Wednesday, 17 December 2014

JK AFARIJI FAMILIA YA MWAIBALE,MWILI WASAFIRISHWA KWENDA MBEYA LEO KWA MAZISHI

 Mdogo wa Mwisho wa akina Mwaibale Ambwene  akitoa salam za Mwisho kwa Marehemu mama yake
 Dada Mkubwa wa akina Mwaibale Mary Anyitike ambaye ni Kamishna Mkuu Msaidizi  wa Skauti Shughuli za Vijana Taifa akitoa salam za Mwisho za kuuaga mwili wa Marehemu Mama yao
 Dotto Mwaibale Akiaga Mwili wa Marehemu mama yake
Kulwa na Dotto Mwaibale wakiuaga Mwili wa Marehemu mama yao
 Kulwa Mwaibale akiwa ameshikiriwa na ndugu zake Baada ya Kuaga Mwili wa Mama yake
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers Eric Shigongo akiwa anaaga Mwili wa Marehemu
 Muhidin Issa Michuzi Mmiliki wa Michuzi Blog akitoa Heshima za mwisho katika Mwili wa Marehemu
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers Akitoa Heshima za Mwisho katika Mwili wa Marehemu
Muhidin Issa Michuzi wa katikati na Abdalah Mrisho wa kwanza kulia wakimpa pole Dotto Mwaibale
 



 
Kulwa na Dotto Mwaibale wakiwa katika ya pamoja na Baadhi ya waandishi kutoka Jambo leo, Global Publishers, Habari Maelezo na vyombo vyengine vya Habari
 
 Kulia ni Kulwa na kushoto ni Dotto Mwaibale wakiwa na sura za Majonzi wakati wa Ibada fupi ya Kumuombea Mama yao Mpendwa kabla ya kuanza Safari ya kwenda Mbeya
Baadhi ya Bloggers wakiwa katika Msiba wa Mama yao Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale kutoka kushoto ni Geoffrey Adroph  wa Pamoja Blog, Cathbert Kajuna wa Habari na Matukio Blog na Joachim Mushi wa The Habari blog
 
 
Baadhi ya  Waombolezaji wakiwa katika Majonzi
 
 
Waombolezaji wakiwa katika Shughuli ya Kuuaga mwili wa Mama yao Dotto,Kulwa na Nico Mwaibale 
******
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atuma salamu za Rambirambi katika Familia ya Mwaibale Kwa kuondokewa na Mama  Mzazi wao mpendwa Bi.Twitikege Mlagha Mafumu aliye fariki majira ya saa 5 usiku siku ya jumamosi wakati akikimbizwa hosipitali ya hindra kwaajiri ya Matibabu

Akiwasilisha salaamu hizo kwaniaba ya Rais Jakaya Kikwete Meneja Mkuu wa Globabal Publishers Limited Abdalah Mrisho Ameweza  kutoa pole  kwa wafiwa wote kwa ujumla wakiwakilishwa na Kulwa,Dotto na Nico Mwaibale Hivyo Kuwa na Moyo wa uvumilivu katika kipindi kigumu kilicho wafika familia ya Mwaibale

Vilevile Aliweza simama Kwa niaba ya Wanahabari Abdalah Mrisho aliweza kufikisha salaamu hizo Kwa kuwapa pole familia na wote walio guswa na msiba wakiwemo ndugu,jamaa na marafiki wa ndugu yetu mpendwa ambaye kwa sasa ni marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mafumu

Mwili wa ndugu yetu Mpendwa  umeagwa leo Mchana majira ya saa 6 katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke na kuanza safari  ya kuusafirisha kwa kwenda  kumpumzisha  mama mpendwa katika kijiji cha Kibumbe,Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya  ambapo Anatarajiwa kuzikwa  kesho Tar 17 alasil mwezi wa kumi na mbili (12) Mwaka huu

Tunapenda kutoa pole kwa wafiwa wote na Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema peponi Amen

No comments:

Post a Comment