Tamasha
kubwa la muziki linalofanyika kila mwaka la Sauti za Busara, maarufu pia kama tamasha kirafiki duniani mara zote limekua
likitoa kipaumbele katika upatikanaji wake kwa wenyeji. Tamasha lijalo
litavikutanisha vikundi 19 kutoka Tanzania kutumbuiza kuanzia tarehe 12 hadi 15
Februari 2015. Kiingilio ni bure kwa
waenyeji kabla ya saa 11 jioni na
baada ya hapo ni shilingi 3,000/= tu kwa
watanzania wote ili waweze kuhudhuria Tamasha! Zaidi ya hapo, watoto
wanaruhusiwa kuingia bila kutozwa chochote hivyo basi wenyeji wanachotakiwa ni kujitokeza nakusherekea
muziki wa Afrika huku wakipeperusha bendera ya Bongo, pamoja na wageni.
Kwa
kupitia mchango wa Sauti za Busara, Tanzania inaendelea kujidhatiti katika
ramani ya dunia katika suala zima la utalii wa kiutamaduni. Mkurugenzi wa
tamasha, Yusuf Mamoud anasema “Sauti za
Busara inawaleta watu pamoja, hutoa ajira, inasaidia kuimarisha tamaduni za
asili, inaendeleza wasanii pamoja na kukutana na kujifunza kutoka kwa wenzao,
lakini pia inatangaza utalii wa kiutamaduni wa Tanzania. Mbali na hapo, Sauti
za Busara inafanya kazi kubwa katika nchi: kukuza amani na umoja kwa kuheshimu
utofauti na mchanganyiko wa tamaduni mbali mbali”.
Wakiwemo
pamoja na wasanii wakubwa wa kimataifa kama Blitz the Ambassador kutoka Ghana, Tcheka (Cape Verde), Isabel
Novella (Mozambique), Aline Frazao
(Angola), Octopizzo na Sarabi kutoka Kenya na Ihhashi Elimhlophe wa Afrika kusini,
wasanii watakaowakilisha Tanzania katika Sauti za Busara 2015 ni: Alikiba, Msafiri Zawose, Leo Mkanyia, Culture Musical Club, Mgodro
Group, Mabantu Africa Ifa Band, Cocodo African Music, Rico Single, Mwahiyerani,
Zee Town Sojaz, Kiki KIdumbaki na
wengine wengi.
No comments:
Post a Comment