Makocha 35 wameteuliwa kushiriki kozi ya ukocha ya
Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika mjini
Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.
Kozi hiyo itaendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday
Kayuni na itafanyikia Mchikichini College ambapo washiriki wote wanatakiwa
kuwasilisha vyeti vyao vya ukocha vya ngazi ya Kati (Intermediate) pamoja na
vyeti vya kitaaluma vya elimu ya sekondari (academic).
Washiriki wa kozi hiyo ni Abdulmaliki Nemes (Airport
FC), Ahmed Haule (Kilimanjaro Talented Youth Sports Centre), Ally Jangalu (Moro
Kids), Amri Saidi (Mwadui FC), Athuman Kambi (Morogoro), Charles Mwakambaya
(Burkina Faso FC), Damian Mussa
(Alliance One) na Daudi Sichinga (Kasulu United).
Denis Maneva (Shule ya Msingi Logo), Edgar Juvenary
(JUT- Mlale), Hamisi Mangolosho (Shule ya Msingi Mtimbwilimbwili), Henry Ngondo
(Chalinze Academy), Issa Hamisi (Polisi Kilimanjaro), Jumanne Chale (Dar es
Salaam), Kizito Mbano (Masasi Alliance), Martin Saanya (Magereza Morogoro) na Masoud
Gumbwa (Sokoine University Academy).
Mbwana Makata (Oljoro JKT), Mrage Kabange (Kagera
Sugar), Muhibu Muhibu (Stand United FC), Nsubuga Solomon (Kishoto FC), Nyamtimba
Muga (Kizuka Secondary), Oscar Mirambo (Makongo), Rashid Abdallah (Tech Fort
Academy), Renatus Shija (Rhino Rangers), Safari Nyerere (Elimu Sports Academy)
na Said Lyakuka (Kizuka Stars).
Simeon Mwesa (Mtibwa Sugar U20), Simon Shija (Tabora),
Suleiman Mtungwe (Ruvu Shooting), Swalehe Allawi Abdul (Alliance Academy),
Yasin Bashiri (Kick Off Sports Academy) na Zuberi Katwila (Mtibwa Sugar).
Wakati huo huo, kutakuwa na kozi ya wiki mbili ya ukocha
ya ngazi ya Kati (Intermediate) itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia
Desemba 29 mwaka huu.
Makocha wote wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma
maombi katika Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA).
No comments:
Post a Comment