Tuesday, 19 August 2014

KISA CHA MAULID KITENGE KUIAMA RADIO ONE KISOME HAPA

Na Karoli Vinsent

SABABU za Mtangazaji Maarufu wa Kipindi cha Michezo na Burudani Maulidi Kitenge  kuipiga Chini Redio one  na Kuamia Redio mpya E.fm 93.7 ya hapa Dar Es Salaam, sasa sababu  zaanza kufichuka,Mtandao huu Umedokezwa Sababu hiyo

         Maulidi Kitenge ambaye ametanga rasmi mwanzoni mwa wiki hii kupitia mtandao wake  wakijamii wa facebook kwamba Miaka 14 aliyokaa redio na Kituo cha Tv cha Itv inatosha yeye kukaa mjengoni hapo na tena yeye kushindwa kuweka wazi sababu ya kuondoka hapo na kuondokea kwenye kituo kipya cha Redio cha E.fm 93.7 Dar Es Salaam,

              Taarifa za kuaminika Ambazo Mtandao huu umedokezwa kutoka kwenye Vyanzo mbalimbali vilivyopo hapo E.FM Redio pamoja na  Radio one zinasema sababu iliyomfanya aondoke hapo ndio sababu ambayo inahisiwa ndio  itakayowafanya Watangazaji wengi waondoke Redio one.

             Akielezea Sababu hiyo,Mfanyakazi wa kituo redio cha Efm, alichohaamia Kitenge ambaye hakutaka Jina lake litajwe Mtandaoni alisema  mtangazaji huyo amekosa uhuru ndio ikapelekea kutoelewana na mabosi zake.

          “Da ni kweli Kitenge sahivi ni mfanyakazi Mwenzetu na teyali kasaini Mkataba,ila sababu iliyomfanya aondoke pale Redio one,inatoka na y eye kuhusika katika kutengeneza Tangazo  linalohusu Ujio wa Timu ya Wazee wa Realmadrid ambao watakuja Tanzania wiki ijayo,sasa baada ya kutengeneza Tangazo lile Viongozi Radio one wakakasilika kwa yeye kutengeneza Tangazo linalohusu redio nyingine tena kwenye Studio tofauti na hapo”alisema mpashaji huyo 

                Chanzo hicho kilizidi kusema mara baada ya kitenge kutengeneza Tangazo hilo aliitwa kujitetea na Mabosi  wa Redio one,lakini yeye alionekana kama anakosa Uhuru kutokana na kuingiliwa hata sehemu zengine ambazo hazihususiani na kazi yake kutokana na kufanya kazi pale inapohitajika,ndipo akachukua maamuzi ya kuachana Redio hiyo.

          Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta Mkurugenzi wa Redio One Deogratus Rweyunga na kutaka kujua ukweli wa taarifa hizi,ambapo Rweyunga alimtaka Mwandishi wa Mtandao huu amtafute Kitenge mwenyewe na kuzidi kusema yeye hana ugomvi na kitenge.

            “Hebu sikiliza Mtafute Kitenge mwenyewe,maana yeye kwenda kwenye Redio hiyo ni changamoto zengine na tunamtakia maisha mema na sisi hatuna ugomvi na kitenge kaamua kuacha kazi hapa ni sawa yeye ameona ni sahihi,na harafu unaposema Tangazo hilo alilotengeneza ndio imetufanya tukasilike na tumfukuze kazi sio kweli kwani mbona yeye katengeneza matangazo mengi ikiwemoa Tamasha la matumaini atujakasilika na limepigwa Redio nyingi sana na hatujamfukuza iweje leo ”alisema Rweyunga

           Mwandishi wa Mtandao huu alipomtafuta kitenge kujua ukweli wa Taarifa hizo hakuweza kupatikana mara moja kutokana na kutopatikana kwenye simu,

        Sababu hiyo ya kitenge Kuondoa Redio one  iliwai kutolewa mara kwa mara kwa Watangazi waliohama hapo  wakisema wanakosa Uhuru wanapokuwa kwenye Redio hiyo.

MAKOCHA COPA COCA-COLA KUNOLEWA DAR

                       Makocha wa kombaini za mikoa zitakazoshiriki Copa Coca-Cola mwaka 2014 pamoja na waamuzi vijana wa michuano hiyo watashiriki kozi ya ukocha na uamuzi itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu.

Kozi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa itakayochezwa Septemba mwaka huu.

Makocha watakaoshiriki kozi hiyo na mikoa yao kwenye mabano ni Ahmed Simba (Mwanza), Ally Kagire (Kagera), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Anthony Mwamlima (Mbeya), Athuman Kairo (Morogoro), Bakari Ali (Kaskazini Pemba) na Charles Mayaya (Shinyanga).

Fidelis Kalinga (Iringa), Gabriel Gunda (Singida), Hafidh Muhidin Mcha (Kusini Pemba), Hamis Mabo (Kigoma), John William (Geita), Joseph Assey (Shinyanga), Joseph Haley (Manyara), Jumanne Ntambi (Kilimanjaro), Leonard Jima (Ruvuma), Madenge Omari (Mara), Mohamed Muya (Dodoma), Nicholas Kiondo (Ilala) na Nurdin Gogola (Temeke).

Osuri Kosuli (Simiyu), Peter Amas (Arusha), Ramadhan Abdulrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Renatus Mayunga (Kinondoni), Samwel Moja (Lindi), Seif Bakari (Katavi), Shaweji Nawanda (Mtwara), Sheha Khamis Rashid (Kaskazini Unguja), Tigana Lukinjo (Njombe), Yusuf Ramadhan Hamis (Kusini Unguja), Zahoro Mohamed (Tanga) na Zakaria Mgambwa (Rukwa).

Waamuzi vijana watakaoshiriki kozi hiyo chini ya Mkufunzi wa FIFA, Felix Tangawarima wa Zimbabwe ni 33. Kwa upande wa ukocha Mkufunzi ni Ulric Mathiott kutoka Shelisheli.

