Usajili wa dirisho dogo msimu wa 2014/2015 umefungwa jana (Desemba
15 mwaka huu) huku wachezaji 15 kutoka nje wakiombewa Hati ya Uhamisho wa
Kimataifa (ITC) kutoka nchi mbalimbali.
Wachezaji walioombewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim
Humoud kutoka Sofapaka ya Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC
(Uganda) kwenda Azam, Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda
Polisi Mara, Charles Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United
na Chinedu Michael Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.
Dan Serunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De
Oliveira Neves Roque kutoka Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso
FC (Brasil) kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda
Stand United na Juuko Murushid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda
Simba.
Kpah Sean Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack
Abel kutoka KCB (Kenya) kwenda Polisi Morogoro, Moussa Omar kutoka Flambeau
(Burundi) kwenda Stand United, Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi)
kwenda Stand United, Serge Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam
na Simon Serunkuma kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inatarajia kukutana
hivi karibuni kwa ajili ya kupitia usajili wa wachezaji wote walioombewa katika
dirisha dogo wakiwemo wale wa mkopo.
RAMBIRAMBI
MSIBA WA KOCHA MADEGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko
taarifa za kifo cha Kocha Mshindo Madega kilichotokea leo (Desemba 16 mwaka
huu) mjini Bukoba.
Mbali ya kuwahi kuwa mchezaji katika timu ya RTC Kagera, Kocha
Madega aliwahi kufundisha timu za Kagera Stars, Mwadui na kombaini ya Copa
Coca-Cola ya Mkoa wa Kagera.
Mchango wake katika mchezo wa mpira wa miguu tangu akiwa kocha na
baadaye kocha utakumbukwa daima.
Tunatoa salama za rambirambi kwa familia ya marehemu, Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu
Tanzania (TAFCA) Mkoa wa Kagera na klabu ya Bukoba Veterans na kuwataka kuwa na
subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo.
TFF itawakilishwa kwenye msiba huo na Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Kagera (KRFA).
MICHUANO
YA COPA COCA-COLA YAENDELEA KUTIMUA VUMBI
Michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15
ngazi ya Taifa inaendelea leo jioni (Desemba 16 mwaka huu) kwa mechi mbili
zitakazochezwa jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani.
Uwanja wa Nyumbu uliopo mkoani Pwani utazikutanisha timu za Mjini
Magharibi na Dodoma katika mechi ya kundi B, wakati kundi C kutakuwa na mechi
kati ya Arusha na Mwanza itakayochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers uliopo Kawe
jijini Dar es Salaam.
Wakati kesho (Desemba 17 mwaka huu) ikiwa ni mapumziko, michuano
hiyo itaingia hatua ya robo fainali keshokutwa (Desemba 18 mwaka huu) kwenye
viwanja hivyo hivyo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
|
People (91)
Show details
|
Tuesday, 16 December 2014
15 KUTOKA NJE WAOMBEWA USAJILI DIRISHA DOGO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment