Thursday, 20 November 2014

SHROSE BANJ AZIDI KUFANYA UJINGA KWENYE BUNGE LA EAC,AIABISHA SERIKALI CCM,ASHINDWA KUJENGA HOJA AISHIA KUPIGANA,SOMA HAPA KUJUA



Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutoka Tanzania Shy -Rose Banji (pichani) na Nderakindo Kessy, wanadaiwa kuingia katika mtafaruku wakiwa jijini Nairobi, Kenya katika vikao vya Bunge hilo.

Taarifa za tukio hilo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Shy-Rose anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kamkunji, Nairobi.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa sababu za kushikiliwa kwake ni baada ya kumkunja na kumpiga ngumi mbunge mwenzake na chanzo cha ugomvu hakijajulikana.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa Kessy ambaye anatoka NCCR-Mageuzi, alikumbana na kipigo hicho juzi jioni, Jijini Nairobi.

“Tumepokea taarifa kutoka kwa Wabunge wa Rwanda wakinieleza kwamba Nderakindo, amepigwa na mbunge mwenzake (Shy-Rose) na kuumizwa vibaya, tuliomba msaada apelekwe hospitali huku tukiendelea kuzungumza na mwanasheria aliyeko Nairobi tufungue kesi,” alibainisha Mbatia.

Hivi karibuni, Mbunge Nderakindo, alisikika akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kuhusu sakata la baadhi ya wabunge kutaka kumtimua Spika wa Bunge hilo, Dk. Margaret Zziwa, kwa madai ya kushindwa 

No comments:

Post a Comment