KOZI YA UKOCHA LESENI A KUFANYIKA SEPTEMBA 4

Kozi ya ukocha wa Leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika mara ya kwanza nchini, jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 4 mwaka huu.

Mkufunzi wa kozi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume atatoka CAF, na itamalizika Septemba 8 mwaka huu wakati ada ya ushiriki ni sh. 300,000.

Washiriki wa kozi hiyo ni wale wenye leseni B ya ukocha ya CAF. Fomu kwa ajili ya ushiriki wa kozi hiyo zinapatikana kwenye ofisi za TFF na tovuti ya TFF.

Boniface Wambura
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MTIBWA, POLISI MORO KUCHEZA MECHI YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI


Timu za Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zinazojiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitacheza Jumamosi (Agosti 23 mwaka huu) mechi ya majaribio ya mfumo wa tiketi za elektroniki.

Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa 10 jioni wakati kiingilio kitakuwa sh. 1,000.

Tiketi za mechi hiyo zitaanza kuuzwa kesho (Agosti 20 mwaka huu) kupitia mtandao wa M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka 30 ya Fahari Huduma yaliyopo katika wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, wengi wao wakiwa Morogoro Mjini.

Washabiki 100 wa kwanza kuingia uwanjani wapata jezi za timu za Mtibwa Sugar na Polisi.

Tayari mechi ya majaribio ya tiketi za elektroniki imeshafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo timu za Tanzania Prisons na Mbeya City zilipambana na kutoka sare.

Mechi nyingine za majaribio ya tiketi za elektroniki zitachezwa Agosti 30 mwaka huu. Uwanja wa Mkwakwani jijini utakuwa na mechi kati ya Coastal Union na Mgambo Shooting wakati katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ni Kagera Sugar dhidi ya mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars.

Septemba 6 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa kutakuwa na mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar. Mechi nyingine ni ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga itakayofanyika Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

WAAMUZI KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI

Waamuzi wanaotarajia kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu watafanya mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) mwezi ujao.

Mtihani huo utahusisha waamuzi wa daraja la kwanza (class one) wakiwemo pia wale wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mbali ya mtihani huo unaotarajiwa kufanyika kabla ya Septemba 10 mwaka huu, pia kutakuwa na semina kwa makamishna ambao watasimamia mechi za VPL na FDL.

Hivyo waamuzi wote wanatakiwa kutumia muda uliobaki kufanya maandalizi kwa ajili ya mtihani huo.

ACT YAJIZOLEA WANACHAMA KWA WAPINZANI WAKE

Na Karoli Vinsent

BAADA ya kuzoa wanachama wengi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Chama kipya cha Siasa nchini cha Alliance for change and Transparency ACT,sasa kimezidi kuzoa wanachama wengine ikiwemo viongozi kutoka vyama vingine vya upinzani .

           Hayo yamejidhililisha  wiki hii  Jijini Dar es Salaam wakati walipokuwa wakitambulishwa wanachama wapya waliohamia chama cha ACT-Tanzania Mbele ya Waandishi wa habari,Ambapo Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT-Tanzania Masega Muhamedi Masega alithibitisha kupokea wanachama wapya watatu ambao walikuwa viongozi waandamizi kutoka Chama cha Upinzani cha Sauti ya Umma SAU,

            Viongozi hao Waandamizi ni Fred Kisena,ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Mahusiano ya Jamii na sera Taifa ya chama cha SAU ,Majinus Mwembe  Mkurugenzi Mkuu wa Fedha pamoja na Zabroni Shilumbi ambaye alikuwa Naibu katibu mkuu wa Sera wa chama hicho.

            Wakizungumza wote kwa pamoja viongozi hao wa chama cha SAU ,waliohamia chama cha ACT-Tanzania  walisema wameamia kwenye chama hicho baada ya kupendezewa sera ya chama hicho na kusema kwa sasa wanaimani chama cha ACT-Tanzania ndio mkombozi Watanzania kutoka kwenye hali ngumu ya Maisha inayowakabili.

           Naye Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT-Tanzania Masega Muhamedi Masega aliwashukuru sana viongozi hao wa chama cha SAU kwa kuungana nao katika kutetea Watanzania na kusema chama hicho kitahakikisha kinashirikiana na wanachama hao kuhakikisha wanamkomboa mtanzania wa leo na kuwataka watanzania kujiunga na chama hicho kwani ndio kimbilio lao,

            Katika Hatua nyingine Chama hicho kipya cha Siasa cha ACT-Tanzania,kwaanzia kesho kitaanza Ziara kwenye mikoa 15 kwa lengo ya kueneza na kukijenga chama hicho hadi ngazi za chini.

          Akizungumzia Ziara hiyo Katibu Msaidizi wa Chama hicho Leopald Luca Mohona alisema wameandaa makundi matatu yatakayogawanywa mikoa 15 ambapo kundi la kwanza litaongozwa na Mwenyekiti wa Mda chama hicho Lukas Kadawa Limbu akisaidiwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Athumani Balozi.

Ambapo ziara hiyo itatumia siku 17 kufikia majimbo 22 kwenye mikoa mitano.

        Vilevile Kundi Jingine litaongozwa na Makamu mwenyekiti akisaidiwa na Naibu katibu mkuu Taifa pamoja na kundi jingine pia litakalo ongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Samsoni Mwigamba atakayeambatana na Katibu Uenezi wa chama hicho kwenye mikoa mengine,

FIFA KUBORESHA MAKAO MAKUU YA TFF


Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) limeahidi kuboresha makao makuu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yaliyoko kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Ilala ili yawe katika kiwango cha kisasa ikiwa ni
pamoja na kuwa na vitendea kazi na miundombinu ikiwa ni pamoja na upanuzi
wa ofisi.

Hatua hiyo itaiwezesha TFF kuwa na mazingira bora ya
kufanya shughuli zake kwa ufanisi.

