.
Ripoti
ya kashfa ya fedha zilizochotwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow
zaidi ya Shilingi Bilioni 300 kutoka Benki Kuu (BoT), imewasilishwa
Bungeni mjini Dodoma hii leo na kusomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe na Makamu wake Deo Filikunjombe
kusoma mapendekezo ya Kamati hiyo dhidi ya wote waliotajwa katika
sakata hilo.
Katika
mapendekezo yake miongoni mwa viongozi wa juu wa Serikali waliotolewa
maamuzi kuwa wajiuzulu nyadhifa zao za kuteuliwa na kuchaguliwa ni
pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Katibu Mkuu wa
Nishati na Madini, Elaichim Maswi.
Pia katika orodha yao wapo viongozi wa dini na wanasiasa ambao walichota fedha hizo za umma.
No comments:
Post a Comment