Na Karoli
Vinsent
CHAMA kipya cha
Siasa nchini cha Tanzania Tanzania Alliance for change and Transparency ACT kimezidi
kuvuna wanachama wapya kutoka vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda Umoja wa
Kutetea Katiba ya wananchi UKAWA vyama hivyo ni Chadema,CUF na NCCR- mageuzi ,baada
ya leo Viongozi mbalimbali kutoka vyama hivyo kuhamia kwenye chama hicho.
Wanachama hao ni aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa chama cha Wananchi CUF mkoa wa Ilala,Ramadhan Khamis na aliyekuwa
mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jimbo la
Korogwe na Afisa Habari Taifa wa chama hicho Tony Kamkanda
Akithibitisha kuwapokea wananchama hao
leo Jijin Dar es Salaam ,Katibu mkuu wa Chama
cha ACT-Tanzania Samson Mwigamba wakati wa Mkutano na Waandishi ambapo
Mwigamba amesema huu sio mwisho kwani
chama hicho kwanzia sasa kitapokea wanachama wengi tena viongozi wakubwa tu
kutoka vyama vingine vya siasa na akasema chama hicho kinawakalibisha wanachama
wote kutoka vyama vyote vya siasa nchini kuhamia kwenye chama hicho kupata Demokrasia ya kweli na yenye kulijenga Taifa
kimaendeleo.
“Nawakalibisha
sana wanachama wengine kuiga mfano wa wananchama hawa wapya kwani ACT ni chama ambacho
chenye nia ya dhati ya kuendeleza Demkokrasia ,na sisi tuko na tofauti na vyama
vingine vya upinzani ambavyo badala ya
kujenga chama vimekuwa vikiishia kuzungumza wahasisi na chama chetu hakina nia
hiyo bali kiko kwa ajiri na kumkomboa mtanzania wa leo”Alisema Mwigamba
Kwa upande
wake wanachama hao waliohamia ACT –Tanzania walisema wamehamia chama hicho
baada ya kuchoshwa na mifumo isiyokuwa na tifa na yenye kuua Domkrasia nchini
kwenye Vyama hivyo ambavyo wanadai viko kwa ajiri ya kutafuta pesa na sio
kumkomboa mtanzania wa leo mwenye matatizo lukuki.
Katika Hatuo Nyingine Chama Kipya cha
Siasa nchini kinatarajiwa kuzinduliwa Rasmi tarehe 5,desemba mwaka huu,na
kushuhudiwa na watu mbalimbali pamoja na vyama vingine vya kisiasa nchini.
Akizungumzia Uzinduzi huo Katibu Mkuu
huyo wa ACT-Tanzania Samson Mwigamba alisema licha ya uzinduzi huo pia chama
hicho kinatarajia kumfanya mkutano wake mkuu wa Mwaka unaotarajia kufanyika
Jijin Dar Es Salaam na kuwataka wananchi kukiunga chama hicho chenye malengo
mazuri kwao.
KUHUSU
MWIGAMBA KUFUKUZWA ACT-TANZANIA
Mwigamba
alisema hawezi kufukuzwa ACT kwani yeye
yupo hapo kisheria na wanao sema hivyo na malalamiko yapo chama hicho kitachukua hoja zao kama mapendekezo ya
kukijenga chama hicho na kusema chama hicho hakina wahasisi kama wanavyodai .
No comments:
Post a Comment