Vilevile kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo ile ya Goal, FIFA imeahidi
kushirikiana na TFF katika kuendeleza mradi wa kiuchumi kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume.

Mwanzoni mwa mwaka huu, TFF ilihamishia makao yake makuu katikati ya
jiji ili kupisha maendeleo ya kuiwezesha Karume kuwa kituo cha kisasa kwa
michezo na vitega uchumi.

Akiongea mwishoni mwa ziara ya kikazi nchini, Meneja Miradi wa FIFA
anayeshughulikia Programu za Afrika, Zelkifli Ngoufonja amesema
FIFA inaunga mkono wazo la kuboresha makao makuu ya Karume na itasaidia
kwa awamu uboreshaji huo.

Katika kuhakikisha usimamizi na utekelezaji
barabara wa mradi huo, ujumbe huo wa FIFA ulikubaliana na Kamati ya
Utendaji ya TFF kuboresha ofisi za Karume ili jengo la utawala lianze
kutumika huku mradi ukitekelezwa kwa awamu.

Pamoja na kuongelea mradi huo muhimu kimichezo na kibiashara, ujumbe huo
uliokuwa nchini kwa juma moja kufuatia mwaliko wa TFF ulikuwa na nafasi ya
kujadiliana na TFF kuhusu maboresho katika masuala mbalimbali yakiwemo ya
Utawala, Fedha, Masoko, Ufundi, Mashindano na timu za taifa.

Akiongea kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya TFF, Rais wa TFF Jamal Malinzi
aliushukuru ujumbe huo wa FIFA kwa msaada mkubwa katika historia ya
mahusiano kati ya FIFA na TFF.

Ujio huo unafuatia maombi ya TFF kuwa sehemu ya mradi wa Performance wa
FIFA. Mradi wa Performance unaoshirikisha nchi
mashirikisho 163 kati ya wanachama 209 wa FIFA, unalenga kuongeza ufanisi
katika uendeshaji na uongozi wa nchi wanachama wa FIFA.

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Saturday, 16 August 2014

LISSU;JK UMESHINDWA KUITAMBUA SHERIA

Na Karoli Vinsent

SIKU moja kupita baada ya Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kusema haina Mamlaka ya kulivunja Bunge Maalum la Katiba kwa madai kwamba Hakuna kipengere cha Sheria kinachotoa mwanya kwa Rais kulivunja Bunge hilo.
            Pia Ikulu ikasema Bunge hilo litaendelea na hata kama Wajumbe wanaounda Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,kutokuwepo kwani umoja huo ni idadi ndogo sana ya wajumbe .
            Nao Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,umeibuka na kusema Ikulu hiyo inashindwa kudagavua sheria vizuri
            Kauli hiyo imetolewa leo na Mwanasheria wa Umoja wa kutetea katiba ya Wananchi UKAWA Tundu Lissu wakati alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu juu ya taarifa hiyo ya Ikulu.ambapo Lissu alisema ni kweli Rais Kikwete hana mamlaka ya kulivunja bunge hilo.
           Bali Rais amefanya mambo mengi kwenye mchakato huu wa katiba na hakuna kipengele chochote cha sheria kinachompa mamlaka ya kufanya mambo hayo.
             “Ni kweli mwandishi hakuna kipengele chochote cha sheria kinachompa mamlaka Rais kulivunja bunge hilo,ila nashangaa sana ikulu inaangalia sheria kwa juu juu tu,hivi mbona Rais amefanya mambo kwenye mchakato huu wa katiba pasipokupewa idhini ya sheria,”
            ”kwa mfano niambie ni wapi kuna kipengele cha sheria kinachompa mamlaka Rais kufungua Bunge Maalum la Katiba lakini mbona Rais alikwenda kulifungua bunge la katiba? Na ni sheria gani inayompa mamlaka Rais kuongeza mda vikao vya bunge la katiba mbona kaongeza mda sheria hizi zinatoka wapi”alihoji Lissu.
            Tundu Lissu ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba alizidi kusema kwamba kwenye sura za Katiba za nchi zinampa Mamlaka Rais kuteua na kufukuza mtumishi yeyote inakuwaje leo ikulu ije na kauli yenye ukakasi kama hiyo.
          Kuhusu kufunguliwa mirango wazi kwa Wajumbe wa UKAWA kwenda ikulu kuonana na Rais.
           Tundu Lissu alisema amezipata taarifa hizo ila kwa sasa anawasiliana na Wenzake ili kujua wanachukuliaje maamuzi hayo.
Kuhusu utata unaoibuka sasa kuhusu 2 ya 3 wajumbe kutoka Zanzibar.
            Tundu Lissu,ambaye pia ni Mbunge wa Singida mashariki CHADEMA alisema anashangaa jinsi ikulu inavyodanganya watanzania kwani ukweli huko pale pale hakuna uwezekano wa kupatikana 2 ya 3 ya wajumbe kutoka Zanzibar.
           “Ukisoma waraka wa chama cha Mapinduzi CCM,uliotolewa baada ya kumalizika kwa vikao vya kwanza vya Bunge maalum la Katiba wanasema wazi kwamba 2 ya 3 ya wajumbe wa Bunge maalum la katiba kutoka Zanzibar haipo sasa hao ikulu wanasemaje idadi hiyo ipo , mimi nawashangaa sana”alisema Lissu 

Thursday, 14 August 2014

TAHLISO WAPINGA MAANDAMANO YALIYOPANGWA KUFANYIKA LEO IJUMAA

DSC_4824 

Makamu Mwenyekiti wa TAHLISO Abdi Mahmoud Abdi akizungumza na Waandishi wa habari leo Mjini Idara ya Habari maelezo Zanzibar kuhusu kukanusha Taarifa ya Maandamano yaliyopangwa kufanyika hapo kesho. 

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 14/08/2014
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu TAHLISO limekanusha Taarifa zilizosambazwa katika Vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii juu ya kuwepo wa maandamano ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu yanayotarajiwa kufanyika hapo kesho Ijumaa.

Shirikisho hilo pia limesema Taarifa za kuwepo kwa maandamano hayo hazijatolewa na TAHLISO na kuwaomba Wanafunzi kutojaribu kushiriki katika Maandamano hayo.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mjini Zanzibar Makamu Mwenyekiti wa TAHLISO Abdi Mahmoud Abdi amesema aliyesambaza Taarifa za Maandamano hayo ni Mtu ambaye alishavuliwa Nyadhifa za Uongozi wa TAHLISO na kwamba anachokifanya ni Upotoshaji na kujipalilia kisiasa.

“Anayejiita Mwenyekiti wa TAHLISO Musa Mdede SI MWENYEKITI HALALI kwasababu vikao halali vya Shirikisho vilivyofanyika May 3,4,2014 katika Chuo cha kodi vilimwondoa madarakani na kwa mujibu wa Katiba nafasi yake ilikaimiwa na Makamu wake ” Alisema Abdi

Amesema sababu ya Msingi ya kumuondoa katika nafasi yake ilitokana na kwenda kinyume na Katiba kwa kujiingiza katika Siasa ambapo aligombea na kuangushwa katika kura za maoni kupitia CHADEMA.

Amedai kuwa anachokifanya Mdede kwa sasa ni upotoshaji kwa TAHLISO ambapo anajitangaza kwa malengo ya kugombea uchaguzi mkuu unaokuja wa mwaka 2015.

Amefahamisha kuwa licha ya kuwepo na Taarifa ya Baadhi ya Vyuo kutokupata Pesa kwa ajili ya Mafunzo ya Vitendo TAHLISO imekuwa bega kwa bega kuhakikisha suala hilo linapatiwa majibu ya haraka.

Amesema BODI ya Mikopo inaendelea kuchukua hatua za haraka katika kuhakikisha Vyuo husika Vinapatiwa fedha na kwamba siku ya Leo Bodi itatoa Fedha kwa Chuo kikuu Kishiriki  cha kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMUCCO)  na Chuo kikuu cha Jordan Morogoro.

“Chuoni siyo sehemu ya kufanya Siasa bali ni sehemu ya kusoma, Maandamano siyo suluhu njia pekee ni mazungumzo na tunaendelea kuyafanya” Alifafanua Abdi.

Aidha Makamu Abdi amesema taratibu zinazohitajika zinaendelea kuchukuliwa ili Vyuo vingine vilivyobakia viweze kupata fedha hizo.

Vyuo ambavyo havijapata Fedha za Mafunzo kwa Vitendo ni pamoja na Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Mwanza na Tabora, Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji Mbeya na Chuo kikuu cha Tumaini Makumira-Iringa.

Katika taarifa zilizosambaa kwenye Vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii inadaiwa kesho Ijumaa kutafanyika Maandamano ya amani ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu kuelekea Ofisi za Waziri Mkuu kushinikiza Serikali kutoa Shiligi Bilioni 6.6 kwa ajili ya mafunzo ya Vitendo kwa wanafunzi hao.

Makamu huyo ambaye anashika nafasi ya Uenyekiti kwa sasa amewaomba Wanafunzi ambao hawajapata fedha zao kuwa watulivu wakati wakisubiri kupata fedha zao huku hatua za haraka zikichukuliwa.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

WASOME WAANDISHI BORA HAPA

Na karoli Vinsent

KWA muda miezi mitatu sasa Mtandao huu umefanya utafiti katika sekta ya Habari hususani magazeti na kutaka kujua ni Waandishi gani wa Habari kwenye magazeti ambao  makala zao zinapendwa sana.

           Mtandao huu katika utafiti wake uliangazia magazeti zaidi ya 20 ambayo yamesajiliwa na msajili wa magazet nchini,utafiti huo ulijikita zaidi katika kuangalia hamasa za watanzania katika kutaka kuzisoma habari za waandishi hao.

            Katika utafiti huo walishirikishwa hadi wauza magazeti pamoja na wasomaji wa magazeti.

          Wafuatao ni ndio Waandishi watano Bora ambao Makala zao zinasomwa sana nchini Tanzania.
               1..Jenerali Ulimwengu
Huyu ndio miongoni mwa Waandishi wa Makala bora kabisa nchini Tanzania,ambaye anaandika makala ambapo wananchi hawataki hata wiki ipite bila kusoma makala zake.

             Ulimwengu ambaye  anaandikia makala zake kwenye Gazeti la Raia mwema na Raia Tanzania,katika magazeti hayo amekuwa akiandika makala mbalimbali ikiwemo za Kisiasa pamoja na kijamii,na kufanya Gazeti la Raia Mwema kuwa ni miongoni mwa gazeti linalopendwa zaidi,

             Gazeti la Raia Mwema ni Gazeti linalotoka maramoja kwa Wiki limekuwa likipendwa sana kutokana na mchango anaoufanya mwandishi huyo.

           Ulimwengu makala zilizompa heshima kubwa sana ni –Acha kelele toa hoja,pamoja Hapa kwetu tunakimbilia wapi ,na makala nyingine.

                  2..Saed Kubenea
Huyu naye ameshika nafasi ya pili ya Waandishi bora wa Makala nchini Tanzania,Kubenea jina lake sio geni sana kwenye masikio ya watanzania kutokana na kazi kubwa anayofanya hapa nchini kwenye sekta ya Habari.

              Kubenea anasifika kutokana na Ujasili aliokuwa nao,mwandishi huyo makala zake nyingi anaandikia kwenye gazeti La Mawio.
            Kabla ya kuandikia Mawio kubenea pia alikuwepo kwenye Gazeti la lilofungiwa kwa muda usiojulikana la Mwanahalisi.

                Katika gazeti la Mwanahalisi kubenea alikuwa ni mkurugenzi wa gazeti hilo,baada ya kufungiwa gazeti hilo,kubenea hakutaka kipaji chake kupotea cha kuhabalisha watanzania ndipo akajiunga kwenye Gazeti la Mawio.

              Uwepo  wake kwenye Gazeti hilo la Mawio ndipo amelifanya limekuwa gazeti linalopendwa zaidi sana nchini Tanzania,gazeti la Mawio linatoka kila alhamisi.
          Kwa Mujibu ya wauza magazeti wanasema katika magazeti yanayofanya Vizuri gazeti la Mawio lipo.
                 3---Edo Kumwembe.
                  Huyo naye ameshika nafasi ya Tatu kati ya Waandishi wa Habari ambao wanaandika makala zinazopendwa zaidi.
               Kumwembe,ambaye ni tofauti na Ulimwengu,kubenea kwani Kumwembe yeye anaandika makala za habari za Michezo kwenye gazeti la Mwanaspoti.
                Kabla ya kuandika mwanaspoti Kumwembe alikuwa anaandika makala kwenye Gazeti la michezo Dimba,ambapo alipokuwa huko kumwembe alisifika sana kwa kuandika makala nzuri zenye kuwafanya wasomaji wasikubali hata wiki kupita bila kusoma makala zake na hata alivyoamia Mwanaspoti huko ndipo alipozidi kupata umaharafu sana kwa makala zake zenye ubora.
              Kitu kinanchomtofautisha kumwembe na waandishi wengine wa makala za michezo kumwembe amekuwa mtu anayefanya utafiti kabla ya kuandika makala zake ikiwemo hata kwenda hata nchi za nje.
            4—Edson Kamukara
             Huyu naye ameshika nafasi ya Nne kati ya Waandishi wa Habari wanaoandika makala zinazowafanya wasomaji wazipende zaidi.
           Edsoni Kamukara ambaye anatoka kwenye Gazeti la kila siku la Tanzania Daima naye anasifika sana kwa kuandika makala zenye kupendwa zaidi amekuwa akiandika makala bila ya uoga wowote.
               Kamukara ambaye pia ni Mhariri wa Gazeti hilo ,amekuwa akiandika makala zenye kutoa elimu pamoja na kuwakosoa vongozi walioko Makadarani  ambao wanakwenda kinyume.
          Umakini wa Kamukara umelifanya Gazeti la Tanzania Daima kuwa ni miongoni mwa magazeti linalopendwa zaidi.
                     5---Jabir Idrissa
                 Huyo naye ameshika nafasi ya Tano kati ya Waandishi wanaongoza kwa undikaji wa Makala zinazowafanya wasomaji walipende Gazeti kulisoma kila siku.
           Jabir ambaye anatoka kwenye gazeti la Mawio naye amekuwa ni miongoni mwa Waandishi wanaongoza kwa uandishi makini wa Habari pamoja na Makala zenye kuifanya Jamii ilipende kusoma gazeti hilo.

UKAWA RUDI BUNGENI JAMANI

indexNa Rose Masaka-MAELEZO
UKAWA waombwa kukubali maoni ya watanzania walio wengi ya kuheshimu pesa za walipa kodi kwa kurudi bungeni na kupingana kwa hoja kwani hoja zao zikiwa za huakika hazitapingwa bali kanuni na taratibu zinazoendesha bunge zitafuatwa badala ya kuendelea kulalamika katika majukwaa ya kisiasa.

Kauli hiyo imetolewa na balozi wa amani Tanzania Risasi Mwaulanga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo leo jijijni Dar es Salaam.

“Nawaomba UKAWA warudi bungeni ili tuweze kupata katiba mpya itayoyokidhi changamoto za watanzania wote na sio masuala ya vyama vya kisiasa na maslahi binafsi kwani vyama hiyvo vinaweza kutoweka wakati wowote na nchi ikabaki palepale”.Alisema Mwaulanga.

Aidha Mwaulanga anaiomba iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya jaji Warioba, viongozi wa dini, na asasi za kiraia kuendelea na jitihada za kuitaka UKAWA kurejea Bungeni ili kurahisisisha upatikanaji wa Katiba mpya yenye maslahi mapana kwa ummma kuliko ya kisiasa.

Balozi huyo wa amani amesema kuwa kauli za vitisho na uvunjifu wa amani unapaswa kupigiwa kelele na kulaniwa na kila mwanademokrasia duniani katika kipindi hiki cha kuandaa Katiba mpya ili wajumbe waweze kuwa huru wakati wa kutoa maoni.

Tanzania ni nchi ya amani,umoja, upendo na maelewano na siyo nchi ya vita,chuki na mafarakano hivyo watanzania tunapaswa kutambua ni Katiba gani tunayoitaka na kuwa na mtazamo sahihi na maamuzi bora.

TAASISI YA WATUMISHI HOUSING KUTUMIA BILIONI 400 KUJENGA NYUMBA ZA WATUMISHI WA SERIKALI


4.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa akitoa mada kuhusu mkopo wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa kwa watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa warsha ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Agosti 14, 2014.
3.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatia uwasilishaji wa mada kuhusu mkopo wa nyumba bora za watumishi wa umma wakati wa warsha iliyotolewa na Taasisi ya Watumishi wa Housing Company leo Alhamisi Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA BENJAMIN SAWE- MAELEZO
 
Na Ismail Ngayonga
MAELEZO

Dar es Salaam
TAASISI ya Watumishi Housing Company imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi za watumishi wa Serikali katika mikoa 13 nchini.

Ujenzi wa nyumba hizo unatarajia kuanza mwezi oktoba mwaka huu, ambapo katika awamu ya kwanza, taasisi hiyo imepanga kujenga jumla ya nyumba 2500 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/15 na Mikoa itayonufaika na ujenzi wa nyumba hizo ni Mtwara, Rukwa,Mbeya, Morogoro, Dodoma, Pwani, na Dar es Salaam.

Mikoa mingine ni pamoja na Tanga, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Kigoma na Kilimanjaro, na jumla ya nyumba 50,000 zinatarajiwa kujengwa na taasisi hiyo hadi kufikia mwaka 2019.

Akizungumza katika warsha ya siku moja kwa Watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Fred Msemwa alisema mara baada ya kukamilika nyumba zinatarajia kuuzwa kiasi cha Tsh. Milioni 19 hadi Milioni 119.

Dkt. Msemwa alisema mpaka sasa Ofisi imeanza utaratibu wa kuuza vipande vitavyowekezwa katika ardhi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Mfuko wa Pensheni wa mashirika ya Umma (PPF), mfuko wa pensheni wa watumishi wa umma (PSPF), na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF),

Mifuko mingine ni pamoja na mfuko wa pensheni wa watumishi wa Serikali za Mitaa ( LAPF), mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF), pamoja na Shirika la Nyumba la Taifa, ambapo waombaji watapaswa kupitisha maombi yao kupitia kwa waajiri wao.

Aliongeza kuwa tayari ofisi yake imekwishapata maelekezo kutoka katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo moja ya masharti ni pamoja na makato ya riba yasiyozidi aslimia 10, na mtumishi atatakiwa kutumia kipindi cha miaka 5 hadi 25 ili kurejesha mkopo katika taasisi hiyo.

Akifafanua zaidi Dkt. Msemwa alisema Nyumba hizo zitakuwa ni za kisasa zaidi kwani maeneo yote yaliyojengwa nyumba hizo yamepimwa na kutakuwa na miundombinu bora zaidi ikiwemo barabara, maji na umeme, hivyo aliwataka watumishi wa umma kujitokeza kwa wingi ili waweze kujipatia nyumba hizo.

Kwa mujibu wa Dkt. Msemwa mpaka sasa wamepokea jumla ya maombi 500 kutoka kwa watumishi wa Serikali na ofisi yake imeanza mchakato wa kupitia maombi hayo na kuangalia kama wamekamilisha vigezo vya kimsingi ikiwemo masharti ya kuwa mwajiriwa katika sekta ya umma pamoja na kuwa mwanachama wa mfumo wowote wa pansheni.

“Leo hii watumushi wengi wa Serikali wameshindwa kununua nyumba kutoka katika taasisi mbalimbali, utakuta nyumba ya Tsh. Milioni 30,000,000 mtumishi anatakiwa kukatwa asilimia 10 ya mshahara wake ambayo ni Tsh. 3,000,000, hivyo wengi wao wamejikuta wakishindwa” alisema.

CHADEMA YASHINDWA KULIPIA KODI OFISI YA RUAHA MJINI CCM YAIMILIKI


IMG_9966 
Katibu wa CCM kata ya Ruaha Rashid Shungu ( wa  pili  kushoto ) na kada wa Chadema aliyehamia CCM Ibrahim Mmasi  pamoja na  wanachama  wengine wa CCM wakiwa  wameshika bendera ya CCM ambayo itapepea katika ofisi mpya ya kata ya Ruaha ,ofisi ambayo awali ilikuwa ikimilikiwa na Chadema kabla ya  kufukuzwa kwa  kushindwa kulipa deni la kodi kiasi cha Tsh 540,000 , kushoto fundi rangi akiendelea  kupaka rangi ya CCM

IMG_9940 
Fundi akipaka rangi kuta za ofizi hiyo



CHAMA  cha  demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kata ya Ruaha  jimbo la Iringa  mjini kimepata  pigo  kubwa baada ya kufukuzwa katika nyumba  waliyopanga kama ofisi  ya kata  hiyo baada ya  kushindwa  kulipa deni la  pango  kiasi cha Tsh 540,000 walizokuwa  wakidaiwa na mwenye nyumba  deni  ambalo limelipwa  na Chama  cha mapinduzi (CCM ) kata ya  Ruahakabla ya  kuichukua ofisi  hiyo .
 
Mmiliki  wa nyumba  hiyo iliyopo mtaa wa Ngeleli Ipogolo Bi  Neema Mwasika alifikia  hatua  hiyo ya  kuwataka  kuondoka katika  ofisi  hiyo baada ya  jitihada za  kudai  deni lake  kushindikana na  hivyo kulazimika  kupangisha nyumba   hiyo yenye  chumba  kimoja na sebure  kwa  mpangaji mpya ambae ni CCM kata ya Ruaha.
 
Akizungumza na waandishi  wa habari  leo katibu  wa  CCM kata ya Ruaha Rashid Shungu alisema  kuwa  awali CCM  kilikuwa na ofisi  yake  eneo la Ruaha  jirani na mto hivyo  kutokana na mvua  kubwa  zilizonyesha mwaka jana  zilipelekea  ofisi hiyo  kuharibiwa  vibaya na  hivyo  kukosa kabisa  ofisi .
 
Alisema kuwa  kutokana na kutokuwa na ofisi  cham a kilikuwa  kikitumia nyumba ya mtu binafsi kama  ofisi  pale ilipohitajika  kukutana  viongozi ama wanachama  .
 
Shungu alisema  kuwa jitihada za  kutafuta  nyumba ya  kupanga  ili  kutumika kama  ofisi ya muda ya  CCM kata  hiyo ya  Ruaha  ziliendelea kufanyika  chini ya aliyekuwa kada wa Chadema kata  hiyo kabla ya  kujiunga na CCM Bw  Ibrahim Mmasi
 
Hata  hivyo  alisema ofisi  hiyo alisema kuwa baada ya  kuona  ofisi  hiyo imefungwa kwa  muda na kuwasiliana na mwenye nyumba alikubali  kuwapangisha kwa makubaliano ya  kulipa deni kwanza jambo ambalo  lilifanyika  hivyo na kulipia kodi ya miaka  miwili zaidi.
 
