Wednesday, 17 December 2014
RIP AISHA MADINDA
Aisha akiwa katika uhai wake
Aliyekuwa Mnenguaji na Muimbaji wa Bandi ya Twanga Pepeta Aisha Madinda amefariki dunia hivi punde Jijini Dar es salaam. Habari imethibitishwa na mmiliki wa bendi ya Twanga pepeta Asha Baraka. Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.
a
“ Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea”. Amesema Asha Baraka
Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment