwaka huu wa fedha.
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF, Khamis Mdee
pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa NHIF, Khamis Mdee,
Uchunguzi wa Chanzo chetu, umebaini kuwa gari hilo lilinunuliwa kwa ajili ya matumizi ya Mkurugenzi wa Mfuko huo.
Gari hilo aina ya Nissan toleo jipya kabisa, lenye namba za usajili SU 39931, lilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Rashid  Oktoba 11, mwaka huu, saa 9.15 na sasa limebadilishwa namba na kuwekwa kibao cha Waziri wa Afya (W AF).
Sababu inayotajwa na NHIF kukabidhi gari hilo kwa waziri huyo ni kwamba gari lake la awali alilopewa na serikali wakati anaingia wizarani, limeharibika na liko kwenye matengenezo.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya mfuko huo, vililiambia  Chanzo  kuwa uamuzi wa kulikabidhi gari hilo kwa waziri, ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa NHIF, Khamis Mdee ambaye aliwaagiza wafanyakazi wa idara ya rasilimali watu kutekeleza agizo hilo na hakutaka kuulizwa maswali.
Baadhi ya watumishi wa mfuko huo walienda mbali zaidi wakidai kuwa Mdee alitoa gari hilo kwa waziri kama moja ya ushawishi wa kutaka ateuliwe kuwa mkurugenzi mpya wa mfuko, kushika nafasi iliyoachwa wazi na Emmanuel Humba aliyemaliza muda wake.
“Kwa kawaida mawaziri hupewa magari na serikali na hata yakiharibika matengenezo yake yanagharimiwa na serikali, lakini sio kazi ya taasisi yoyote ya umma iliyo chini ya wizara husika kununua gari kwa ajili ya waziri.
“Hivi leo kaimu mkurugenzi wetu akikosea kitu chochote kile, waziri aliyepewa gari hilo atakuwa na uwezo wa kumwajibisha?”alihoji mmoja wa maafisa waandamizi wa mfuko huo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
Bodi yatafuna bil.2/-
Kuhusu kashfa ya matumizi ya sh. bilioni 2 katika kipindi kisichozidi miezi sita, uchunguzi umebaini kuwa feha hizo zilitengwa kwa ajili ya bajeti ya Bodi ya wakurugenzi kwa mwaka huu wa fedha.
“Jambo la ajabu ni kwamba, bodi hiyo imetumia fedha hizo ndani ya miezi mitatu tu na sasa inaishi kwa kukopa kutoka kwenye kasma zingine,” alisema mtoa taarifa wetu.
Habari zinasema kuwa bodi hiyo imekuwa ikitumia fedha nyingi kwa ajili ya kufanya ziara za mafunzo nje ya nchi na zimekuwa zikigharimua mamilioni ya fedha.
Mkuregenzi ajitetea
Kaimu mkurugenzi wa NHIF, Mdee alipoulizwa kuhusu madai hayo, alikiri taasisi yake kukabidhi gari hilo kwa waziri wa Afya, lakini alikana kwamba hatua hiyo haina nia ya kushawishi ateuliwe kuwa mkurugenzi mpya wa mfuko huo.
Akizungumza na Chanzo chetu, alisema huo ni utaratibu wa kawaida na hata utoaji wa gari hilo umezingatia matakwa ya sheria.
Alisema mfuko huo umeamua kukabidhi gari hilo kwa waziri huyo kwani gari lake la awali alilokuwa akilitumia limeharibika na litakapotengamaa gari hilo litarudishwa mikononi mwa NHIF.
“Tuhuma hizo na nyingine zote unazozisikia ni majungu ambayo sijui lengo lake. Huyo ni waziri wetu na taasisi hii ipo chini ya wizara yake. Kuna ubaya gani kumpa gari akalitumia kwa muda wakati anasubiri gari lake?” alihoji Mdee na kusisitiza kuwa hayo ni majungu.
Akijibu madai kwamba ametoa gari hilo kama ushawishi wa kutaka uteuzi wa ukurugenzi, Mdee alisema wenye mamlaka ya uteuzi huo wako juu na hakuna namna mtu anaweza kufanya ushawizi ili ateuliwe.
Baada ya Humba aliyeasisi kuanzishwa kwa mfuko huo, kumaliza muda wake, Bodi ya wakurugenzi ilimteua Mdee kukaimu nafasi ya hiyo.
Serikali ilitangaza nafasi hiyo kuwa wazi na kuwataka wenye sifa kuomba, lakini hadi sasa mchakato wa kumpata mkurugenzi mpya, bado unaendelea. Hata hivyo ni miezi sita sasa imepita tangu kukamilika kwa usaili wa kumtafuta mkurugenzi mkuu mwingine na Mdee anapewa nafasi kubwa.
Kauli ya Wizara
Akizungumza na Chanzo chetu, Msemaji wa Wizara ya Ujenzi ambayo pamoja na mambo mengine inahusika na suala la magari ya viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri, Segolema Francis alisema hawana taarifa na gari la Waziri wa Afya kuharibika na pia hawana taarifa kama Bima ya Afya kutoa gari kwa ajili ya kumsaidia waziri katika kipindi hiki.


“Kweli tunahusika na magari ya mawaziri na watendaji wengine wa serikali, lakini hatujui kama waziri unayemtaja hana gani na ameazimwa la NHIF. Naomba unipe muda nifuatilia suala hilo hadi leo tunalitolea majibu,” alisema.

RAIS MALINZI KUFUNGUA KOZI YA FUTURO III

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kesho (Oktoba 29 mwaka huu) anafungua kozi ya ukufunzi wa waamuzi ya FUTURO III ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Hafla ya ufunguzi wa kozi hiyo inayoshirikisha zaidi ya waamuzi 40 wakiwemo baadhi ya wale ambao bado wanachezesha mpira wa miguu kutoka nchi mbalimbali za Afrika itafanyika saa 4 asubuhi kwenye hoteli ya Holiday Inn, Dar es Salaam.

Kati ya hao, washiriki wanane wa kozi hiyo inayoanza kesho hadi Novemba 3 mwaka huu chini ya wakufunzi wa FIFA wakiongozwa na Carlos Henriques ni kutoka Tanzania.

Washiriki kutoka Tanzania ni Emmanuel Chaula, Joan Minja, Josephat Bulali, Paschal Chiganga, Ramadhan Ibada, Richard Kayenze, Samuel Mpenzu na Soud Abdi.

SALUM ABUBAKAR MCHEZAJI BORA OKTOBA
Kiungo wa timu ya Azam, Salum Abubakar amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Abubakar ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) aliwashinda wachezaji wengine 20, huku wanne kati ya hao wakichuana naye kwa karibu.

Wachezaji hao ni Joseph Mahundi wa Coastal Union, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Najim Magulu wa JKT Ruvu Stars.

Kwa kuibuka mchezaji bora, Abubakar atazawadiwa kikombe na fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Wednesday, 15 October 2014

NOVEMBA 15 UCHAGUZI MDOGO TPLB

Mkutano Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) utafanyika Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo moja ya ajenda ni uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi moja ya uongozi kwenye bodi hiyo.

Nafasi hiyo ya ujumbe kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB iliyokuwa ikishikiliwa na Kazimoto Muzo imebaki wazi baada ya klabu yake ya Pamba ya Mwanza kushuka daraja kutoka la Kwanza hadi la Pili.

Hivyo, wagombea wa nafasi hiyo ni kutoka kwenye klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Klabu hizo zina nafasi mbili kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB ambapo nyingine inashikiliwa na Omari Mwindadi wa klabu ya Mwadui ya Shinyanga.

SDL WAONGEZEWA MUDA WA USAJILI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili wa wachezaji kwa timu za Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa siku saba ambapo sasa utamalizika Oktoba 21 mwaka huu.

Awali usajili huo unaofanyika kwa njia ya mtandao (online) ulikuwa umalizike jana (Oktoba 14 mwaka huu), lakini ni klabu chache ndizo zilizoweza kusajili ndani ya muda uliopangwa.

Klabu ambazo hazijakamilisha shughuli hiyo ya usajili, zinatakuwa kukamilisha ndani ya siku hizo saba kwani TFF haitaongeza tena muda wa usajili. Vilevile klabu za SDL zinakumbushwa kuwasilisha majina ya viwanja vya nyumbani ambavyo timu zao zitatumia kwenye ligi hiyo.

TFF ilifanya mafunzo ya usajili kwa maofisa usajili wa klabu hizo Oktoba 6 na 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Timu za SDL zimegawanywa katika makundi manne ya timu sita zitakazocheza ligi kwa mtindo wa nyumbani na ugenini. Kundi A lina timu za Mpanda United ya Katavi, Ujenzi (Rukwa), Mvuvumwa FC (Kigoma), Mji Mkuu FC (Dodoma), Milambo (Tabora) na Singida United (Singida).

Kundi B ni Mbao FC (Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Eleven Stars (Kagera), JKT Rwamkoma (Mara), Pamba (Mwanza) na AFC (Arusha). Kundi C ni Navy, Mshikamano, Transit Camp na Abajalo za Dar es Salaam, Kiluvya United (Pwani) na Kariakoo (Lindi(.

Timu zinazounda kundi D ni Magereza (Iringa), Town Small Boys (Ruvuma), Njombe Mji (Njombe), Volcano FC (Morogoro), Wenda FC (Mbeya) na Mkamba Rangers (Morogoro).

MAREKEBISHO YA RATIBA FDL KUNDI A
Mechi nne za Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimefanyiwa marekebisho ili kutoa fursa ya matumizi ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Timu za African Lyon na Kimondo FC ambazo awali zilikuwa zicheze Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, sasa zitacheza Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Nayo mechi ya Polisi Dar es Salaam na Majimaji ya Songea iliyokuwa ichezwe Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, sasa itachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

Mechi ya Friends Rangers na Ashanti United iliyokuwa ichezwe Mabatini mkoani Pwani, Oktoba 26 mwaka huu, sasa itachezwa Uwanja wa Karume, Oktoba 28 mwaka huu.

Pia mechi ya Lipuli FC na JKT Mlale iliyokuwa ichezwe Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa, imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba 26 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

7000/. KUIONA SIMBA NA YANGA

Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000.

Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.

Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani Kilimanjaro.

Washabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi.

Magari maalumu tu yenye stika ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia Barabara ya Mandela. Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa. Barabara ya kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


Sunday, 12 October 2014

AJALI YA KUSIKITISHA YATOKEA HUKO BUNJU 'B', DAR ES SALAAM

Wasamaria wema wakifunuka mwili marehemu baada ya kutoka kwenye jeneza



Wasamalia wema wakimmsaidia mume wa marehemu ambaye yupo taabani.

Gari lilipata ajali likiwa limevamia nyumba lakini halikuweza kuleta madhara yeyote kwenye nyumba hiyo.

Ajali ya kusikitisha imetokea maeneo ya Bunju B karibu na darajani leo majira ya saa 5 asubuhi, ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya Defender lenye namba T289 CJX ambalo lilikuwa linasafirisha mwili wa marehemu kutoka Dar kwenda Bagamoyo kwa ajili ya maziko.

Chanzo cha ajali hiyo imesadikika  ni kwamba dereva wa gari ambalo lilikuwa limebeba maiti alikuwa anaovertake  gari nyingine, ambapo ghafla alilikutana na lori , baada ya kuona hivyo dereva ilimbidi achepuke barabara kuu na kuingia kwenye korongo na kufanya gari hilo kupinduka mara tatu na kuvamia nyumba.

Kwa msaada wa mashuhuda wa ajali hiyo na majirani wa eneo hilo wanatujulisha kwamba mpaka sasa hakuna mtu yeyote ambaye amepoteza maisha ila kuna baadhi ya majeruhi ambao wako taabani akiwemo mume wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kupatikana maramoja.



Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo

JUKATA;ZANZIBAR KURA FEKI ZILIZOPIGWA KATIKA RASMU YA KATIBA ZAENDELEA KUJITOKEZA


  Kwa kuamini amefanya kuwa  siri kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta kuchakachua Theluthi mbili upande wa Zanzibar ili kupitisha Rasimu iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba sasa Siri hiyo imeanza kufichukua.
 
          Baada ya Jukwaa la Katiba nchini JUKATA  limefichua  hujuma nyingine ya Thelithi nbili kwa upande wa Zanzazibar baada ya kubaini kuorodheshwa kwa Mjumbe wa Bunge hilo kutoka Tanzania bara ambaye jina lake limeorodheshwa kwa majina ya wapiga kura kwa upande wa Zanzibar.
 
          Mjumbe huyo ni Zakhia Meghji ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya   Chama cha Mapinduzi CCM ambapo amepiga kura  kwa wajumbe wa Upande wa Zanzibar wakati yeye anatambulika kwamba ni mjumbe wa Tanzania bara.
 
