Na Karoli
Vinsent
KATIBU mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa na Waziri mkuu
aliyejiuzuru na Mbunge wa Monduli Edward lowassa wameibuka kuwa wanasiasa wanapendwa
zaidi nchini.
Na pia wanasiasa hao wametajwa kupewa
nafasi kubwa ya kumruthi Rais anayemaliza mdawake, Jakaya Kikwete kwenye
uchaguzi Mkuu mwakani 2015.
Hayo yamegundulika leo Jijini Dar Es
Salaam, wakati wa uzinduzi wa Utafiti uliofanywa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali
la TWAWEZA ambapo utafiti huo ulifanyika kwa lengo la kuwaoa sauti watanzania
kuelekea uchaguzi mkuu na kuwahoji watanzania kuhusu hali ya kisiasa nchini
pamoja na mambo mbalimbali yanawazunguka,uzinduzi huo ulishuhudiwa na watu mbalimbali wakimemo
wanasiasa na waandishi wa habari,
Ambapo Akisoma Utafiti huo Ervis Mushi,ambaye ndio amesimamia suala hilo
amesema utafiti huo ulianza mwaka 2012
na kumalizika mwezi Agosti mwaka huu na kusema kuwa katika utafiti huo
wamewahoji watu Elfu 1500,na wametumia njia mbalimbali kukusanya maoni ya
utafiti huo ikiwemo nia ya simu na kuwafuata wananchi walipo.
Bwana Mushi alisema kwaanzia mwaka 2012
waliwahoji watanzania katika utafiti huo kama endapo uchaguzi mkuu ungefanyika
mwaka huo nani angefaa kumrithi Rais anayemaliza mda wake Jakaya Kikwete ambapo
Dk Wilbroad
Slaa alipata asilimia 19%
Mizengo panda
alipata asilimia 16%
Edward
Lowassa alipata asilimia 6%
Profesa
Ibrahimu lipumba alipata 3%
Nawasiojua nani
watamchagua walikuwa asilimia 22%
Bwana Mushi
alisema mwaka 2013 walifanya utafiti bado Katibu huyo wa Chadema alizindi
kuongoza akiwaacha wanasiasa kutoka vyama vingine nchini ambapo mambo yalikuwa
hivi
Dk Wilbroad
Slaa alipata asilimia 19%
Edward
Lowassa alipata asilimia 13%
Mizengo panda
alipata asilimia 12%
Profesa
Ibrahimu lipumba alipata 6%
Nawasiojua nani
watamchagua walikuwa asilimia21
Mwaka 2014
Edward
Lowassa alipata asilimia 13%
Dk Wilbroad
Slaa alipata 13%
Mizengo panda
alipata 12%
Profesa
ibrahimu lipumba alipata 6%
Freeman
Mbowe alipata 3%
Nawasiojua nani
watamchagua walikuwa asilimia 33%
Kwa upande
wa Mgombea ambaye anakubalika ndani ya chama cha mapinduzi CCM ambaye amepata
alama nyingi ili kuweze kumrithi Rais anayemaliza mda wake Profesa Jakaya
Kikwete,imeonekana Edward Lowassa akichuana vikali na Waziri mkuu Mizengi Pinda
Edward
lowassa amepata 17%
Mizengo panda
amepata 14%
John
Magufuli amepata 5%
Samwel Sitta
amepata 5%
Wasiokuwa na
upande ni 18%
Nao umoja wa
Vyama vikuu vya upinzania ambavyo vimeungana UKAWA wakati wa kumsiamisha mgombea mmoja kugombania
Urais imeoneka bado Dk Wilbroad Slaa ni kinara
Dokta
Wilbroad Slaa amepata 44%
Profesa Ibrahim
lipumba amepata 14%
Freemana
Mbowe amepata 11%
Zitto Kabwe
amepata 6%
Kuhusu chama
cha siasa kinachopendwa zaidi nchini hiko hivi
Mwaka 2012
Chama cha
Mpinduzi CCM-65%
Chadema
alipata 26%
CUF
ilipata 3%
NCCR Mageuzi
0%
Mwaka 2013
Chama cha
Mpinduzi CCM-54%
Chadema
alipata 32%
CUF
ilipata 4%
NCCR Mageuzi
1%
Wasiokuwa na
chama 8%
Mwaka 2014
Chama cha
Mpinduzi CCM-54%
Chadema
alipata27 %
CUF
ilipata 4%
NCCR Mageuzi
1%
Wasiokuwa na
chama 10%
Akizungumzia
Utafiti huo Profesa Benson Bana kutoka chuo Kikuu cha Dar Es Salaam
aliwapongeza Twaweza kwa utafiti huo na kusema ni wakati wa wanasiasa
kutafakali kwa umakini kuhusu utafiti huo na kuchukau maauzi ya mazuri katika
kuvijenga vyama vyao.
Na kuongeza
kuwa utafiti bado unaonyesha sana haiba ya mgombea binafsi
Katika hali
ya kushangaza Katibu wa Itikadi na Uenezi kutoka chama cha Mapinduzi CCM,Nape
Nnauye alionekana kama kutokubaliana na utafiti wenyewe na kujiondoa
kumzungumzia Edward Lowassa aliyetajwa sana na kujitita kusema wananchi wa sasa
wanaitaji matatizo yao ya msingi yatatuliwe na sio katiba.
No comments:
Post a Comment