” Tumeipata  ofisi  hii kihalali na sio hujuma kwani  makubaliano  kati ya mmiliki wa nyumba na mpangaji yalifanyika na  hivyo kwa  kuwa  hitaji letu  nyumba ya kupanga  tuliona  hiyo  ina  sifa ambayo tuliitaka  hivyo  tunachofanya ni kufuta rangi na nembo  za Chadema na kuweka rangi ya CCM na nembo  zetu …..na tutaizindua rasmi jumapili  wiki  hii”
 
Kwa upande wake  kada   wa CCM aliyehama kutoka Chadema Bw Mmasi  alisema  kuwa ofisi hiyo  ilikuwa imezinduliwa na viongozi wa  kitaifa  kupitia zoezi la oparesheni Sangara tarehe 19 mey 2011 chini ya  naibu mkuu wa Chadema enzi hizo Zitto Kabwe na mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa na viongozi  wengine .

SERIKALI YAJIPANGA KUKABILIANA NA EBOLA TANZANIA

Na Karoli Vinsent

SERIKALI imesema hakuna mtanzania yeyote aliyegundulika kuwepo na Ugonjwa wa Ebola ,bali serikali imejipanga kuhakikisha hakuna Mtu atakayeupata Ugonjwa  huo.
        Kauli hiyo ya Serikali inakuja Siku moja kupita Baada ya Gazeti la Sani,toreo la Jana Jumatano   tarehe 13 hadi  18 mwezi huu,kuripoti taarifa  juu ya kuingia Ugonjwa wa Ebola nchini.
             Akinusha Taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo Assah Mwambene,amesema taarifa  hiyo haina ukweli , kwani hakuna Mtanzania yeyote aliyegundulika kuwa na ugonjwa huo.
              “Gazeti hilo limeandika taarifa ambayo sio za kweli kwani hakuna mtanzania ambaye amegundulika kuwapo na ugonjwa wa Ebola na serikali kwasasa imejipanga kuhakikisha hakuna mtanzania ambaye ataupata ugonjwa huo kwa sasa”alisema Mwambene.
                Mwambene ambaye pia ni Msemaji wa Serikali alizidi kusema kwa sasa amemwandikia Barua Mhariri wa Gazeti la Sani na kumtaka ndani ya siku 18 awe amekanusha Taarifa hiyo,ambayo imewachanganya wananchi na kuwapa hofu kubwa.
                    Vilevile Mwambene alitumia nafasi hiyo kuwasihi Wahariri na Waandishi wa Habari nchini kufanya kazi kwa ukweli na wazi.
“Natumia nafasi hii,kuwaomba waandishi wa Habari nchini pamoja na Wahariri kufanya kazi kwa weredi mkubwa tukumbuke Habari za Ugonjwa wa Ebola ni habari za kuwa makini sana ,hizi sio Habari kama za UKAWA,hizi ni Habari zinazohusu maisha ya watu moja kwa moja kwahiyo tuwe makini sana”alisema Mwambene.
              Taarifa hiyo ya Mwambene inakuja siku moja kupia baada ya Gazeti hilo pendwa toreo No.1148 la kuanzia Jumatano 13 hadi 18 mwezi lilobeba kichwa cha Habari Ebola Yatua nchini,huku likitoa picha ya Mgonjwa ambaye ameupata ugonjwa huo,taarifa hiyo ambayo ilizidisha hofu kubwa kwa Watanzania.
               Ugonjwa huo wa Ebola ambao mpaka sasa umeua watu zaidi ya elfu kumi huko Afrika ya Magharibi na kujeruhi mamia ya watu,huku mpaka sasa hakuna dawa ya Ugonjwa huo .    