          Kufichuliwa kwa Siri hiyo na Jukwaa la katiba nchini  juu ya uchakachuaji wa theluthi mbili kwa upande zanzibar umekuja siku chache baada ya chama cha NCCR Mageuzi kubaini kuorodheshwa kwa mjumbe kutoka chama hicho kwa upande wa Zanzibar kupiga kura ya ndio wakati hakushiriki vikao vya bunge maalum la katiba.
 
            Akifichua hujuma hiyo leo Jijini Dar ES Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba nchini JUKATA Deus Kibamba wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kibamba akizungumza kwa hisia alisema  kwamba wamechunguza wameibani kuorodheshwa Zakhia Meghji ambaye ni Mjumbe kutoka Tanzania bara kupiga kura ya ndio kwa upande wa Zanzibar.
 
            “Jukwaa la katiba limebaini kuwapo kwa mjumbe mwingine feki kwa upande wa Zanzibar Zakhia Meghji ambaye  ameorodheshwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Bunge la Maalum la katiba namba 149  kwamba ni mjumbe wa Zanzibar na kapiga kura ya ndio wakati yeye anajulikana wazi ni mjumbe wa Tanzania bara wakati  mjumbe huyo kupitia Gazeti la Serikali la mwezi julai lilimtaja Zakhia Meghji kuwa ni mjumbe Tanzania bara inakuweje leo tena wakati wa kupiga kura  atambulike kwamba ni  mjumbe wa Zanzibar yote haya ni kufanya hujuma ili kupata theluthi mbili“Alisema Kibamba .
 
         Kibamba alizidi kusema kwa ishara hiyo ni wazi Theluthi mbili haikupatikana bali Samwel Sitta na wenzake walifanya uchakachuaji wa makusudi ili kupisha katiba yao na kusema hizo kura mbili zilizopitisha kura kwa upande wa Zanzanibar ni wazi ni uongo wa wazi kwani mapaka sasa kura mbili tayari zimebainika ni feki.
           Aliongeza kuwa kwa sasa Jukwaa la katiba baada ya kuona uchakachuaji huo wameipa kazi kampuni iliyobobea kufanya uchunguzi kwenye kura za ndio kwa upande wa Zanzibar ili kujua ukweli na wakibaini tena kama kuna uchakachuaji mwengine basi hawatasita kuchukua hatua kali.
 
             Aidha Kibamba alisema  JUKATA wamesikitishwa sana  na kitendo cha Bunge Maalum la Katiba kuyazika kwa kiasi kikubwa maoni ya wananchi kwa kitendo cha kuondoa Mamlaka na madaraka ya Wananchi,maadili na mikio ya uongozi na utashi kwa umma na kuzidi kuendelea Tanganyika kuvaa koti la Muungano.
 
            Ambapo alisema kwa sasa Jukwaa la katiba Linajipanga kusambaza Rasimu ya katiba iliyopendekezwa na bunge maalum nchi nzima ili wananchi waamue ukweli juu ya katiba.
 
        Vilevile JUKATA limewataka watanzania kusoma kwa umakini Katiba iliyopendekezwa na bunge iliwaweze kujua ukweli.  

TAARIFA YA KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA ILIYOKUTANA OKTOBA 11, 2014- DAR ES SALAAM

Kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kimefanyika leo kujadili matukio ya hivi karibuni, hasa mwenendo wa wadau wa Bodi ya Ligi. Shirikisho linatoa tamko kwa umma kama ifuatavyo:

1. Kamati ya Utendaaji imesikitishwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni mpya za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo inaomba radhi kwa wadau ambao wameguswa na kusumbuliwa na matukio hayo.

2.Kufuatia matukio hayo, Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, imefungua mashtaka kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Damas Ndumbaro ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba. Pia wadau wote waliohusika na upotoshaji huo wakiwemo wafanyakazi wa TFF na Bodi ya Ligi watashughulikiwa kulingana na nafasi zao.

3.Kutokana na madai ya klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu 2014/15, Kamati ya Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu siku ya Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana kuhusu changamoto za kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla.

4.Kamati ya Utendaji itaendelea kuboresha Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi (Governing Regulations) ili kuweka uwiano wa utendaji na kuepusha tofauti kati ya Bodi ya Ligi, vilabu na TFF. Aidha Kamati ya Utendaji itafanya kila linalowezekana kuboresha ligi kwa kuijengea uwezo Bodi ya Ligi kwa lengo la kuwa na ligi zinazoendeshwa kisasa (Professional Leagues).