Saturday, 29 November 2014

UFAFANUZI WA MASUALA MBALIMBALI YA TIMU YA MBEYA CITY COUNCIL FOOTBALL CLUB.

MBEYA CITY COUNCIL FOOTBALL CLUB


Klabu ya Mbeya City Council Football Club leo 25/11/2014 inatoa ufafanuzi wa mbalimbali ikiwemo suala la utaratibu wa maslahi kwa watumishi wake (benchi la ufundi, wachezaji na watumishi wengine) na uwepo wa fedha za wadhamini katika klabu yetu.

Uamuzi wa kutoa taarifa hii umefikiwa baada ya vikao vya menejimenti na kamati ya fedha na utawala kufuatia taarifa mbalimbali zinazozalishwa kila siku juu ya klabu yetu toka katika vyanzo ambavyo sio vya klabu

MASLAHI YA WACHEZAJI
Hivi karibuni baadhi ya wadau wa mchezo wa mpira wa miguu wamehusisha matokeo ya uwanjani iliyopata timu na maslahi kwa wafanyakazi wa klabu kama taasisi.

Sehemu kubwa ya wafanyakazi wa klabu ikijumuisha timu ni wafanyakazi chini ya masharti ya mkataba chini ya muajili ambaye ni Halmashauri ya jiji la Mbeya, Hivyo maslahi ya mfanyakazi(kwa kada hii) hujadiliwa na kukubaliana kwa pande zote mbili(Klabu kwa niaba ya muajiri na Mchezaji kama muajiriwa) kulingana na bei ya soko ndipo mkataba husainiwa.

Klabu imeweka utaratibu wa namna ya wafanyakazi wake kujadiliana na mwajili kuhusu mambo mbali mbali yenye lengo la kuboresha utendaji wa kazi na mazao yake pamoja na masuala ya maslahi pindi kukiwa na haja hiyo.

Mishahara ya wachezaji pamoja na kuamuliwa kwa makubaliano baada ya majadiliano ya pande zote mbili pia bei ya soko huangaliwa na kuzingatiwa. Msimu wa 2014/2015 mishahara ya wachezaji ilipanda kati ya asilimia 100 – 300(%) ikilinganishwa na msimu uliopita 2013/2014.

Posho zote zitolewazo na klabu zilirekebishwa ikilinganishwa na msimu uliopita kwa kuzingatia makubaliano kati ya wachezaji na menejimenti kabla ya kuanza kwa msimu huu.

Klabu inatambua wazi kuwa mpira ni ajira kama zilivyo ajira zingine,maslahi haya yamewekwa kwa makusudi ili kuboresha hali za maisha za wafanyakazi wetu hasa wachezaji kwani hiyo ndiyo ajira yao.
Ukiondoa mshahara unaoendelea kulipwa kila mwezi hakuna mfanyakazi yeyote anayedai chochote kati ya maslahi yake.

FEDHA ZA WADHAMINI:

Pamoja na kuwa na kipengele cha kutotoa siri (Confidentiality)za mikataba yetu na wadhamini wetu, klabu inasikitishwa namna ambavyo umma wa wanamichezo unavyopotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa changamoto ambazo klabu inapitia hivi sasa kama taasisi zinatokana na kuwepo kwa fedha za wadhamini.

Klabu inaomba ikumbukwe kuwa katika msimu uliopita 2013/2014 ilitumia zaidi ya shilingi milioni 700 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri ikiwa kama mmiliki wa klabu. Wadhamini kwa mujibu wa makubaliano hawajatoa wala hawatoi fedha zote mara moja kwa mujibu wa mkataba, fedha hizo hutolewa kila mwezi na kwa awamu.

Matumizi ya kawaida ya klabu kwa mwezi si chini ya shilingi 49,000,000.00(bila kuhusisha mishahara), katika kipindi cha Julai-Sept 2014, Klabu ilikuwa na mdhamini mmoja tu ambaye ni Binslum tyres Co Ltd anayetoa shilingi 15,000,000.00 kwa mwezi sawa na shilingi 180,000,000.00 kwa mwaka kwa mujibu wa mkataba uliopo.

Ukiangalia mahitaji ya klabu kwa mwezi mmoja hapo juu, fedha hizi za mdhamini zilichangia asilimia 30.6(%) ya gharama za klabu kwa mwezi.  Hii ikiwa na maana kuwa bado asilimia 69.4(%) ya gharama za uendeshaji wa timu zilitoka Halmashauri.

Kuanzia mwezi oktoba 2014 ambapo kampuni ya coca cola ilisaini mkataba wa udhamini na klabu yetu. Kampuni ya Coca Cola itakuwa inatoa fedha taslimu Tsh 60 milioni ambazo inazitoa kwa mwaka. Fedha hizi hutolewa kila baada ya robo mwaka shilingi milioni 15. Hii ina maana kuwa coca cola inatoa shilingi 5,000,000.00 milioni kila mwezi.