NNCR=Mageuzi;Hatuvumilii wasaliti wa UKAWA

Na Karoli Vinsent
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR Mageuzi Jems Mbatia amesema chama chake,hakitamvumila mjumbe  ambaye atausaliti Umoja wa Kutetea katiba ya Wananchi UKAWA na kurejea kwenye Vikao vya Bunge Maalum la katiba,basi kama akitokea chama hicho kitamchukulia hatua kali sana.
               Kauli hiyo ya Jemsi Mbatia ameitoa ,Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anaongea Wajumbe wa Mkutano mkuu wa Chama cha NCCR mageuzi kuhusu mipango mbalimbali ya kukijenga chama hicho,ambapo Mbatia alitumia nafasi hiyo kuwasihi wajumbe wanaotoka chama chake kuachana kabisa na mipango ya kurejea kwenye Bunge hilo kwa madai mchakato wa katiba umujumiwa na CCM.
            Na endapo ikitokea mjumbe ambaye atakwenda kinyume na kurejea kwenye Bunge Maalum La Katiba basi atakuwa amejifukuzisha mwenyewe kwenye Chama hicho.
            “Ngoja kabisa niseme endapo Mjumbe yeyote  anayetokana na Umoja huu wa Ukawa anayetoka chama NCCR Mageuzi akirejea kwenye Bunge hilo basi ajue kabisa chama hakitamvumilia na kitamchukulia hatua kali sana ya Kinidhamu ikiwezekana hata kumfukuza kabisa,maana atakuwa amekwenda kinyume na mapendekezo ya Chama chetu”alisema Mbatia
              Kauli hiyo ambayo iliungwa na Wajumbe wote wa Chama hico waliokuwepo Ukumbini hapo na kuitikia wote kwa sauti moja kwamba mjumbe yeyote kutoka chama cha NCCR mageuzi basi ajue atakuwa amejifukuzisha mwenyewe.
            Mbatia ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba alisema Umoja huo wa ukawa hauwezi kukatishwa Tamaa na wajumbe wachache walioasi na kurejea kwenye Bungeni,kwani yeye anajua tama ya fedha ndiyo iliyowapeleka huko.
               “Tumeona jinsi wajumbe wachache wa Ukawa ambao wametusaliti na kurejea Bungeni juzi na wajumbe hao wametoka kwenye chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na wamefanya hivyo hao wajumbe ni tamaa za pesa ndizo zimawarudisha bungeni tu na wala hawakuwa teyali kuwatetea wananchi na sisi hatuwezi kukatishwa na watu hao”alizidi kusema Mbatia
            Vilevile Mbatia alitumia nafasi hiyo kumshambaulia Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta,na kusema ndiye mtu ambaye anafaa kulaumiwa kutokana na yeye kusimamia upotevu wa Mabilioni ya Watanzania huku akijua Katiba haiwezi kupatika.
               Mbatia ambaye vilevile ni Mbunge wa kuteuliwa na Rais alizidi kusema Bunge hilo linafanya ufisadi wa kutisha kwenye pesa za Watanzania.
                 “Jamani nchii hii ni masikini leo ukipita mjini balabala ni mbovu,lakini Sitta anaendelea kusimamia Bunge la katiba ambalo limejaa ufisadi wa kutisha,haiwezekani kabisa bunge hili la katiba vipaza sauti tu kwa siku vinatumia milioni tisa,jamani Sitta haoni huu wizi kweli?”
                     “Leo wajumbe walioko huku bungeni wanatupigia simu na kusema mnakosa pesa ,eti wanasema hivyo kutokana na wao wamefuta jumamosi na jumapili kwenye ratiba za bunge maalum,badala yake wamejingezea siku sitini,yaani maana yake kila mbunge ataondoka kwa kwenye vikao hivi zaidi ya milioni 27 huku wakijua katiba haitopatikana kutokana na kutokuwa 2ya 3”alizidi kuhoji Mbatia
                Katika hatua nyingine Chama hicho kimezidi kumuomba Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge maalum la Katiba kutokana na kukosa sifa ya kuendelea kwake badala yake wameomba katiba iliyopo iendelee na kupisha uchaguzi mkuuu na katiba hiyo ya zamani ifanyiwe marekebisho ikiwemo kuwepo na kipengere cha tume huru ya Uchaguzi,pamoja na umri wa mgombea wa Urais upunguzwe,  
          Na uchaguzi mkuu ukikamilika basi mchakato wa katiba mpya uendelee.Ukawa ni muunganiko wa  vya  Vikuu vya Upinzani ikiwemo CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi pamoja na Baadhi ya wajumbe 201 waliochaguliwa na Rais Kikwete wamesusia vikao hivyo kwa madai mchakato huo umehujumiwa na CCM.

Sunday, 10 August 2014

ZITTO ATIKISA MWIDAU CUP PANGANI


100_8828
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa mashindano ya soka ya Mwidau CUP leo mjini Pangani. IMG_5362
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiingia uwanjani kuzindua mashindano ya Mwidau CUP .Kushoto ni mdahamini wa mashindano hayo ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau. IMG_5373
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiwa ameshika ngao ya hisani ambayo iliwania katika mchezo wa ufunguzi wa Mwidau CUP, ambapo timu ya Torino iliibamiza APL ya Mwera bado 2-0

WANAWAKE WOTE DUNIANI TUNALILIA AMANI – MAMA PINDA

13
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
 
MKE WA WAZIRI MKUU, Mama Tunu Pinda amesema wanawake wote duniani wanalilia amani na hawapendi vita wala machafuko kwani husababisha amani kutoweka kwenye familia na vifo vya watu wasio na hatia.
 
Ametoa wito huo leo mchana (Jumapili, Agosti 10, 2014) wakati akitoa mada kama mzungumzaji mkuu (keynote speaker) kwenye Mkutano wa Dunia wa siku tano ulioanza leo jijini Seoul, Korea Kusini.
 
Mkutano huo ambao umeandaliwa na taasisi ya Universal Peace Federation (UPF) ambayo inatoa ushauri kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uchumi na Kijamii unajadili masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo.
 
Akiwasilisha mada yake kuhusu usalama, amani na maendeleo barani Afrika, Mama Tunu Pinda alisema: “Ninaiomba jamii ya Kimataifa duniani kote tusimamie amani na usalama kwani kinyume na hapo ni kuleta machafuko na vita. Wanawake hatupendi vita wala machafuko…,” alisema huku akishangiliwa.
 
Aliwataka washiriki wa mkutano huo wasimame katika nafasi zao kama baba na mama, kama kaka na dada na kuhakikisha kuwa dunia inakuwa ni mahali pazuri pa kuishi. “Ninawasihi tuendeleze maono ya Muumba wetu, tuweke utu mbele kwa kuwajali wengine na tuache kutanguliza maslahi yetu binafsi,” alisema.
 
Mapema, akiwakaribisha wajumbe zaidi ya 500 kutoka nchi 68 wanaoshiriki mkutano huo, Rais wa UPF, Dk. Thomas Walsh alisema taasisi hiyo inasimamia misingi ya amani, usalama na maendeleo ya jamii kwa nia ya kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa mataifa mbalimbali.
 
Alisema anatumaini uwepo wa wakuu wa nchi mbalimbali na viongozi mashuhuri, utasaidia kupata majibu ya changamoto inayoikabili dunia juu ya upatikanaji wa amani ya kudumu.
 
Naye, Mfalme Letsie Mswati III kutoka Lesotho, akizungumza katika mkutano huo alisema dunia inakabiliwa na changamoto nyingi za ukosefu wa amani kubwa ikiwa ni uharibifu wa mazingira. Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wanahimiza utunzaji wa mazingira kama njia ya kupunguza matatizo yanayojikeza kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
 
Alionya kwamba kuna haja ya kuweka mifumo madhubuti ya kuhakikisha kuwa dunia haiendelei kuwa na matukio ya kigaidi na matumizi ya silaha za maangamizi. “Kama tutakubali vita viendelee kutokea, na migogoro isiyokwisha barani Afrika na nchi za Uarabuni, ni lazima tukubali kuwa hakutakuwa na maendeleo katika mabara haya,” alisema.