Monday, 10 November 2014

HUU NI UZALENDO AU KICHEKESHO?,WATANZANIA WANAKUFA KWA KUKOSA DAWA WATAWALA WANATIBIWA NJE.SOMA HAPA KUJUA ZAIDI




Na Karoli Vinsent
Afya ya taifa ipo mashakani,uhakika wa uhai upo mashakani vile vile kwa kuwa hata kutumbuliwa chunusi ni lazima upande ndege kwenda ulaya.Ni hali tete kwa kuwa serikali ni mdeni sugu anaye daiwa na MSD zaidi ya bilioni 90 kiasi cha kusitishiwa kupewa mgawo wa madawa,ambao waathirika wakubwa ni wananchi labda ndo maana hata rais wetu ameamua kutumia kodi za wananchi kwenda kufanyiwa operesheni ya tezi ya uzazi ilihali tuna madaktari bingwa na hospital nyingi za rufaa zingeweza kuifanya kazi hiyo,kwa kuwa MSD wamegoma kutoa dawa.

Hali ni tete kweli kweli,pamoja na uchangiaji wa gharama za matibabu lakini serikali bado inadaiwa mabilioni hayo ya shilingi,kuna nini kwa nchi yetu ikiwa kila kukicha serikali ni mdeni sugu ambaye anayeathirika na madeni hayo ni mwananchi wa hali ya chini,Kimantiki serikali inawaaminisha wananchi wake kuwa wakiugua ni lazima wafe hata kama muda wao wa kuishi duniani haujamalizika.

Kuna haja gani basi ya kuwa na hospital za rufaa ikiwa haziwezi kutibu viongozi wetu ilihali kila siku tunamsikia rais akiinadi sera ya afya kuwa imeboresha afya ya taifa kwa serikali kuweza kuagiza vifaa mbalimbali vya gharama kubwa kwaajili ya kutibu wananchi.

Mbona serikali inatutonesha kidonda cha Dr. Ulimboka ambaye alihukumiwa kwenye mahakama ya Mwabwepande kwa kosa la kuwashawishi madaktari kugoma kwa kuwa hospital zetu hazina sifa za kuitwa hospitali, kwa kukosa vitendea kazi kiasi cha rais wetu kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa ugonjwa ambao hata hospitali ya wilaya ya Manyoni ingeweza kumtibu.

Uko wapi uzalendo wa washauri wa rais na daktari wake ikiwa hospital ya Muhimbili imeshindwa kutatua tatizo la afya ya viongozi wetu,kwa hali hii tuna wakati mgumu kama taifa.

Tumuombe Mungu sana atujalie akili ya kupembua mambo kwa hekima na kuhoji adha hii inayo sababishwa na serikali hii sikivu, ambayo hospitali zetu hazina dawa ndo maana kiongozi wetu mkuu amekimbilia nje ya nchi kujinusuru asije kukumbwa na adha ya kusubiri MSD walipwe deni na serikali yake anayo iongoza ndipo dawa zitolewe.

Mimi sipingi kutibiwa nje ya nchi kwa rais wetu laa,nasikitika kuwa ametumia kodi zetu kwa gharama kubwa sana ilhali Muhimbili wanaweza kutatua tatizo hilo. Lakini kikubwa nini ujumbe wa serikali hii kwa wananchi wake kwa hospitali zetu kukosa dawa na wakati huo huo kushindwa kuchunguza afya za viongozi wetu ilihali tunazalisha madaktari bingwa kila mwaka kwa gharama za kodi za wananchi ilihali hawana tija kwa afya ya taifa

No comments:

Post a Comment