Wednesday, 17 December 2014

Mshindi bora wa ubunifu wa program za simu apatikana


Ni kupitia shindano la AppStar linaloendeshwa na  kampun i ya mawasiliano ya Vodacom na Mshindi wa kwanza kwenda India kushiriki katika ngazi ya kimataifa

Roman Mbwasi ameibuka kidedea katika shindano la kutafuta vipaji vya ugunduzi wa program za simu la AppyStar lililoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Shindano hilom  Likiwa linawalenga  wanafunzi wa vyuo vikuu wanaosoma  masomo ya Sayansi ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano na watanzania wote.

Wazo la program lililomfanya kuibuka mshindi linahusu upashanaji taarifa za barabarani kupitia mtandao wa simu.

Hii ni mara ya pili kwa Roman Mbwasi kushiriki na kuwa mshindi katika shindano hili mara ya kwanza ikiwa mwaka 2012 ambapo pia aliibuka kuwa mshindi wa kwanza.Kwa ushindiwa mwaka huu

Mshindi huyo  atajinyakulia zawadi ya shilingi milioni 2 na atakwenda Bangalore nchini India kushiriki katika awamu ya pili ya shindano hili ngazi ya kimataifa litakalofanyika Januari 15,2014.


No comments:

Post a Comment