Dr. James Benedict Diu akifafanua jambo katika mkutano wa wadau, Diu ni Mkurugezni uchumi wa mamlaka hiyo. |
Wadau wakijadili jambo katika kikao hicho cha wadau wa usafiri mapema hii leo. |
Mamlaka ya Anga hapa nchini imeendelea
kuonyesha nia yake ya kuhakikisha kuwa wazawa wanakuwa mstari wa mbele
kutumia huduma za ANGA ambazo kwa muda mrefu wageni wameonekana kushika
hatamu katika huduma hiyo,
Akizungumza katika mkutano maalum wa
kujadili changamoto za usafiri wa Anga katika mkutano wa wadau wa
usafiri hapa nchini, Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Anga TCAA Bw.
Charles Chacha amesema kwa sasa watanzania bado hawajaamkuka kutumia
huduma ya usafiri wa anga,
Amesema kikwazo kikubwa kwa watanzania
hao kushindwa kutumia usafiri huo ni kutokana na Ada ya kusafiri kutoka
sehemu moja kwenda nyingine, Lakini amewahakikishia wananchi kuwa
mamlaka yake imejikita kuhakikisha kuwa changamoto hiyo inamalizwa na
hivyo kuwa na bei ambayo kila mtu anauwezo nayo,
Chacha ameenda mbele na kusema kuwa
kwanza wao kama mamlakayenye dhamana ya kudhibi mifumuko ya bei kwa
wasafiri, wamejipanga kuhakikisha inaleta makampuni mengi ya ndege ili
kuongeza ushindani katika soko hilo la usafiri wa anga hapa nchini,
Mipango mingine ni kuhakikisha kuwa
viwanja vyetu vinajengwa miundo mbinu mizuri itakayovutia watoa huduma
kuanza kufanya kai masaa 24 ili kutoa fursa kwa wazawa nao kufaidi
huduma za ndege
Alipoulizwa swali kuwa wanafanya nini
ili kuongeza idadi ya watu wanaotumia uafiri huo kuongezeka, kutoka
idadi ya sasa, Mkurugenzi huyo amekiri kuwa bado ni changamoto ingawaje
kwa sasa tunaviwanja takribani mia tano 500lakini bado ndege zetu
zimekuwa zikilala usiku kama binadam anavyolala na hilo ni tofauti na
nchi zingine ambazo ndege zimekuwa zikikesha kutokana na viwanja vyao
kuwa na taa zinazoruhusu kufanya hivyo,
Katika hatua nyingine, mkurugenzi
anayeshugulikia uchumi na udhibiti kutoka mamlka ya ANGA HAPA NCHINI Dk
James Diu amebainisha baadhi ya changamoto ambazo kwa sasa zimekuwa ni
kubwa katika viwanja vyetu ni kwamba watendaji bado hawana ujuzi mzuri
wa kufanya kazi,
Ufanisi wa wafanyakazi katika viwanja vyetu bado ni changamoto hususani wakaguzi ambao pengo lao linaonekana hadharani,
Nye katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi
wa Anga, Bw. Laurance PAUL ameelezea masikitiko yake juu ya serikali
ambapo wameamua kuacha sekta mbili muhimu kuziunganisha ili kufanya
ndege zetu zifanye kazi usiku na mchana,
AKizungumza n mtandao huu katika
mahojiano maalum, Kati bu huyo amesema ili ndege zetu ziweze kufanya
kazi masaa 24 kama nchi zingine ni lazima sekta ya utalii iunganishwe na
usafiri wa nga ili kupata wateja wengi,
Pili viwanja vyetu ni lazima vijengwe
taa ambazo zitawaruhusu watoa huduma kufanya kazi zao katika nyakati za
usiku kkama nchi zilizoendelea kiuchumi,
Sisi watanzaia tunaviwanja vingi sana
kiasi kwamba kama tunavitumia ipasavyo na tukishusha bei watanzania
wengi wataanza kutumia usafiri wa nga.
No comments:
Post a Comment