Hivyo kuanzia mwezi oktoba klabu inapata toka kwa wadhamini wake wawili (Binslum Tyre Co Ltd na Coca Cola Kwanza) shilingi 20,000,000.00 kwa mwezi. Fedha hizi zinachangia asilimia 40.8(%) ya gharama za uendeshaji wa timu kwa mwezi na asilimia 59.2(%) ya gharama hizo bado zinabebwa na Halmashauri.

Uwepo wa wadhamini hivi sasa haujaongeza fedha kutoka katika bajeti hiyo bali umepunguza utegemezi wa timu kwa Halmashauri.
Hivyo basi shutuma zinazotolewa na baadhi ya wadau  kuwa changamoto ambazo timu inazipitia kwa sasa ni kutokana na kuwepo kwa fedha za wadhamini ni
UPOTOSHAJI MKUBWA.
MWALIMU JUMA MWAMBUSI

Mwalimu Juma Mwambusi ni muajiriwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya anayesimamia benchi la ufundi la timu yetu.

Menejiment ilikutana na Mwl Juma Mwambusi katika vikao vyake vya kawaida kupitia changamoto kadhaa zilizojitokeza katika michezo saba ya awali mara baada ya kuwasilisha ripoti ya maendeleo ya timu. Mwalimu Mwambusi na menejiment tumeridhiana kwa faida ya mpira wa miguu na jamii inayoizunguka timu yetu anaendelea kuifundisha timu ya Mbeya City Fc.

Nachukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa Mwl.Juma Mwambusi ndiye Kocha Mkuu wa timu na hivi sasa anandaa program ya mafunzo kwa mzunguko wa pili wa ligi unaotarajia kuanza disemba 2014.

MWISHO

Klabu kama taasisi inayokuwa inapitia katika changamoto mbalimbali, ni imani ya menejimenti kuwa changamoto hizi zitaiimarisha na kuikomaza klabu ili kuwa klabu bora zaidi kwa vizazi vijavyo.

Tunatoa shukrani za dhati kwa wadau wetu wote wanaoendelea kutuunga mkono katika kipindi hiki.
Imetolewa na

E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC 

Thursday, 27 November 2014

BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA AKUTANA NA DR. SHEIN


unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo kwa Rais baada ya kuteuliwa rasmi.[Picha na Ikulu.]
unnamed1 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo  kujitambulisha  kwa Rais baada ya kuteuliwa .[Picha na Ikulu.] unnamed2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana  na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka baada ya mazungumzo  alipofika   kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar baada ya kuteuliwa.[Picha na Ikulu.]

...SAKATA LA ESCROW KULAMBA VIGOGO WA SERIKALI

.

Ripoti ya kashfa ya fedha zilizochotwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zaidi ya Shilingi Bilioni 300 kutoka Benki Kuu (BoT), imewasilishwa Bungeni mjini Dodoma hii leo na kusomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe na Makamu wake Deo Filikunjombe kusoma mapendekezo ya Kamati hiyo dhidi ya wote waliotajwa katika sakata hilo.

Katika mapendekezo yake miongoni mwa viongozi wa juu wa Serikali waliotolewa maamuzi kuwa wajiuzulu nyadhifa zao za kuteuliwa na kuchaguliwa ni pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Elaichim Maswi.

Pia katika orodha yao wapo viongozi wa dini na wanasiasa ambao walichota fedha hizo za umma.

WATANZANIA KUPIGIA KURA JEZI YA TIMU YA TAIFA


Watanzania wanatakiwa kupigia kura jezi ya timu ya Taifa ya nyumbani na ugenini kupitia mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa www.tff.or.tz ambapo jezi hizo zimewekwa.

TFF ilipokea mapendekezo ya mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa kutoka kwa Watanzania 86. Jezi 11 za nyumbani, bukta nane za nyumbani, jezi nane za ugenini na bukta tano za ugenini ndizo zimepitishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.

Mwisho wa kupiga kura ni Desemba 31 mwaka huu. Mpigaji kura anatakiwa kubonyeza kwenye jezi na bukta ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini.

Tunawashukuru wote waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa.

Monday, 24 November 2014

MKUSANYIKO WA U12 DAR ES SALAAM


Watoto wenye umri chini ya miaka 12 wa Mkoa wa Dar es Salaam wanakusanyika kesho Jumamosi (Novemba 22 mwaka huu) asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa ajili ya kusaka kombaini ya mkoa.

Mkusanyiko wa kusaka kombaini hiyo kwa ajili ya timu itakayoshiriki mashindano ya Taifa yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao uko chini ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).

Wachezaji hao wataanza kujaribiwa saa 1 hadi saa 5 asubuhi. Mashindano ya Taifa yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu.


TUCTA WAJITOSA KWA JK

Na karoli Vinsent

CHAMA cha Wafanya kazi nchini (TUCTA) nao wamejitosa Kwa  mara ya Kwanza kwenye sakata la Ufisadi wa zaidi ya bilioni 400 za kitanzania kwenye Akaunti ya Escrow na kusema  chama hicho hakiwezi kukubaliana na ufisadi huo na kuitaka serikali kuwachukulia hatua kali ya watu wate waliohusika na wizi.
    Na  kama endapo Bunge pamoja na serikali hawatawachukulia hatua zozote Viongozi waliohusika na wizi huo, basi TUCTA itachukua Jukumu la kuwaunganisha wakulima na wafanyakazi wa idara zote kushikilia bango suala hilo.
     Kauli hiyo kali imetolewa leo Jijini Dar Es Salaam na Rais Mpya wa Chama cha Wafanyakazi nchini TUCTA Gration Mukoba wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, ambapo Mukoba alisema wao TUCTA ambao nao pia ni walipa kodi nchini  hawawezi kukubaliana na wizi wa zaidi ya Bilioni 400 kwenye Akaunti ya Esrow.
“Kusema kweli sisi wafanyakazi tumechoka na hali ya Ufisadi unaoendelea nchini, na ukizingatia sisi TUCTA ni walipa kodi wakubwa sana ,tunasikitika sana kusikia serikali inaweza kusimamia mambo ya ufisadi yanayotokea maeneo  mbalimbali nchini, na sisi vyama vya Wafanyakazi nchini kwa pamoja tunaiomba serikali iwachukulia hatua kali sana Viongozi waliohusika kwenye wizi huu wa mali za umma”alisema Mukoba.
Mukoba aliongeza kuwa kwamba wafanyakazi nchini wanaishi katika mazingira magumu sana huku wengine bado wakiwa wananchukua mashahara mdogo ambao usioendana na hali ya maisha ya sasa na wanasikitika kusikia pesa zinaibwa  na watendaji wa serikali  na huku wakishindwa kuchukuliwa hatua.
      Aidha Mukoba aliwashangaa watu ambao wanasema pesa ambazo zimeibwa kwenye Akaunti ya Escrow kusema sio za umma bali ni za wamiliki wa Kampuni ya IPTL  na kusema sio kweli kwani  pesa hizo ni za watanzania wote, kwani zimechukuliwa kwenye shirika la Umeme nchini Tanesco.
       Vilevile TUCTA waliitaka Jamii kujiweka Tayari kuungana nao ili kuchukua maamuzi magomu kuhusu ufisadi huo na  kama endapo Serikali itashindwa kuwachukulia hatua Viongozi waliohusika kwenye wizi huo ambao haujawai kutokea tangu nchi kupata Uhuru.

Friday, 21 November 2014

KESI YA MADAI DHIDI YA MAOFISA WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KUDAIWA KUIFUNGA KLINIKI YA FOREPLAN HERBAL YAWAVUTA WATU WENGI

 Mawakili kutoka Kampuni ya Kamanija and Company Advocates,  wanao mtetea Dk. Juma Mwaka katika kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya maofisa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wanaodaiwa kuifunga Kliniki ya ForePlan Herbal iliyopo Ilala, inayomilikiwa na Dk.Mwaka, wakizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo, mara baada ya kusikiliza kesi hiyo ambapo itatolewa uamuzi Novemba 26 mwaka huu iwapo kama upande wa jamhuri utaunganishwa katika kesi hiyo. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Flora Haule. Kutoka kulia ni Wakili Charles Kamanija, Ngassa Ganja na Revocatus Thadeo.
 Mawakili hao wakibadilishana mawazo kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo ambayo imewavuta watu wengi wakiwepo wanahabari kutokana na unyeti wake.
 Wakili wa Serikali, Karim Rashid akizungumza na wanahabari kuhusu kesi hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

Wananchi mbalimbali wakisubiri kusikiliza kesi hiyo.

Thursday, 20 November 2014

SHROSE BANJ AZIDI KUFANYA UJINGA KWENYE BUNGE LA EAC,AIABISHA SERIKALI CCM,ASHINDWA KUJENGA HOJA AISHIA KUPIGANA,SOMA HAPA KUJUA



Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutoka Tanzania Shy -Rose Banji (pichani) na Nderakindo Kessy, wanadaiwa kuingia katika mtafaruku wakiwa jijini Nairobi, Kenya katika vikao vya Bunge hilo.

Taarifa za tukio hilo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Shy-Rose anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kamkunji, Nairobi.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa sababu za kushikiliwa kwake ni baada ya kumkunja na kumpiga ngumi mbunge mwenzake na chanzo cha ugomvu hakijajulikana.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa Kessy ambaye anatoka NCCR-Mageuzi, alikumbana na kipigo hicho juzi jioni, Jijini Nairobi.

“Tumepokea taarifa kutoka kwa Wabunge wa Rwanda wakinieleza kwamba Nderakindo, amepigwa na mbunge mwenzake (Shy-Rose) na kuumizwa vibaya, tuliomba msaada apelekwe hospitali huku tukiendelea kuzungumza na mwanasheria aliyeko Nairobi tufungue kesi,” alibainisha Mbatia.

Hivi karibuni, Mbunge Nderakindo, alisikika akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kuhusu sakata la baadhi ya wabunge kutaka kumtimua Spika wa Bunge hilo, Dk. Margaret Zziwa, kwa madai ya kushindwa 

SDL SASA KUANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 6

Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu huu iliyokuwa ianze kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu kwa mechi kumi katika viwanja vitano tofauti imesogezwa mbele hadi Desemba 6 mwaka huu.

Mechi hizo zimesogezwa ili kutoa fursa ya kukamilisha maandalizi mbalimbali ya ligi hiyo inayoshirikisha timu 24 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Mikoa yenye timu katika ligi hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Katavi, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora.

MASHINDANO YA TAIFA YA U12 YASOGEZWA
Mashindano ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 yanayoshirikisha kombaini za mikoa yote ya Tanzania yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 30 mwaka huu hadi Januari 5 mwakani.

Awali mashindano hayo yalipangwa kuanza Desemba 6 mwaka huu, lakini yamelazimika kuyasogeza ili kutoa fursa ya kukamilika kwa matengenezo ya viwanja vitatu ambayo vitatumika.

Kila timu ya mkoa inatakiwa kuwa na ujumbe wa watu 16, wakiwemo wachezaji 14 na makocha wawili katika mashindano hayo ya timu yenye wachezaji saba (7 aside).

Timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu tayari kwa ajili ya uhakiki wa umri na taratibu nyingine za mashindano. Timu zote zitafikia katika shule ya Alliance (Alliance Schools).

Wachezaji wanaotakiwa kushiriki mashindano hayo ni wenye umri chini ya miaka 12, hivyo ni wale waliozaliwa kuanzia Januari 2003 na kuendelea.

RAMBIRAMBI MSIBA WA MUNYUKU, KARASHANI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko vifo vya waandishi wa habari Innocent Munyuku na Baraka Karashani vilivyotokea jana (Novemba 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu, na tasnia ya habari nchini kwa ujumla kutokana na mchango mkubwa waliotoa katika ustawi wa mpira wa miguu nchini kupitia kalamu zao.

Munyuku alikuwa mmoja wa waandishi waanzilishi wa gazeti la Mwanaspoti wakati Karashani kwa nyakati tofauti alifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo kampuni ya New Habari 2006 akiripoti habari za mpira wa miguu.

Tunatoa pole kwa familia za marehemu, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), na kampuni ya New Habari 2006 na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Monday, 17 November 2014

JAJI MKUU AMJULIA HALI RAIS MAREKANI


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini  Washington  na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nhini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya  rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi, daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein Katanga.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji wa Mahakama Ya Rufani Tanzania Mhe Ibrahim Juma  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe Ignass Kitusi  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe Ignass Kitusi  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Meja Jenerali Adolph Mutta ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani  Dkt. Sweetbert Mkama ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014

TFF YAIPONGEZA AFRIKA KUSINI KWA KUFUZU AFCON


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa pongezi kwa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kufuatia timu yake ya Taifa (Bafana Bafana) kufuzu kucheza fainali zijazo za AFCON nchini Equatorial Guinea.

Afrika Kusini iliifunga Sudan mabao 2-1, hivyo kufuzu kabla ya kukamilisha michezo yote. Bafana Bafana bado imebakiza mchezo mmoja katika hatua hiyo.

Wakati huo huo, TFF imeipeleka barua ya shukrani kwa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kwa kufanikisha kambi ya Taifa Stars nchini humo kabla ya kwenda kucheza Swaziland.

SAFA ilitoa viwanja vya mazoezi kwa Taifa Stars na usafiri wa basi la kisasa kutoka Johannesburg kwenda Swaziland na kurudi, hivyo kuokoa zaidi ya dola 15,000 ambazo TFF ingetumia kama ingegharamia yenyewe safari hiyo au kuweka kambi ya timu hiyo nyumbani.

Awali Benchi la Ufundi la Taifa Stars chini ya Kocha Mart Nooij lilipendekeza timu kufika Swaziland mapema au kuweka kambi nchini Afrika Kusini. SAFA ikajitolea kusaidia kambi hiyo.

Pia TFF inakanusha madai ya gazeti moja la kila siku lililodai kuwa wakaguzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wamevamia/wamefanya ukaguzi wa siri kukagua fedha za udhamini wao kwa Taifa Stars.

Ukaguzi wa hesabu ni utaratibu wa kawaida wa kila robo ya mwaka wa fedha. TFF ndiyo huwaalika TBL kutuma wakaguzi wao ili kuhakiki vitabu vya fedha. Uhusiano kati ya TFF na TBL ni mzuri, na kila kinachofanyika ni kwa nia njema kwa makubaliano ya pande zote mbili.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Sunday, 16 November 2014

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ‘KUTIMULIWA’ KWA KATIBU MKUU WA ACT-TANZANIA

Alliance for Change and Transparency-Tanzania
(Mabadiliko na Uwazi)
                 
  1. Mnamo tarehe 11 Novemba 2014 kuliripotiwa na vyombo vya habari kwamba Katibu Mkuu wa ACT-Tanzania Ndugu Samson Mwigamba alikuwa ‘ametimuliwa’ katika nafasi yake na vijana waliojiita waasisi wa chama, ambao ni Ndugu Greyson Nyakarungu na Ndugu Leopold Mahona. Tunakiri kwamba Ndugu Greyson Nyakarungu na Ndugu Leopold Mahona ni wajumbe katika Kamati ya muda ya Uongozi ya chama. Ndugu Leopold Mahona ni Naibu Katibu Mkuu (Bara) wakati Ndugu Greyson Nyakarungu ni Mjumbe wa Kamati.
  2. Kwa utamaduni wa chama cha ACT-Tanzania, tangazo la vijana hawa lilichukuliwa kama kiashiria cha tatizo linalohitaji kutatuliwa, na ambalo lilielekea kuchafua hali ya kisiasa na amani ndani ya chama. Kwa sababu hiyo, Kamati ya Uongozi ilikutana kwa muda wa siku mbili Jijini Dar es Salaam na kujadili kwa kina dukuduku walizokuwa nazo Ndugu Mahona na Ndugu Nyakarungu.
  3. Kwa kuwa chama chetu kinaamini katika uhuru kamili wa maoni ambayo yanaweza kutolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano na waandishi wa habari, Kamati ya Uongozi ilipokea taarifa iliyosambazwa katika vyombo vya habari na Ndugu Nyakarungu na Ndugu Mahona kwa tahadhari kubwa katika kulinda misingi ya chama na haki ya viongozi na wanachama kutoa maoni yao chanya na hasi kwa uwazi.
  4. Baada ya majadiliano marefu na tafakuri ya kina, viongozi tumekubaliana:
    1. kujenga utamaduni wa kuwasiliana mara kwa mara na tabia ya kutoa dukuduku zetu ndani ya vikao vya chama
    2. Pale ambapo ni muhimu kutumia vyombo vya habari kutoa dukuduku zetu kuhusu mwenendo wa viongozi wenzetu ni vizuri kufanya hivyo katika namna ambayo italinda misingi ya chama na kuendeleza udugu, umoja na amani ndani ya chama chetu na jamii kwa ujumla.
  5. Tunatoa wito kwa viongozi wetu na wanachama kwa ujumla kuendelea na maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Tunawakikishia kwamba viongozi wenu wote katika ngazi ya kitaifa tupo pamoja na tunaendelea kuchapa kazi kama kawaida.

Kadawi Lucas Limbu, Mwenyekiti wa Taifa. 

KUBUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA MWISHO KESHO


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini ambapo mwisho wa kufanya hivyo ni kesho (Novemba 15 mwaka huu). Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.
*       
Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).

Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe:info@tff.or.tz au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Friday, 14 November 2014

MACHINGA KOMPLEX


HUO I MOSHI MZITO KATIKA SOKO LA MACHINGA COMPLEX JIJINI DARESALAAM, AMBAPO SOKO HILO LINADAIWA KUTEKETEA KWA MOTO. MPAKA SASA BADO HATUJATAMBUA HASARA KAMILI NA CHANZO CHA MOTO HUO KATIKA SOKO HILO.

SOKO KUU LA WAMACHINGA LAUNGUA VIBAYA (MACHINGA COMPLEX)

-UKAWA YAZIDI KUBOMOLEWA,CHAMA CHA ACT CHAVUNA VIONGOZI WAKE ,SAMSON MWIGAMBA HAWA MWIBA MKALI, ASEMA VIONGOZI WENGI KUHAMIA ACT

Viongozi mbambali kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA wakihamia Chama cha ACT Wakipokolewa na Katibu Mkuu wa Chama ACT-Samsoni Mwigamba kuria, picha Hawadhi Ibrahim kutoka Mjengwa.Blogs
Na Karoli Vinsent
CHAMA kipya cha Siasa nchini cha Tanzania Tanzania Alliance for change and Transparency ACT kimezidi kuvuna wanachama wapya kutoka vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda Umoja wa Kutetea Katiba ya wananchi UKAWA vyama hivyo ni Chadema,CUF na NCCR- mageuzi ,baada ya leo Viongozi mbalimbali kutoka vyama hivyo kuhamia kwenye chama hicho.
       Wanachama hao ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF mkoa wa Ilala,Ramadhan Khamis na aliyekuwa mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jimbo la Korogwe na Afisa Habari Taifa wa chama hicho Tony Kamkanda

         Akithibitisha kuwapokea wananchama hao leo Jijin Dar es Salaam ,Katibu mkuu wa Chama  cha ACT-Tanzania Samson Mwigamba wakati wa Mkutano na Waandishi ambapo Mwigamba amesema  huu sio mwisho kwani chama hicho kwanzia sasa kitapokea wanachama wengi tena viongozi wakubwa tu kutoka vyama vingine vya siasa na akasema chama hicho kinawakalibisha wanachama wote kutoka vyama vyote vya siasa nchini kuhamia kwenye chama hicho kupata  Demokrasia ya kweli na yenye kulijenga Taifa kimaendeleo.
“Nawakalibisha sana wanachama wengine kuiga mfano wa wananchama hawa wapya kwani ACT ni chama ambacho chenye nia ya dhati ya kuendeleza Demkokrasia ,na sisi tuko na tofauti na vyama vingine vya upinzani  ambavyo badala ya kujenga chama vimekuwa vikiishia kuzungumza wahasisi na chama chetu hakina nia hiyo bali kiko kwa ajiri na kumkomboa mtanzania wa leo”Alisema Mwigamba
Kwa upande wake wanachama hao waliohamia ACT –Tanzania walisema wamehamia chama hicho baada ya kuchoshwa na mifumo isiyokuwa na tifa na yenye kuua Domkrasia nchini kwenye Vyama hivyo ambavyo wanadai viko kwa ajiri ya kutafuta pesa na sio kumkomboa mtanzania wa leo mwenye matatizo lukuki.
        Katika Hatuo Nyingine Chama Kipya cha Siasa nchini kinatarajiwa kuzinduliwa Rasmi tarehe 5,desemba mwaka huu,na kushuhudiwa na watu mbalimbali pamoja na vyama vingine vya kisiasa nchini.
        Akizungumzia Uzinduzi huo Katibu Mkuu huyo wa ACT-Tanzania Samson Mwigamba alisema licha ya uzinduzi huo pia chama hicho kinatarajia kumfanya mkutano wake mkuu wa Mwaka unaotarajia kufanyika Jijin Dar Es Salaam na kuwataka wananchi kukiunga chama hicho chenye malengo mazuri kwao.
KUHUSU MWIGAMBA KUFUKUZWA ACT-TANZANIA

Mwigamba alisema hawezi kufukuzwa ACT kwani  yeye yupo hapo kisheria na wanao sema hivyo na malalamiko yapo chama hicho  kitachukua hoja zao kama mapendekezo ya kukijenga chama hicho na kusema chama hicho hakina wahasisi kama wanavyodai .

Thursday, 13 November 2014

TCAA NA NDOTO YA MATUMIZI YA ANGA KUANZA KUTUMIKA KWA WATANZANIA

 
Mkurugenzi wa mamlaka ya Anga Bw. Charles M. Chacha akifafanua jambo mbele ya wadau wa usafiri uliofanyika mapema hii leo,Chacha amesema Tanzania inatatizo kubwa la viwanja vyake kutokuwa na Taa huusani vile vya mikoani
Dr. James Benedict Diu akifafanua jambo katika mkutano wa wadau, Diu ni Mkurugezni  uchumi wa mamlaka hiyo.
Wadau wakijadili jambo katika kikao hicho cha wadau wa usafiri mapema hii leo.
Mkuu wa shule ya Anga kutoka chuo Cha usafirishaji, Bw. Fimbo akifafanua jambo mbele ya wadau katika mkutano huo wa wadau. Mkutano huo umeitishwa ili kujadili mambo mbalimbali yanayoikabili sekta hiyo ya anga.

Mamlaka ya Anga hapa nchini imeendelea kuonyesha nia yake ya kuhakikisha kuwa wazawa wanakuwa mstari wa mbele kutumia huduma za ANGA ambazo kwa muda mrefu wageni wameonekana kushika hatamu katika huduma hiyo,
 
Akizungumza katika mkutano maalum wa kujadili changamoto za usafiri wa Anga katika mkutano wa wadau wa usafiri hapa nchini, Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Anga TCAA Bw. Charles Chacha amesema kwa sasa watanzania bado hawajaamkuka kutumia huduma ya usafiri wa anga,

Amesema kikwazo kikubwa kwa watanzania hao kushindwa kutumia usafiri huo ni kutokana na Ada ya kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, Lakini amewahakikishia wananchi kuwa mamlaka yake imejikita kuhakikisha kuwa changamoto hiyo inamalizwa na hivyo kuwa na bei ambayo kila mtu anauwezo nayo,
Chacha ameenda mbele na kusema kuwa kwanza wao kama mamlakayenye dhamana ya kudhibi mifumuko ya bei kwa wasafiri, wamejipanga kuhakikisha inaleta makampuni mengi ya ndege ili kuongeza ushindani katika soko hilo la usafiri wa anga hapa nchini,
 
Mipango mingine ni kuhakikisha kuwa viwanja vyetu vinajengwa miundo mbinu mizuri itakayovutia watoa huduma kuanza kufanya kai masaa 24 ili kutoa fursa kwa wazawa nao kufaidi huduma za ndege
 
Alipoulizwa swali kuwa wanafanya nini ili kuongeza idadi ya watu wanaotumia uafiri huo kuongezeka, kutoka idadi ya sasa, Mkurugenzi huyo amekiri kuwa bado ni changamoto ingawaje kwa sasa tunaviwanja takribani mia tano 500lakini bado ndege zetu zimekuwa zikilala usiku kama binadam anavyolala na hilo ni tofauti na nchi zingine ambazo ndege zimekuwa zikikesha kutokana na viwanja vyao kuwa na taa zinazoruhusu kufanya hivyo,
 
Katika hatua nyingine, mkurugenzi anayeshugulikia uchumi na udhibiti kutoka mamlka ya ANGA HAPA NCHINI Dk James Diu amebainisha baadhi ya changamoto ambazo kwa sasa zimekuwa ni kubwa katika viwanja vyetu ni kwamba watendaji bado hawana ujuzi mzuri wa kufanya kazi,
 
Ufanisi wa wafanyakazi katika viwanja vyetu bado ni changamoto hususani wakaguzi ambao pengo lao linaonekana hadharani,
Nye katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa Anga, Bw. Laurance PAUL ameelezea masikitiko yake juu ya serikali ambapo wameamua kuacha sekta mbili muhimu kuziunganisha ili kufanya ndege zetu zifanye kazi usiku na mchana,
 
AKizungumza n mtandao huu katika mahojiano maalum, Kati bu huyo amesema ili ndege zetu ziweze kufanya kazi masaa 24 kama nchi zingine ni lazima sekta ya utalii iunganishwe na usafiri wa nga ili kupata wateja wengi,
 
Pili  viwanja vyetu ni lazima vijengwe taa ambazo zitawaruhusu watoa huduma kufanya kazi zao katika nyakati za usiku kkama nchi zilizoendelea kiuchumi,
Sisi watanzaia tunaviwanja vingi sana kiasi kwamba kama tunavitumia ipasavyo na tukishusha bei watanzania wengi wataanza kutumia usafiri wa nga.

ADC YAWAVUA NGUO UKAWA, CCM,YAIBUA MAZITO AMBAYO HAJAWAHI KUANDIKWA.


 Mwenyekiti wa chama cha ADC Said Miraji akiwa pamoja na kamishna wa chama hicho kusiniNanjase H. Nanyase akifafanuazaidi kuhusu kanuni za chaguzi za mitaa na kusemakwamba ni uozo mtupu, lakini wao wanashiriki kwa shingo upande, tena wakijua wazi kunahujuma nzito inakuja

Mwenyekiti huyoa akifafanua baadhi ya vipengele ambavo vimo katika kitabu cha kanuni cha uchaguzi wa serikali za mitaa, amesema uchuzi wa mwaka huu ni wa kukurupuka, na waziri amekalia mapendekeoz ya wadau kwa kushindwa kupeleka mbele chaguzi hizo
Katika kile kinachoonekana ni kuibua uozo na uchafu wa ofisi ya waziri mwenye dhamana na uchaguzi wa serikali za mitaa, Chama cha ADC kimemwaga mboga baada ya kuweka hadharani mipango ya siri ambayo wadau wa siasa na msajiri wa vyama vya siasa hapa nchini na waziri mwenyedhamana walikubaliana huko mjini Morogoro,
Akizungumza na mtandao huu katika mahojianao maalum, hivi karibuni mwenyekiti wa chama hicho Bw. Siadi Miraji Abdallah, amesema liwalo na liwe lakini ukweli lazima usemwe ili wakati vyamapinzani vitakapoanguka katika uchaguzi wa mitaa asitafutwe mchawi nani,
Miraji ameweka wazi kuwa moja ya hoja ambayo ilikuwa na mvutano mkubwa huko Morogoro wakati wa kikao chao na waziri mwenye dhamana ni kuhusu kanuni za kupiga kura kwa serikali za mitaa ambazo zilionekana kuwa ni uwozo mkubwa ambao umelenga kuisaidia chama cha CCM kushinda katika chaguzi hizo,
Kanuni ya chaguzi ya serikali ya mtaa imejaa ubabaishaji ambapo kwa vyovyote vile atakaeumia ni vyama vya upinzania ambazo wapiga kura wake wataonekana kama wakimbizi katika TAifa lao.
 
KANUNI INATAMKA WAZI KUWA MWENYE HAKI YA KUPIGA KURA NI MKAAZI WA KAWAIDA:
Hapa kwenye ukaazi wa kawaida ndipo kimbembe kilipo ambapo kanuni haisemi huyu mkaazi wa kawaida ni makazi wa muda gani???? je ni mwaka, miaka, miezi siku wiki ama masaa.
Huyu mkazi wa kawaida anathibitishwa na nani??, 
Maswali hayo ndiyo yatakayodhalisha watu kutoka mtaa mmoja kwenda mtaa mwingine kwa hoja kwamba ni mkaazi wa kawaida, CCM wanafahamu wazi kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kupata watu wao wanaowataka na huku wakiwakataza watu kupiga kura kwa kipengele hiko kuwa si waakazi wa kawaida,
Daftari lennyewe la kuandikisha wapiga kura nalo linamatatizo kibao ambapo kwa sauti moja wadau wa mkutano huo mjini Morogoro walikubaliana kuahirisha uchaguzi wa mwaka huu ili upangiwe wakati ambapo watu watajiandaa kufanya chaguzi hizo za mitaa,
Kwa kanu hiii, Mweneyekiti huyo wa Adc amekiri kuiona vurugu kubwa ambayo itaibuka huku wa kuzuia vurugu hiyo asiwepo,
Hapo ndipo Abdallah akakili kuwa ni wazi mchakato u,meharakishwa ni kama wa zimamoto huku wachezaji wake hajajiandaa kupigana vizuri na hapo ndipo CCM itakapiga magoli ya mbali na kuibuka washindi wa jumla katika mpambambano huo.
 SAKATA LA UKAWA KUUNGANAASEMA NI DANGANYA TOTO,
Aidha katika hatua Nyingine mwenyekiti huyo hakusita kusemakuuzungumzia mashirikiano ya hivi karibuni kati ya chama cha CHADEMA, CUF, NCCR na vingine vyo kuwa ni danganya Toto kwani si rahis kwa CUF kumuachia Chadema kushika nchi huko Zanzibar,
Aidha Abdala ameenda mbele zaidi na kusema si ajabu kuuna watu hao wakiungana kwani mpaka sasa tayari washaungana mara ya sita na hakuna muungano ambao umedumu kwa muda mrefu bila misukosuko
Sisi Adc tunaamini kuwa muungano ni njia nzuri ya kumuondoa adui lakini ni lazima mpange namna ya kufanya mashirikiano hayo, sio leo mnaungana alafu mnaonyesha dhana zenu na namna ya kuiondoa ccm, hivyo sio njia nzuri kwani CCM watajipanga na kushinda pambano mapema, kwa tafsiri nyingine ukawa wamewahi sana kuungana, wangesubiri baadae ndipo waungane tena kwa kuwashirikisha wanachama wao
Mimi nashangaa vyama vya siasa hapa Tnaznaia vinakaa kuangalia kipanzi katika jicho la mwenzake kumbe yeye ana bolt, wanasema muungano kati ya Tanganyika na Zanziba si wa wananchi ni wa viongozi mbona sasa wao wanafanya muungao wa kiungozi na si wa wananchi, kama tunawapa nchi hawa si watauza watu wote humu aliongeza Abdalal,
Chama ambacho kinaamini mamalaka ya wanachama kingeweza kukaa na wanachama wake ndipo wangeamua kuingia katika makubalianao,
Aidha alipoulizwa kama yeye ataungana na vyma sitta ambavyo vimeungana hivi karibuni kuwashinda UKAWA NA CCM, ametoa jibu moja tu kwamba hajashirikishwa katika kila hatua. Anaamini