Pichani ni Waziri Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam |
SIKU chache kupita baada ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kumwandikia Barua Rais Jakaya Kikwete ya
Kujiuzulu na Rais kuridhia kujuzulu kwake na kumshukuru kwa kazi aliyofanya.
Naye Waziri Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa
Anna Tibaijuka amekuja Juu na kuwavaa wanaotaka yeye ajiuzulu na kusema hawezi
kufanya hivyo kutokana na kutohusika
katika wizi huo,
Pichani ni Waandishi wa Habari kutoka Vyombo Tofauti wakimasikiliza waziri Tibaijuka |
Na kusema pesa alizopewa zaidi ya Bilioni 1.6 na Mbia wa Kampuni ya
IPTL bwana James Rigimarila ilikuwa kwa ajili ya kusaidia kuboresha elimu ya
mwanamke na kumkomboa kutoka kwenye hali duni ya elimu.
Kauli hiyo ambayo imekuwa ni Tofauti na
Matarajio ya Wengi imetolewa Mda leo jijini Dar Es Salaam na Waziri huyo wa
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari
Pamoja na Mambo Mengine Waziri Tibaijuka akizungumza kwa
uchugu alisema hawezi kujiuzulu kutokana
na yeye kutohusika katika ufisadi huo.
“Mimi Nijiuzulu kwa sababu gani? yaani
kwa sababu ya mafanikio ya kuwakomboa wanawake kwenye Elimu ndio mimi
nijuzulu,maana kujiuzulu kunasababu, na hakuna sababu ya mimi kufanya hivyo na
sitofanya hivyo kwani wanaodai mimi nijiuzulu ni wanafiki wenye nia mbaya na
mimi ,na mimi sijiuzulu ng’o na nikifanya wanavyotaka Rais atashangaa ”alisema
Waziri Tibaiujuka.
Waziri
Tibaijuka aliongeza kuwa madai
anayodaiwa kupewa pesa zaidi ya Bilioni 1.6 na Mbia wa Kampuni ya IPTL
bwana james
Rugimalira ilikuwa kwa ajili ya kuinua elimu ya wanawake kwa kuikomboa
shule ya Barbro Johansoon ambapo waliochangia kwenye Shule hiyo ni
wengi kuliko bwana James Rugimalira.
“Leo
natuhumiwa na kila mtu kwamba nimepewa pesa na Rugimalira kwamba ni za
kifisadi,Jamani tuwe wa kweli kuhusu madai haya maana nimepewa pesa na
Rugimalira kwa ajiri ya shule hizi na sio huyo pekee alliyechangia kwani
waliochangia pesa hizi ni watu wengi ikiwema Rais wa Awamu ya Tatu,Benjamin
Mkapa,Mfanya Biashara Maarufu Reginald Mengi na wengine wengi,inakuwaje leo mchango
wa Rugumarila kwa Ajiri ya Elimu kwenye Shule hii ndio iwe nongwa”
“Kwasababu
ukisema ni pesa alizonipa ni za ufisadi wa Escrow sio kweli,kwani Bodi ya Shule
ilimuomba Bwana Rugimalira pesa kwa kutumia Kampuni yake ya Mabibo Wine na
kipindi kile ndio alikuwa kiongozi, sasa hawa watu wanaozani ni za ufisadi
inakuwaje jamani tuwe wakweli”Aliongeza Waziri Tibaijuka.
Waziri
Tibaijuka akiongea kwa uchungu huku kama akitaka kulia alivishangaa vyombo vya
Habari hususani Magazeti kumtuhumu kana kwamba ndio Mhusika wa Ufisadi wa
Escrow
“Taifa la
Ujerumani liliteketea kwa Uwongo uliokuwa ukienezwa,na Tanzania ndio tunaelekea
huko yaani Magazeti yananituhumu mimi kwamba mimi ni mhusika wa Escrow,hivi
haya Magazeti yana nini jamani hivi kweli huyo ni Mwandishi wa Habari kweli,na
gazeti linaandika Escrow ya Tibaijuka,hivi msaada wangu wa kuwakomboa Wanawake
kielimu ndio imekuwa haya jamani mbona hatuna hofu ya Mungu?”alihoji Waziri
Tibaijuka.
No comments:
Post a Comment