Na Karoli
Vinsent
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisuasua
kuwachukulia hatua viongozi waliotajwa na Bunge kuhusika Katika Wizi wa zaidi
ya Bilioni 320 kwenye Akaunti ya Tegeta Esrcow ,naye Mbunge wa Kigoma Kusini
David Kafulila Ameibuka upya na Ameivaa Ikulu
Baada ya kusema Ikulu ya Rais Jakaya
Kikwete inamedhamilia kuwalinda wezi waliohusika katika kuiba pesa hizo,baada ya
kumzuia Mkurugenzi wa ofisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa PCCB Dk Edward
Hosea kutoiwasilisha Taarifa ya uchunguzi juu ya sakata hilo la Esrcow kwa Umma kutokana na Ripoti ya PCCB kuwataja
vigogo wa Ikulu kuhusika katika kuchota pesa kwenye Benk ya Stabink.
Hayo yamebuliwa mda huu Jijini Dar es
Salaam na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila wakati wa Mkutano na Waandishi
wa Habari ambapo Kafulila huku
akizungumza kwa uchungu alisema Inasikitisha kuona jinsi Ikulu inavyotumia
ubabe wake kumzuia Dk Hosema kutoiweka wazi ripoti yake ya uchunguzi.
“Tunafahamu wazi serikali inataka kuwalinda
watu waliochota pesa,kutokana na kitendo chake kumzuia PCCB asiweka hadharani
ripoti kwa kisingizia uchunguzi ujakamilika,ujakamilika kivipi wakati
tunakumbuka wazi Mkurugenzi wa PCCB Dk Hosea wakati kongamano la SADC kuhusu Rushwa
uliofanyika mkoani mwanza mwezi Novemba”
“Alisema
ripoti yake ya uchunguzi kuhusu Akaunti ya Escrow umekamilika na tayari
wameshamkabidhi Waziri Mkuu ingawa waziri huyo mkuu alikana,na hii yote
inafanyika hivi ni kutokana na Ripoti ya PCCB kuwepo na majina ya Vigogo wa Ikulu ambao walichota
pesa kwenye Benki ya Stabink”alisema Kafulila
Kafulila aliongeza kuwa leo majina ya
watu waliochota pesa kwenye Benki ya Mkombozi tu wanatajwa ,huku wengine kwenye
Benki ya Stabink Benki wakiachwa kwakuwa ni vigogo wa Ikulu.
“Leo majina ambao kamati ya PAC
waliyopewa na PCCB ni ya Benki ya mkombozi huku majina ya Benki ya Stabink
ambao watu walichota pesa kwa maboksi,Sandalusi,magunia ambao wengi wao ni
vigogo wakubwa wa ikulu wakiachwa,na ndio maana Ikulu hii inakataza Ripoti ya
PCCB iwekwe wazi kwakuwa itaweza kuvuruga nchi kwasababu wahusika waliochota
pesa wengi ni watu wa Ikulu”aliongeza Kafulila.
Kuhusu Jeuri ya Mmiliki wa IPTL Bwana
Seith
Kafulila ambaye pia ni katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR
Mageuzi alisema Jeuri aliyekuwa nayo bwana Seith kwa kuzivimbia Mamlaka zote
ikiwemo Mamlaka ya ukusanyaji Kodi TRA inatokana na kigogo huyo kufahamu wizi
huo ameufanya na vigogo wa kubwa wan chi.
“Huyu bwana seith anakuwa jeuri sana kwakuwa
anauhakika pesa za Escrow amekula na wengi hata akifanya jambo anajua wazi
hakuna wakumchukulia hatua kwakuwa wako wengi, na hii inatokana kutokuwa na serikali makini
ndio maana inamuacha huyo taperi kufanya anavyotaka ila serikali ijue huyo mtu
avyojisifu hivi atakujakuleta machafuko nchini”alitabainisha Kafulila.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo wa
kigoma Kusini alisema kwa sasa chama chake cha NCCR kwa kushikiliana na Umoja wao
wa Vyama vya upinzani nchini waanza Rasmi kwenda kwa wananchi kuwaeleza kuhusu
suala nzima lilivyo la Escrow na Wamepanga kuanza na Mkoa wa Kigoma.
“Tuanza tena ziara Mkoani Kigoma
kuhamasisha Umma uelewe kuhusu Ufisadi huu,na tunatawajulisha Watanzania kuwa
CCM haina uhalali wa kuchaguliwa kwasababu imeshindwa kuisimia serikali yake
kwani Makam mwenyekiti Taifa na Katibu wa CCM wamesisitiza kuwa wahusika
wawajibike lakini wamegoma”alisema Kafulila
|
Friday, 5 December 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment