Friday, 21 November 2014

KESI YA MADAI DHIDI YA MAOFISA WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KUDAIWA KUIFUNGA KLINIKI YA FOREPLAN HERBAL YAWAVUTA WATU WENGI

 Mawakili kutoka Kampuni ya Kamanija and Company Advocates,  wanao mtetea Dk. Juma Mwaka katika kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya maofisa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wanaodaiwa kuifunga Kliniki ya ForePlan Herbal iliyopo Ilala, inayomilikiwa na Dk.Mwaka, wakizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo, mara baada ya kusikiliza kesi hiyo ambapo itatolewa uamuzi Novemba 26 mwaka huu iwapo kama upande wa jamhuri utaunganishwa katika kesi hiyo. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Flora Haule. Kutoka kulia ni Wakili Charles Kamanija, Ngassa Ganja na Revocatus Thadeo.
 Mawakili hao wakibadilishana mawazo kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo ambayo imewavuta watu wengi wakiwepo wanahabari kutokana na unyeti wake.
 Wakili wa Serikali, Karim Rashid akizungumza na wanahabari kuhusu kesi hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

Wananchi mbalimbali wakisubiri kusikiliza kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment