Monday, 24 November 2014

TUCTA WAJITOSA KWA JK

Na karoli Vinsent

CHAMA cha Wafanya kazi nchini (TUCTA) nao wamejitosa Kwa  mara ya Kwanza kwenye sakata la Ufisadi wa zaidi ya bilioni 400 za kitanzania kwenye Akaunti ya Escrow na kusema  chama hicho hakiwezi kukubaliana na ufisadi huo na kuitaka serikali kuwachukulia hatua kali ya watu wate waliohusika na wizi.
    Na  kama endapo Bunge pamoja na serikali hawatawachukulia hatua zozote Viongozi waliohusika na wizi huo, basi TUCTA itachukua Jukumu la kuwaunganisha wakulima na wafanyakazi wa idara zote kushikilia bango suala hilo.
     Kauli hiyo kali imetolewa leo Jijini Dar Es Salaam na Rais Mpya wa Chama cha Wafanyakazi nchini TUCTA Gration Mukoba wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, ambapo Mukoba alisema wao TUCTA ambao nao pia ni walipa kodi nchini  hawawezi kukubaliana na wizi wa zaidi ya Bilioni 400 kwenye Akaunti ya Esrow.
“Kusema kweli sisi wafanyakazi tumechoka na hali ya Ufisadi unaoendelea nchini, na ukizingatia sisi TUCTA ni walipa kodi wakubwa sana ,tunasikitika sana kusikia serikali inaweza kusimamia mambo ya ufisadi yanayotokea maeneo  mbalimbali nchini, na sisi vyama vya Wafanyakazi nchini kwa pamoja tunaiomba serikali iwachukulia hatua kali sana Viongozi waliohusika kwenye wizi huu wa mali za umma”alisema Mukoba.
Mukoba aliongeza kuwa kwamba wafanyakazi nchini wanaishi katika mazingira magumu sana huku wengine bado wakiwa wananchukua mashahara mdogo ambao usioendana na hali ya maisha ya sasa na wanasikitika kusikia pesa zinaibwa  na watendaji wa serikali  na huku wakishindwa kuchukuliwa hatua.
      Aidha Mukoba aliwashangaa watu ambao wanasema pesa ambazo zimeibwa kwenye Akaunti ya Escrow kusema sio za umma bali ni za wamiliki wa Kampuni ya IPTL  na kusema sio kweli kwani  pesa hizo ni za watanzania wote, kwani zimechukuliwa kwenye shirika la Umeme nchini Tanesco.
       Vilevile TUCTA waliitaka Jamii kujiweka Tayari kuungana nao ili kuchukua maamuzi magomu kuhusu ufisadi huo na  kama endapo Serikali itashindwa kuwachukulia hatua Viongozi waliohusika kwenye wizi huo ambao haujawai kutokea tangu nchi kupata Uhuru.

No comments:

Post a Comment